FT: Esperance 0-0 Al Ahly | CAF Champions League Final | 1st Leg | Stade Olympique Hammadi Agrebi | 18.05.2024

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
21,158
46,256
Mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika unapigwa leo katika dimba la Olympique Hammadi Agrebi baina ya wenyeji Esperance dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Saa 4:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki.

Updates ==================
30’ Esperance 0-0 Al Ahly
Bado timu zote zinasomana

Al ahly ameamua kupaki basi muda mwingi anacheza kwenye zone yake

32’ Hakuna timu iliyolenga goli mpaka sasa

34’ Esperance wanapata faulo lakini wanashindwa kutumia nafasi

36’ Esperance 0-0 Ahly, timu zimekamiana sana

37’ Kuumia kwa Maaloul dakika za mwanzoni ni kama kumeleta pengo kwenye kikosi cha Ahly

40’ Esperance wanapata faulo nje ya 18 ya Al Ahly lakini wanapaisha

41’ Al Ahly mpaka sasa washacheza faulo 6 huku Esperance akicheza faulo mbili

43’ Esperance wanajitahidi kufika langoni mwa Al Ahly ila wanakutana na changamoto ya ukuta mgumu wa Ahly

45’ Mwamuzi anaongeza dakika 2 kabla ya mapumziko

HT’ Esperance 0-0 Al Ahly

2nd half imeanza…

55’ bado timu hazijafungana

56’ Hussein El Shahat (Al Ahly) anapokea pasi nzuri na kutoka nje kidogo ya eneo la hatari anaachia shuti kali, lakini shuti hilo linazuiwa na beki.

60’ Hakuna timu iliyopata shot on target hata moja
Esperance 0-0 Ahly

62' Emam Ashour (Al Ahly) anaenda kwa goli kwa shuti la mbali, lakini juhudi hizo hupaa nje ya lango la kulia.

65’ Esperance 0-0 Ahly

69' Houssem Teka anatoka nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na Zakaria El Ayeb (Esperance Tunis).

69' Mohamed Ben Ali anaondoka na Miguel Cardoso anatoa maagizo ya mwisho ya kimbinu kwa Raed Bouchniba (Esperance Tunis).

71' Kadi ya njano inatolewa kwa Rodrigo Rodrigues (Esperance Tunis).

75’ Al Ahly wanaamua kurudi nyuma sasa na kupaki basi

80’ Esperance 0-0 Al Ahly

Hakuna shot on target mpaka sasa🤣

81' Mwamuzi anasimamisha mchezo ili abadilishwe na Emam Ashour atoke nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na Afsha (Al Ahly).

85’ Esperance 0-0 Al Ahly

90’ Refarii anaongeza dakika 5

Esperance 0-0 Al Ahly

Al Ahly wanafanikiwa kupata shot on target ya kwanza

FT’ Esperance 0-0 Al Ahly

Fainali ya Mkondo wa Pili itapigwa 25/05/2024 pale Cairo
 
1716056685606.png

Leo Esperance De Tunis watakuwa uwanja wa nyumbani Hammadi Agrebi wakiwakaribisha Al Ahly katika fainali ya ligi ya mabingwa Afrika mechi ya mkondo wa kwanza

Ni Esperance de Tunis ama Al Ahly nani kuanza kuonja harufu ya ubingwa?

Uzi huu utakuwa live muda wote wa mchezo, stay tuned.

1716056980880.png

Kikosi cha Al Ahly kinachoanza
 
Back
Top Bottom