Escrow tuachane nayo,tufanye mengine

Escrow tuachane nayo,tufanye mengine

Sikubaliani na wazo hilo. Hao ni wahalifu na lazima pesa waliyoiiba irudishwe na wahalifu hao kufikishwa mahakamani....wote bila kujali mtu. Utawala bora ukija uhakikishe hilo kwa sababu makosa hayasauliwi, hayasamehewi, hata ichukue miaka mingapi.

Hapa kaka ni kusubiri mpaka Mkulu atoke maana yeye ndiye aliyeratibu,akaidhinisha,akalipwa, na akawapa wengineili kuwafunga midomo.

Sasa kesi ya NYANI utampa ngedere kweli?Kwa sababu mnufaikaji wa kwanza ni MKULU ndiyo maana Mzee Tupatupa katuambia bora tunyamaze tugange yajayo.

Ukifika wizi mwingine tutapiga kelele yataisha,utakuja mwingine vivyo hivyo.Cha msingi wenye pesa zao wandelee kuzifungia mpaka VIONGOZI wetu wapate akili ya kujua mema na mabaya.
 
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.

Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.

Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.

Escrow is extremely complicated. Limekwama.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Nadhani uko sawa. Tuamue kimyakimya. Hakuna cha ziada.
 
Naona vikao vya chama vimeishafikia uamuzi kumtoa sadaka AG maana sio mwanachama mwenzao
 
Hapa kaka ni kusubiri mpaka Mkulu atoke maana yeye ndiye aliyeratibu,akaidhinisha,akalipwa, na akawapa wengineili kuwafunga midomo.

Sasa kesi ya NYANI utampa ngedere kweli?Kwa sababu mnufaikaji wa kwanza ni MKULU ndiyo maana Mzee Tupatupa katuambia bora tunyamaze tugange yajayo.

Ukifika wizi mwingine tutapiga kelele yataisha,utakuja mwingine vivyo hivyo.Cha msingi wenye pesa zao wandelee kuzifungia mpaka VIONGOZI wetu wapate akili ya kujua mema na mabaya.

Hukunisoma vizuri, nimesema utawala bora ukiwepo washughulikiwe. Tunaona mpaka siku za karibuni wauaji wa Nazi wa Hitler wakisakwa na kuhukumiwa kwa makosa waliyoyafanya miaka 1945!! Inawezekana kabisa kuwatia hatiani kama nia ipo!
 
Nasisitiza tuachane na masuala ya Escrow

Mzee Tupatupa
 
yaan ni escrow sawa na jambazi sugu linalosumbua mji then unawaambia polisi waache msako kwa kuwa eti lipo mafichoni!
 
kinaeleweka taratibu dhambi zao hazitasahaulika mioyoni mwetu.miaka 100.
 
Unfair end to Professor Tiba, very unfair. Rais alikuwa haongei kama rais, alikuwa anaongea kama mtu ambaye amejikuta tu katika hiyo position. Hata kumtoa can be very easy. But the unknowns is what keeps many afraid. Hii ya leo kama ile speech ya mei mosi ya mwaka uleeee!

But for sure somebody will pay for this mess. The first to pay is a poor Tanzanian who cannot afford private services (education, health, etc). The second to pay is you and me. Even if we can afford private education and health, there is a consequence like currency depreciation that is going to erode our purchasing power. We can put our hope in opposition, but again in there there are still a lot of "unknown unknowns and known unknowns"
 
This is the sum total of our capacity as as a country. Our president is the best that we could produce. CCM is our leaders' cooking machinery. If that was the best that CCM could produce, understand that's what we deserve as a nation. I still believe that we get leaders we deserve. We don't get leaders that we want. The current man in state house is the leader we deserve as a nation.
 
Kwa kuwa tuna mgogoro na mhimili wa mahakama.

Na mimi nashida na mhimili moja tayari, nisaidie namna ya kufanya fomulashen nzuri. Waheshima wabunge lazima tuwe makini hapa. Haya maneno yaliniudhi kuliko maneno yote yaliyosemwa ndani ya Bunge siku hiyo.
 
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.

Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.

Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.

Escrow is extremely complicated. Limekwama.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Halipo complicated hata kidogo. Gumu lilikuwa Meremeta na Kagoda kwasababu jamaa alikaa kimya. Hata akiulizwa hajibu kitu.

Hili amejianika.....na sasa anasingizia yezi dume..mara mshono....mara siwezi kukaa.

Tutaliacha lakini hili ndo rahisi zaidi kutokea....wizi wa wazi kabisa ndo huu.
 
Hukunisoma vizuri, nimesema utawala bora ukiwepo washughulikiwe. Tunaona mpaka siku za karibuni wauaji wa Nazi wa Hitler wakisakwa na kuhukumiwa kwa makosa waliyoyafanya miaka 1945!! Inawezekana kabisa kuwatia hatiani kama nia ipo!

Unisamehe,ila maana yangu kukujibu,huo utawala bora hauwezi kuwepo ikiwa mshughulikiaji wa huo UTAWALA BORA naye ni mmoja wa wezi wa mali za umma.

Ndiyo maana nikasema labda utawala huu ukiondoka utakaokuja utaweza kuziba mapengo haya.Kwa sasa kaka RAIS hatuna,Mahakama wala Bunge,tupotupo tu kama Mbuzi tusio na mchungaji.
 
Saizi ndiyo nimegundua hii issue ya Escrow ni zito sana.

Ni zito sana ZIGO lA ESCROW,sababu MKULU anapima maji kwanza,kamamarefu au la!Kumbuka kuna waliojiapiza,kuna wale waliobeba kwa mifuko pesa,kuna wengi walio ndani ya BLACK haouse pale magogoni.Nyumba isiyo na hadhi ya kuitwa WHITE HOUSE.
 
Back
Top Bottom