Escrow tuachane nayo,tufanye mengine

Escrow tuachane nayo,tufanye mengine

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.

Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.

Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.

Escrow is extremely complicated. Limekwama.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Hoja imekubaliwa na kuungwa mkono.
Sasa nitawahoji wanaoafiki waseme ndiooooooo... na wasioafiki waseme sio.
Nadhani waliosema ndio wameshinda.
 
sasa tutaachana na mangapi...tumeachana na richmond, epa, deep green, meremeta, na hili pia.... hell no...
 
Kuendelea na escrow ni kutaka kuleta uhaini ktk taifa sababu mtuhumiwa namba moja ni mkulu. Sioni ni jinsi gani litaisha na mkuu akabaki salama.
 
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.

Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.

Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.

Escrow is extremely complicated. Limekwama.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ungeshauri watanzania tubadili utaratibu wa kushughulika na mambo kama ESCROW ningekuelewa zaidi...

Mfano ungeshauri tuanze kuyatumia vema masanduku yetu ya kura katika kushughulika na hawa jamaa.

Maana tunajitoa ufahamu kwa kuwasubiri wezi wajihukumu wenyewe.
 
Naunga mkono hoja, tuliache kwa muda, halafu tutalifufua zikianza kampeni za uchaguzi mkuu 2015.
 
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.

Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.

Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.

Escrow is extremely complicated. Limekwama.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hapana, mtujulishe kwanza. Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. Rais akikataa kutekeleza maazimio ya bunge, nini kinapaswa kufanywa na bunge? Hauwezi kuanzishwa mchakato wa impeachment?
 
Sikubaliani na wazo hilo. Hao ni wahalifu na lazima pesa waliyoiiba irudishwe na wahalifu hao kufikishwa mahakamani....wote bila kujali mtu. Utawala bora ukija uhakikishe hilo kwa sababu makosa hayasauliwi, hayasamehewi, hata ichukue miaka mingapi.
 
Hoja imekubaliwa na kuungwa mkono.
Sasa nitawahoji wanaoafiki waseme ndiooooooo... na wasioafiki waseme sio.
Nadhani waliosema ndio wameshinda.

Hii bado mkuu tunatafuta Formulation
 
haswa.mbia simba trust ndo mwenye project nzima ya escrol na chakushangaza ndiye mkuu wa nchi.alafu unategemea nani awajibishwe kwa project ya mtu.yeye kama raisi atoke madarakani kwa kuwa ndie mwenye project ya escrow.pamoja na project zote zilizopita za kuifilisi nchi hii.hakika jakaya kikwete ni kiongozi mbinafsi sans.
 
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.

Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.

Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.

Escrow is extremely complicated. Limekwama.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Kuachana na escrow ni uzembe mkubwa sana na unafki pia. Wachagga wanasema mwanaume haogopi vita ambayo haijapiganwa bado.

Hatuwezi kukata tamaa kirahisi namna hiyo. Namnahii hawa jamaa watazoea, we should fight them to death!
 
Nakubaliana na wazo ingawa sio zuri. Nakushauri uielekeze mahakama itoe pingamizi kwa nchi wahisani ili kuzilazimisha ziendelee kuchangia bajeti yetu.
 
kumtoa mkulu ni mgumu ktk vitu anafikiria sana ni jinsi ya kuweka vzr usalama wake! Mboma aliyekuwa mkuu wa jeshi kwenye ngao wa ESCROW yumo vizuri, huyu wa sasa na wakubwa jeshini wanasubilia nafasi kama hizo wakistafu!
kwa ufupi ktk kiwango kama hiki cha crisis ya ubafhilifu ungetegemea kuona mchango wa jeshi, mfano ni jeshi la misri! lakini si la tanzania, wao wanaonekana mtu akivaa nguo zao tu! si ktk kutetea na kulinda maslahi ya kiuchumi wa watz!
 
Bora huyo mkulu akatolewa tu kuliko kufuga mwizi.

Kutolewa madarakani ndiyo hatua pekee iliyobaki walau kunusuru kidogo taifa,lakini ni kwa njia ipi mkuu...? Bunge la akina Mariam Kisangi,Komba,assumpta mshama,mwijage....! Hapo sahau,labda kwa njia nyingine ya umma.
 
Back
Top Bottom