BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Escrow kuiadhiri CCM
HARAKATI za Chama cha Mapinduzi(CCM),kutaka ripoti ya uchunguzi wa akaunti ya Tegeta Escrow, isijadiliwe bungeni huenda zikagonga mwamba, Tanzania Daima Jumapili, limebaini.
Jitihada hizo zinaweza kutoweka baada ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kukamilisha uchunguzi wake na anatarajia kuwasilisha ripoti hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali inayoongozwa na Zitto Kabwe.
Iwapo ripoti hiyo itawasilisha, inaweza kukipasua Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikituhumiwa kwa kulea na kulinda ufisadi
Tanzania Daima Jumapili, lilidokezwa kuwa CCM inahofia ripoti inaweza kuwagusa vigogo, mawaziri na watendaji wa serikali ambao itamlazimu Rais Jakaya Kikwete, kulivunja baraza la mawaziri.
Inaelezwa kwamba, ripoti hiyo huenda ikawagusa baadhi ya mawaziri waandamizi wa serikali na viongozi wa CCM miongoni mwao, ni wale walioanza harakati za kuwania urais katika uchaguzi ujao.
Kufikishwa bungeni kwa ripoti hiyo, kunatabiriwa litakuwa anguko jingine kwa serikali kama ilivyokuwa mwaka 2008 alipong'oka Waziri Mkuu Edward Lowassa kwa kashfa ya kutoa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa timu ya Richmond.
Kashfa hiyo ya Richmond ilitengeneza uhasama miongoni mwa makada wa CCM hata kukifanya chama hicho, kipoteza majimbo mengi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Mbali na Richmond kukitesa CCM na serikali pia uhasama wa makada wake umekijengea makundi yanayotishia uhai wake.
Vigogo wa CCM na serikali yake hawataki ripoti hiyo iwasilishwe bungeni kwasababu itawaweka katika wakati mgumu wa kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Disemba mwaka huu.
Katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), ya CCM kilichokaa hivi karibuni mjini Dodoma suala hilo liiibuka ambapo Christopher ole Sendeka, anadaiwa kusimama katika kikao hicho na kueleza wazi kuwa chama chao kinachafuliwa na ufisadi wa IPTL na kwamba fedha hizo zinatumika Dodoma kwenye kampeni za urais.
Madai ya Sendeka, yalizimwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, akisema kuwa suala la IPTL waliache kwanza maana wanasubiri ripoti ya uchunguzi unaoendelea hivi sasa.
Hata hivyo wakati hali ikionekana kuwa tete, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge na hesabu za serikali (PAC), Zitto Kabwe,ameshamuandikia barua CAG, kumueleza umuhimu wa ripoti hiyo.
Zitto alisema suala hilo lazima litafika bungeni hata kama CCM hawataki jambo hilo lifike, kwa
sababu kamati yake ndiyo yenye jukumu la kufanyia kazi na kulipeleka huko.
Alisema CAG alitakiwa kutoa taarifa ya uchunguzi huo wiki iliyopita lakini aliomba apeleke taarifa wiki hii.
"Tukishakutana na CAG wiki hii, suala hili litajadiliwa kwenye vikao vya Bunge la 17 au 18, kulingana na mpangilio wa shughuli za Bunge, hili haliwezi kukwepeka"
"Sisi kazi yetu ni kulifikisha bungeni suala hili na wabunge wana uamuzi…hili la kuzuia sidhani kama litafanikiwa" alisema Zitto.
Zitto alibainisha kuwa Oktoba 24 mwaka huu, alimuandikia barua CAG akimueleza umuhimu wa ripoti hiyo kwa taifa.
Katika barua hiyo ambayo Tanzania Daima Jumapili, imefanikiwa kuiona Zitto anasema uchunguzi wa ripoti hiyo utaiokoa nchi na mpasuko unaoweza kujitokeza baada ya wafadhili wa serikali kuacha kutoa misaada kwa Tanzania mpaka ripoti ya Tegeta Escrow itakapowekwa hadharani.
Sehemu ya barua hiyo inasomeka "Kamati imejulishwa na wizara ya fedha na Benki Kuu kwamba uamuzi wa wafadhili kuzuia misaada ya kibajeti unaathiri sana utekelezaji wa bajeti,
Sharti la kutolewa misaada hiyo ni taarifa hii kutolewa kwa vyombo vilivyoomba, kuendelea kuchelewa kutoa taarifa kutaumiza zaidi wananchi kwa kukosa dawa hospitalini na hata mishahara kukosekana"iliandikwa.
Barua hiyo imeongeza kuwa gavana wa Benki Kuu ameijulisha kamati kuwa serikali imeanza kukopa katika soko la ndani na kuathiri uchumi kwa kushindwa na sekta na hivyo kuongeza riba na kusababisha uchumi wa nchi kusinyaa.
Mbali na Zitto, mbunge wa Kigoma Kusini,David Kafulila alisema ripoti hiyo isipowasilishwa bungeni atawasilisha hoja binafsi ya kutokuwa na imani na serikali.
Kafulila alisema anaamini ofisi ya CAG inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa vigogo wakubwa serikalini wanaohusika na ufisadi huo.
Alisema uhakika wa jambo hilo unadhihirishwa na muda alioutumia CAG ni zaidi ya ule alioomba bungeni kwamba kazi hiyo ingekamilika baada ya siku 45 na kwamba mpaka jana ni zaidi ya siku 200 zimepita huku ripoti hiyo ikiwa imekaliwa.
"Nashangaa PCCB wamemaliza kazi na kwenda kuikabidhi Ikulu badala ya kumfikishia mwendesha mashtaka(DPP), ili aweze kuwachukulia hatua wahusika kwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, Hosea anapaswa kuwasilisha ripoti yake bungeni kwa sababu aliagizwa na Bunge na siyo Ikulu"alisema Kafulila katika ujumbe mfupi wa simu kwa gazeti hili.
Sakata la Escrow liliibuliwa na Kafulila Mei 8 mwaka huu akiwa bungeni mjini Dodoma na kuwatuhumu baadhi ya vigogo wa serikali kuwa nyuma ya uchotwaji wa dola za marekani kiasi cha milioni 122 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 200.
Vigogo waliotajwa na Kafulila ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospiter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Beno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Kafulila alisema vigogo hao wamehusika na ufisadi wa fedha hizo zilizokuwa zimewekwa katika akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (ESCROW) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, Chakaza, Elly B, MziziMkavu, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, August, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi
- Zitto asema ripoti yake haizuiliki
- CAG kuanika madudu wiki hii