Akilazimishwa kuzirudisha tutamchangia tu, ni askofu wetu. Maaskofu wetu wanaishi ndani ya jamii ya waumini na wanategemezwa na waumini wao, akiwemo huyo James Rugemalila. Askofu wa kikatoliki hana familia binafsi inayoweza kufaidika na chochote anachopewa, familia yake ni sisi waumini, na nina uhakika fedha hizo alizitumia kwa manufaa ya kanisa kwani hana pengine pa kuzipeleka. Akidaiwa tutazichanga kanisani tumpe akarudishe.