jaman ndg zangu naomba nipewe ukwel juu ya hii hbr...
Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki
hisa IPTL James Rugemalira.
Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki
hisa IPTL James Rugemalira amefungua kesi
mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh.
398 bilioni zilizokuwemo/ zinazotakiwa
kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na
zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta
mjafala mkubwa bungeni.
Katika madai yake, mwenye hisa hatambui
malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa
kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa
na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa
makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate
kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania
Investment Center na wala mmliki wake kuwa
na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini
kutoka idara ya Uamiaji.
Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni
jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa
nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu
wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje.
Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa
serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni
ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering
kuingia ubia na Kampuni Feki na
kumsababishia hasara ya sh. Bilioni 56 kwani
alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia
mashitaka mbia mwenza PAP baada ya
kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni
hiyo.
Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama
zote alizotumia kuendesha kesi sh. 36.8
bilioni.
Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali
kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye
account ya Escrow na endapo serikal ingeona
kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP
au IPTL account ambayo yeye alikuwa
signatory.
Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo
anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa
PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena
madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa
serikali siku 14 tu toka 1 Januari, 2015 kuwa
wamelipa malipo yote.
Katika madai hayo, ili kuyadhitisha
ameambatinisha:
1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za
serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa
kwa PAP
2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji
hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala
kupewa Taxe clearance certificate.
3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa
kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa
haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa
au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi
ya Shirika lolote la Uma.
3. Report ya Bunge kama muhimili mwingine
wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za
serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/
kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa
kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.
4. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa
serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki
wake.
5. Mapendekezo ya bunge kwa serikali
yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.
6. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya
watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya
kuilipa kampuni isiyo halali.
7. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la
serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na
kuridhia mapendezo hayo.
8. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha
serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote
waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo
halali.
9. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika
hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa
kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi
kwa uzembe huo.
10. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali
kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya
uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.
11. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu
kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri
wa kulipa kampuni isiyo halali.
Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hasia za
wanachi juu ya malipo ya Escrow account. Ni
mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na
wanachi hawako tiyari kuona pesa kama hiyo
ikilipwa tena.