Escrow bado mbichi, Kafulila ndiye wa kupuliza kipenga

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Mambo bado. Escrow haijaisha. Upelelezi wa taasisi mbalimbali za kiintelijensia umetamalaki ukisaka ukweli zaidi na zaidi. Wahusika bado watashughulikiwa. Nyaraka nzitonzito zinaendelea kukusanywa na wahusika kuongezeka. Amini nawaambia,Escrow bado mbichi na in action.

Bado wafadhili wanafuatilia hatma ya Escrow na wahusika wake. Hawajaanza kuonesha sura zao za tabasamu na za kuridhika juu ya kadhia hii iliyoliweka Taifa kwenye ubao wa aibu na mjadala wa hasara. Escrow bado mbichi.

Mamlaka za Mkombozi Commercial Bank na Stanbic Bank bado zinahaha na uchunguzi wao kwa ajili yao na Taifa kwa ujumla. Hatua kali za kinidhamu zisizo za hamu ziko njiani kuchukuliwa.

Mahakamani nako hakujapoa. Kuanzia nje hadi hapa Tanzania,kesi zihusuzo Escrow bado ni alive. Zitatolewa nyaraka,sauti na sinema za kutosha kuthibitisha au kukanusha kesi hizo. Kesi vutizi ni kati ya IPTL na David Kafulila Mahakama Kuu ya Tanzania. Itajidhihiri kama Kafulila aliichafua au kuisemea ukweli IPTL.

Kafulila ndiye mwanzilishi wa Escrow Scandal Bungeni. Anafuatilia kila hatua ya sakata hili. Anashiriki kama refa wa kati wa mpambano huu. Ndiye anayetumiwa kutoa kauli mbalimbali za Escrow huku akijilinda Mahakamani kwenye kesi yake na IPTL. Ni yeye wa kupuliza kipenga cha mwisho!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Hatutadanganyika kwa ya amboni wala ya ......maoni
 
Mkuu
Hata unataka tujadili nini mzee Tupa?

Vipi kuhusu wagombea wenu?

Vp kuhusu Chenge na zuio lake la mahakama?

Anyway Escrow itaiva endapo na Jk akijumlishwa
 
Mambo bado. Escrow haijaisha. Upelelezi wa taasisi mbalimbali za kiintelijensia umetamalaki ukisaka ukweli zaidi na zaidi. Wahusika bado watashughulikiwa. Nyaraka nzitonzito zinaendelea kukusanywa na wahusika kuongezeka. Amini nawaambia,Escrow bado mbichi na in action.

Bado wafadhili wanafuatilia hatma ya Escrow na wahusika wake. Hawajaanza kuonesha sura zao za tabasamu na za kuridhika juu ya kadhia hii iliyoliweka Taifa kwenye ubao wa aibu na mjadala wa hasara. Escrow bado mbichi.

Mamlaka za Mkombozi Commercial Bank na Stanbic Bank bado zinahaha na uchunguzi wao kwa ajili yao na Taifa kwa ujumla. Hatua kali za kinidhamu zisizo za hamu ziko njiani kuchukuliwa.

Mahakamani nako hakujapoa. Kuanzia nje hadi hapa Tanzania,kesi zihusuzo Escrow bado ni alive. Zitatolewa nyaraka,sauti na sinema za kutosha kuthibitisha au kukanusha kesi hizo. Kesi vutizi ni kati ya IPTL na David Kafulila Mahakama Kuu ya Tanzania. Itajidhihiri kama Kafulila aliichafua au kuisemea ukweli IPTL.

Kafulila ndiye mwanzilishi wa Escrow Scandal Bungeni. Anafuatilia kila hatua ya sakata hili. Anashiriki kama refa wa kati wa mpambano huu. Ndiye anayetumiwa kutoa kauli mbalimbali za Escrow huku akijilinda Mahakamani kwenye kesi yake na IPTL. Ni yeye wa kupuliza kipenga cha mwisho!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Nimekusoma katikati ya mistari nimegundua kua ccm nikichaka chamafisadi
 
Kama ikulu haichukuliwi hatua basi hatuna haja ya kuendelea kujadiri make kwa hapa Tz ikulu no mwizi namba 1
 
Mambo bado. Escrow haijaisha. Upelelezi wa taasisi mbalimbali za kiintelijensia umetamalaki ukisaka ukweli zaidi na zaidi. Wahusika bado watashughulikiwa. Nyaraka nzitonzito zinaendelea kukusanywa na wahusika kuongezeka. Amini nawaambia,Escrow bado mbichi na in action.

Bado wafadhili wanafuatilia hatma ya Escrow na wahusika wake. Hawajaanza kuonesha sura zao za tabasamu na za kuridhika juu ya kadhia hii iliyoliweka Taifa kwenye ubao wa aibu na mjadala wa hasara. Escrow bado mbichi.

Mamlaka za Mkombozi Commercial Bank na Stanbic Bank bado zinahaha na uchunguzi wao kwa ajili yao na Taifa kwa ujumla. Hatua kali za kinidhamu zisizo za hamu ziko njiani kuchukuliwa.

Mahakamani nako hakujapoa. Kuanzia nje hadi hapa Tanzania,kesi zihusuzo Escrow bado ni alive. Zitatolewa nyaraka,sauti na sinema za kutosha kuthibitisha au kukanusha kesi hizo. Kesi vutizi ni kati ya IPTL na David Kafulila Mahakama Kuu ya Tanzania. Itajidhihiri kama Kafulila aliichafua au kuisemea ukweli IPTL.

Kafulila ndiye mwanzilishi wa Escrow Scandal Bungeni. Anafuatilia kila hatua ya sakata hili. Anashiriki kama refa wa kati wa mpambano huu. Ndiye anayetumiwa kutoa kauli mbalimbali za Escrow huku akijilinda Mahakamani kwenye kesi yake na IPTL. Ni yeye wa kupuliza kipenga cha mwisho!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Kweli ni ya moto maana ile mechi kati ya Chichiem na Ukawie kufika naona Chichiem mmetandikwa sana huko sumbawanga sasa sijui kama kwa Mizengwe Kayaanza Petero Pinda kunakalika tena.
 
Binti yangu Tetty,mambo ni moto na tight hasa. Matokeo ya Sumbawanga ni kuimarika kwa upinzani na ukomavu wa demokrasia. Mechi ya fainali ni hapo Oktoba.

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:

Ungewastua WAZEE huko basi hata hii UA UA ya raia wasio na hatia si njema kwa TAIFA letu.Hata hiyo October 2015 wengine tunaiogopa maana Chama Chetu Cha Majambazi hakijakubali bado upinzani kama ni haki yao kuwepo sababu Katiba ina waruhusu.

Mie naomba washtue wazee huko bado tunaihitaji NCHI yetu ,tunajua wao wanapesa kukifyatuka watakimbilia UGHAIBUNI na familia zao
 
Faru ni mpole akiuwawa, lakini akijeruhiwa anaogopa sana kufa na anakuwambogo......PIGA TU na UA!!! ndio defence mechanism ya mwizi mzoefu au jambazi anapoanikwa hadharani
 
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!Wajua Nyoka mwenye MAkengeza nafuu kumuua kabisa kuliko kumjeruhi?Japo ukisha mjeruhi nyoka kwa muda atakuwa na SUMU kali sana,lakini ni baada ya muda mfupi anakufa,lakini je nyoka huyu atajeruhi wangapi kabla hajafa?Mimi na wewe hatuna majibu upooooooooooooooooooooooooo:disapointed:
 
Tetty unaongea mambo makubwa mno. Ya kifalsafa hasa

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Sugu alizingumza kuwa wahusika wewekwe msalabani tusonge mbele.......napendaga sana huyu jamaa akiwa anachangia mijadala mbali mbali....
 
binti yangu tetty,mambo ni moto na tight hasa. Matokeo ya sumbawanga ni kuimarika kwa upinzani na ukomavu wa demokrasia. Mechi ya fainali ni hapo oktoba.

Mzee tupatupa

ngoja tusubiri kwenye kampeni zijazo kama watasema vyama vya upizani ni vyama vya musimu
 
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!Wajua Nyoka mwenye MAkengeza nafuu kumuua kabisa kuliko kumjeruhi?Japo ukisha mjeruhi nyoka kwa muda atakuwa na SUMU kali sana,lakini ni baada ya muda mfupi anakufa,lakini je nyoka huyu atajeruhi wangapi kabla hajafa?Mimi na wewe hatuna majibu upooooooooooooooooooooooooo:disapointed:

Ukitaka kukamua maziwa kutoka kwa ng'ombe chizi unamfunga kamba miguu yote miwili na kumpatia pumba yenye magadi. Utakamua mpaka mikono ipate ganzi. Kina Mnyika na Kafulila ndiyo kazi wafanyayo.
 
Tetty unaongea mambo makubwa mno. Ya kifalsafa hasa

Mzee Tupatupa

Mzee Tupatupa bwana,mie naongea ukweli wa maisha ya kawaida tu.Ni ukweli usiopingika NYOKA akijeruhiwa haishi muda mrefu uhakika wa kufa upo,lakini anakuwa na hasira ya kuua chochote kilichopo mbele yake,kwa kutumia mbinu yoyote ile kutema mate au kuuma vyote vyawezekana.
 
Ukitaka kukamua maziwa kutoka kwa ng'ombe chizi unamfunga kamba miguu yote miwili na kumpatia pumba yenye magadi. Utakamua mpaka mikono ipate ganzi. Kina Mnyika na Kafulila ndiyo kazi wafanyayo.

Hivi wajua waweza mkamua ng'ombe bila hata kumgunga kamba?Njia nyepesi mwekee MACHICHA yaliyokamuliwa toka kwenye pombe na ongeza chumvi kidogo tu,lazima asahau kila kitu,ndicho wafanyacho wapinzani wetu wakuu CCM.Wanatumia sana PESA na maneno matamu ya uwongo kuwarubuni wapiga kura wetu.Upo kaka?
 
Wow!!! tatizo ni laana aliyowaachia Mwalimu JKN, walianza kupuuza aliyoyaasisi akiwa bado hai anaona. Ameondoka duniani akilalamika. Mfano "Ukitaka kulisemea azimio la arusha lenye maadili unatakiwa uwe na moyo wa kimwenda wazimu"; ....."Natembea na vitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha.....Mpaka sasa nkila ninaposoma azimio la Arusha sioni ni wapi penye makosa"..... "Wenye uchu wa madaraka, walevi wa madaraka tu waliamua kwenda Zanzibar na waliporudi tukajua tu hata kama hawajatuambia, tukaona mambo yamebadilika, watu wazima tukatambu ndio basi tena maadili yamekwishafutwa....."..... "Ukianza kula nyama ya mtu wala huachi, utaendelea tu....." nk nk Ndio maana Jericho Nyerere anasema wazi tu kwamba ana wasiwasi na uhalisia wa kifo cha mwalimu, CCM ilishamkolimba mtu haiwezi kuacha kukolimba kila anayezuia wasiibe na kupora. Laana hiyo itawafuatilia vizazi vyao mpaka kizazi cha saba. labda waombewe.
 
Mambo bado. Escrow haijaisha. Upelelezi wa taasisi mbalimbali za kiintelijensia umetamalaki ukisaka ukweli zaidi na zaidi. Wahusika bado watashughulikiwa. Nyaraka nzitonzito zinaendelea kukusanywa na wahusika kuongezeka. Amini nawaambia,Escrow bado mbichi na in action.

Bado wafadhili wanafuatilia hatma ya Escrow na wahusika wake. Hawajaanza kuonesha sura zao za tabasamu na za kuridhika juu ya kadhia hii iliyoliweka Taifa kwenye ubao wa aibu na mjadala wa hasara. Escrow bado mbichi.

Mamlaka za Mkombozi Commercial Bank na Stanbic Bank bado zinahaha na uchunguzi wao kwa ajili yao na Taifa kwa ujumla. Hatua kali za kinidhamu zisizo za hamu ziko njiani kuchukuliwa.

Mahakamani nako hakujapoa. Kuanzia nje hadi hapa Tanzania,kesi zihusuzo Escrow bado ni alive. Zitatolewa nyaraka,sauti na sinema za kutosha kuthibitisha au kukanusha kesi hizo. Kesi vutizi ni kati ya IPTL na David Kafulila Mahakama Kuu ya Tanzania. Itajidhihiri kama Kafulila aliichafua au kuisemea ukweli IPTL.

Kafulila ndiye mwanzilishi wa Escrow Scandal Bungeni. Anafuatilia kila hatua ya sakata hili. Anashiriki kama refa wa kati wa mpambano huu. Ndiye anayetumiwa kutoa kauli mbalimbali za Escrow huku akijilinda Mahakamani kwenye kesi yake na IPTL. Ni yeye wa kupuliza kipenga cha mwisho!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Majanga matupu
 
Back
Top Bottom