PreGE2025 Eric Shigongo ajitolea Mitambo kuboresha barabara Buchosa

PreGE2025 Eric Shigongo ajitolea Mitambo kuboresha barabara Buchosa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,398
Reaction score
14,527
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amepeleka mitambo maalum kwa ajili ya kuchimba na kufungua barabara zote za mitaa ambazo hazijawahi kupitika kwa urahisi, katika hatua ya kuboresha maisha ya wananchi na kurahisisha shughuli za kila siku za kiuchumi na kijamii.

Akizungumzia mitambo hiyo, Shigongo ameitaja kuwa mali binafsi ya watu wa Buchosa na si ya serikali, na itasambazwa jimbo hilo ili kutumika kufungua na kutengeneza barabara mpya.

Ameongeza kuwa zoezi la utengenezaji na uboreshaji barabara litafanyika kwa ushirikiano na usimamizi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

 
BuNgeni si wamasema MAZA HADAIWI?
 
Weh.. yale matrekta aliyosema yapo kwenye makontena kipindi kile ndiyo yamefika leo?
 
Back
Top Bottom