Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 745
- 1,504
Ukikutana na mtoto wa kike, mtoto wa watu ukampenda na kumwambia, kwa uaminifu akakubali kuwa nawe, muheshimu. Ukiona hauwezi tena kuwa nae, kwa sababu zako mwenyewe unazojua, kama ulivyomkuta mwanzo basi mwache kwa salama aende zake kwao. Usimdhuru au kumtendea unyama kwa kuwa tu mmeshindana, bali mruhusu aende zake kwa amani na utulivu.
Ukatili wa kijinsia ni tatizo linaloendelea kuongezeka katika jamii, hasa kwa wanawake. Sina maana kuwa wanaume hawatendewi ukatili na wanawake. Maana yangu inatokana na kutokuwepo idadi linganifu ya visa hivyo baina ya wanaume na wanawake; visa vingi vya ukatili katika ndoa au mahusiano, vinawahusisha wanawake zaidi kuliko wanaume. Wanawake wanadhulumiwa kiutu kuliko wanaume. Hii inatishia usalama wao, heshima na amani katika jamii zetu, zinazopigana kusimamia usawa na haki za binadamu.
Malcolm X, Mwana harakati kindakindaki wa stahiki za watu weusi katika karne ya 20 nchini Marekani aliwahi kutamka, "Jamii yoyote haiwezi kupiga hatua kimaendeleo, kwa kupuuza heshima ya wanawake wake" Mwanamke ni shina la familia au jamii, ndio maana ukimwelimisha yeye basi umeelimisha taifa zima. Mwanamke kwenye familia zetu hana tofauti kabisa na waziri mkuu: huratibu shughuli zote za makaazi ili kuhakikisha kuwa masuala yote yahusuyo maendeleo, usalama na utulivu yanakuwa ktk msawazo sahili.
Wanawake hawajakamilika ndio, kuna wakati wanatenda makosa kwa kuwa nao ni binadamu lakini, yafaa nini kumuhukumu kwa labda kumtendea unyama unaomwacha na ulemavu au hata kupora uhai wake haliyakuwa unaweza tu kumwacha akaenda zake kuendelea na maisha yake, huku wewe ukibakia na yako?
Wengi tunasema hasira huja tu, haidhibitiki. Hii si kweli. Hasira si sawa na usingizi ukujiao kwa kuchochewa na ubongo wa matendo yasiyo na hiyari. Hasira ina mchakato; kutupa tupa maneno makali, kuchemka na kukosa utulivu nk, yote hayo na mengine huanza kabla ya mtu kufikia hatua ya kufanya tendo la hasira. Kwa lugha nyingine, ni viashiria vya hasira kuja. Unawezaje basi kusema ni kitu kisichozuilika, haliyakuwa kina hadi symptoms and characteristics? Badala ya kulaumu tunda la viashiria, kwanini mtu usifanyie kazi symptoms mapema zinapoanza kuonekana? Kama unahisi kuanza kubadilika kwa kuwa hapo, kwanini usiondoke kwenda mbali kidogo kwa muda, urudi baadae? Si ni hekima kuikwepa shari kuliko kuendelea kuisogelea au kuipa "KARIBU"? Kwanini mtu ubaki mahali, mahali ambapo unaona kabisa panakuhamisha upepo kihisia, jambo linaloweza kuishia na kutenda dhulma au kitu cha aibu?
Kuchinja, kubaka, kujeruhi nk zimekuwa miongoni mwa namna nyingi zinazotumika kuwaumiza wanawake katika miaka ya karibuni katika jamii zetu na mataifa yetu. Haya mambo yanatia doa juhudi za hata serikali zetu ktk uletaji demokrasia ya kweli, kwa sababu demokrasia ikikosa pumzi ya usawa wa kijinsia na uheshimuji haki za binadamu baina ya watu, inakosa maana. Inakosa mizizi ya kuishikilia. Haiwezekani tuendelee kuishi ktk mataifa yanayoitwa "ya kidemokrasia" halafu matukio ya kinyama kwa dada zetu, mama zetu, shangazi zetu, wake zetu nk yanashamiri na kugeuka kama sehemu ya utamaduni unaotutambulisha. Hatupaswi kuruhusu unyama kurasimishwa na watu wachache, wasio na hekima ya kujizuia au kutawala idara ya hisia zao.
Mambo ya enzi za kijima, ni ya kijima. Hii ni karne ya 21, sio ya kwanza au ya tano, wakati ambapo sifa bora ya wanaume ilikuwa ni kutamba kishujaa amepata kuua watu wangapi au kunyanyasa wanawake wangapi kingono au vyovyote. Wakati ambapo kuua, kulimpa muuaji umashuhuri na heshima mbele ya jamii. Huu si wakati huo, wa kutukuza unyama. Huu wa sasa ni wakati wa kuheshimu Haki za binadamu, miongoni mwake ikiwa ile ya kuishi au uhai. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kutimiza malengo yake. Kwa maana hiyo basi, UKISHINDWANA NA MTU, KULIKO KUDHIHIRISHA UKALE WAKO WA FIKRA KWA KUMTENDEA DHULMA NA USHENZI, MWACHE AENDE. Wakati mwingine watu hukutana kwa bahati mbaya tu, yamkini ana mtu aliyekusudiwa kuishi nae kwa amani tofauti na wewe. Mwache afikie hatma ya maisha yake kwa njia iliyokusudiwa juu yake na Mwenyezi Mungu. Ukatili unaumiza, ukatili ni aibu, ukatili ni ushenzi kama mwingine wowote.
*ChanyaDaima*