mchungaji7
Senior Member
- Feb 2, 2017
- 187
- 396
Wana MMU habari za mchana?
Nimeona niwashirikishe hili wakati mnajiandaa kwa lunch.
Maagano ni sawa na makubaliano au mkataba. Katika hali ya kawaida mtu unapopata mwenza mpya unaweza dhani kuwa umepatia sana. Mahusiano mapya huwa yanakuja na mihemko mingi ya miili kuliko yale ya zamani.
Watu wanapokutana katika hali ile ya upya hudhani wameyapatia sana mahusiano na wengi wao huwa hawapendi kusikiliza ushauri utakaokuja kinyume na kile walichokiumba kwenye fikra zao.
Katika eneo ambalo watu wanaongoza kwa kuumizana na kudanganyana kwa hali ya juu ni kwenye mahusiano. Wengi wamekuwa wakiahidiana ahadi nyingi ambazo mwisho wa siku zina kuwa kinyume. Ktk ahadi zote yenye madhara makubwa ni ahadi ya kulishana au kubadirisha damu.
Wahusika huchanja sehemu za miili yao na kisha kula kiapo cha kutoachana kwa kuunganisha damu zao au kulishana. Maagano haya yana nguvu sana ktk ulimwengu wa roho kwakuwa yamehusisha damu. Mungu hausiki na maagano kama hayo mwenyewe ni shetani.
Kwetu wakristo tuna agano moja tu la damu na lilifanyika Mara moja tu pale msalabani. Ikitokea mmoja amevunja huleta madhara makubwa sana kwa katika mahusiano mapya. Moja ya madhara hayo ni kuwa na mahusiano yanavunjika vunjika hovyo kwakuwa ile damu inataka urudi ulipo apa .
Kuna watu huwa wanafanya hivi kwakuongozwa na mihemko, au hisia za mwili. ..
Usijaribu kuweka agano la damu na mwenza wako , kama kweli mnapendana hamuhitaji chchte kuwaunganisha zaidi ya upendo.. Maagano yoyote yanayohusisha damu hayatokani na Mungu kuna nguvu za kishetani zina yasimamia.
Epuka, kataaa, kimbia maagano kama hayo.
Barikiweni sana!
Mchana mwema!