Epuka Kosa la kuanzisha mahusiano kwa kumuona huruma Mwanamke /Mwanaume ulievutiwa naye

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,079
Watu wengi hivi sasa wameshaumizwa sana kwenye mahusiano mpaka wengine wamejenga chuki, kinyongo,hisia za kisasi dhidi ya wanaume au wanawake wote ulimwenguni.

kutokana na matukio hayo nimekuletea ufumbuzi wake wa kuepuka kuumizwa kwenye mapenzi.Kwa maana maumivu ya mapenzi kwako yatabaki historia na hakuna mwanaume au mwanamke ambaye anaweza kukupiga tukio katika maisha yako yote .

1.MWANAMKE MWEMA SANA HUWA ANATESWA SANA KWENYE MAHUSIANO KWANINI?

Ukifanya uchunguzi utabaini kwamba

° Mwanamke mwenye sifa nzuri kama huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu, Mwanamke mwenye nia njema ya kujenga familia imara huwa anateswa sana kwenye mahusiano lakini Mwanamke ambaye hapendeki wala hashauriki huwa haumizwi kwenye mahusiano isipokuwa yeye anakuwa bingwa wa kuwapiga matukio wanaume wenye nia njema na malengo naye.Kwanini inakuwa hivyo angalia hapa chini

MAKOSA AMBAYO MWANAMKE MWEMA SANA HUWA ANAFANYA YENYE KUSABABISHA ANATESWA SANA KWENYE MAHUSIANO

Makosa hayo ni kama ifuatavyo

°Anataka kumbadilisha tabia Mwanaume ambaye haeleweki.Kwa mfano mwanaume anakuwa ni mlevi kupindukia, mcheza kamari, mhalifu sugu,mwanaume hataki kazi, akipewa mtaji anakula, akitafutiwa kazi anatafuta kisingizio cha kuacha kazi,mwanaume anakuwa na majibu ya mkato,mwanaume anakuwa na hasira kupitiliza.

°Mwanamke kwa sababu anajichukia kwa muonekano,au ni single mother ambaye alitelekezwa na ujauzito au watoto,au mwanamke anakuwa na umri mkubwa sana labda miaka 30+.

°Hapo mwanamke anakuwa anajiona mwenye mikosi,laana,kujiona mzee kabla ya umri,kujiona kichekesho,kujiona mbaya sana wa muonekano,kujiona "shapeless" hivyo Mwanamke huamua kujitutumua sana ili aonekane ni wife material.

Ili athibitishe kuwa ni wife material hufanya uwekezaji kama ifuatavyo

°Kumtafutia kazi, kumchukulia mkopo, kumfungulia biashara, kumjengea nyumba

°Akikuta mwanaume
amenunua kiwanja yeye Mwanamke huamua kujenga nyumba kwa fedha zake kwenye uwanja wa mwanaume lakini hati ya nyumba imeandikwa majina ya mwanaume matokeo yake nyumba ikisimama tu mwanaume huanza vituko ili kumfukuza nyumbani kwa lengo la kuingiza mahawara zake ambao huwa anaona ni wanawake wa ndoto zake.

°Kujibebesha mimba, kujitambulisha kwa mama mkwe yeye mwenyewe,kujilipia mahari yeye mwenyewe, kulazimisha aolewe, kujiweka karibu na mama mkwe pamoja na mawifi ili aonekane ni wife material

°Kutaka kumbadilisha tabia mwanaume,labda mwanaume ni mlevi kupindukia anataka kumuachisha pombe,mwanaume anacheza kamari anataka kumuachisha kucheza kamari,mwanaume anafanya sana starehe Mwanamke anataka kumuachisha tabia hizo.

°Mwanaume anakuwa na hasira kupitiliza, ubabe, utemi, dharau, majivuno, kiburi,na ujuaji Mwanamke anafanya kazi ya kumfariji, kumliwaza, kujishusha ili kuepuka ugomvi.

°Kama ameachiwa mali za urithi huamua kuandika majina ya mwanaume akiamini ndiyo ataonekana wife material lakini mwanaume anakuwa amepata tiketi ya kwenda kutafuta Mwanamke wa ndoto zake kisha mwanaume atasubiri akiwa amepauka, amefubaa, ananuka, anaumwa, hajiwezi kwa chochote atarudi kuomba msamaha, kupiga magoti, kutishia kujiua, kumbembeleza sana,kudai shetani alimpitia.

kutokana na uwekezaji mkubwa kama huo husababisha Mwanamke anakuwa hawezi kujiondoa kwenye mahusiano hayo hata kama anapigwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani,mwanaume anakuja na mahawara ndani kwenye kitanda anacholalia yeye huku Mwanamke analazimishwa kulala nje ya chumba.

Mwanamke huwa hawezi kujiondoa kwenye mahusiano ambayo amewekeza jasho lake.Siku zote mapenzi ya Mwanamke yapo kwenye jasho lake.Ndiyo maana ukiona Mwanamke hafanyi uwekezaji wowote kwa mwanaume tambua kwamba amejiandaa kuachana na mwanaume kimyakimya.

MWANAUME MWEMA SANA HUWA ANATESWA SANA KWENYE MAHUSIANO KWANINI?

Mwanaume mwenye malengo na nia njema ya kujenga familia imara huwa anateswa sana kwenye mahusiano kwa sababu zifuatazo

-Mwanaume anakuwa anataka kuonekana ni tofauti kabisa na wanaume wengine kwenye jamii,hivyo mwanaume huanza kwa kuongea kwa sauti ya upole, kumnyenyekea sana, kumjali sana, kumbembeleza sana, kumwambia asije kumuacha,mwanaume atakuwa anajitutumua kuonyesha kwamba yeye ni husband material kuliko wanaume wengine wote kwenye jamii.

-Mwanaume anakuwa anataka kumsaidia Mwanamke ambaye ametelekezwa na ujauzito au watoto kwa lengo la kumsomesha, kuwasomesha watoto ambao ametelekezwa nao, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea, kusaidia ndugu wa Mwanamke, kumchukulia mkopo, kumkabidhi ATM card kwa lengo la kumruhusu Mwanamke wake kutoa fedha kiasi chochote anachotaka ili kumthibitishia kwamba anampenda sana na yupo tayari kuhatarisha maisha yake ili kumfurahisha.

-mwanaume anakubali kunyimwa unyumba muda mrefu sana kila siku anakubali visingizio ambavyo Mwanamke anakuwa anatoa mara kusingizia uchovu, kusema hana mood nzuri, kusema mgonjwa,kusema mwanaume anawaza ngono kuliko kazi,mara mwanamke ataonyesha uso wa hasira, Mwanamke anagoma kupika,hafui,hafanyi usafi , Mwanamke anakuwa na safari za mara kwa mara kwenda nyumbani kwao,kisha akiwa nyumbani kwao anasingizia kunyanyaswa kisha mwanaume anamfuata nyumbani kwao kumbembeleza, kumkumbusha wema amefanya zamani, kumnunulia zawadi, kumpeleka "Out" kwenye restaurant za gharama.

-Mwanamke anaanza mawasiliano na ex wake mpaka saa 8 za usiku kisha mwanaume wake akiuliza tu Mwanamke anakuja juu kwa jazba anaporomosha matusi ya nguoni,atasusa kulala kitandani,atadai ananyanyaswa,atadai hana uhuru.Mwanamke huanza kufanya hivyo baada ya kuona ameanza kupendeza, amekuwa na muonekano mzuri sana na ex wake ameanza kumsifia,atasubiri punde tu amesimama vizuri kiuchumi anaanza kufanya vituko.

-Mwanaume mwema hufanya kosa la kumlipia madeni ambayo mwanamke wake anakuwa nayo, vilevile kosa lingine mwanaume mwema hufanya ni kumuandika majina yake kwenye mali zake wakati huohuo Mwanamke huyo anakuwa hajachangia hata senti tano

-Kosa lingine mwanaume mwema hufanya ni kumchukulia mkopo kwa kuweka dhamana mali zake wakati huohuo Mwanamke huyo anakuwa hana faida wala mchango wowote wa maendeleo kwenye maisha ya mwanaume.

-Kosa lingine mwanaume mwema hufanya ni kusaidia ndugu wa Mwanamke wakati huohuo Mwanamke huyo hana kazi wala biashara yoyote yenye kusaidia kukuza uchumi wa familia

-Kosa lingine mwanaume mwema hufanya ni kusomesha ndugu wa Mwanamke wakati huohuo Mwanamke huyo hana kazi yoyote wala hana biashara yoyote ambayo anayofanya kwa lengo la kuinua uchumi wa familia.

-Kosa lingine mwanaume mwema hufanya ni kusamehe makosa haraka,ikiwemo kusamehe fumanizi na usaliti wa Mwanamke wake wakati huohuo Mwanamke huyo hana mchango wowote katika kuleta maendeleo ya familia.

-Kosa lingine mwanaume mwema hufanya ni anakubali kukonda , kupauka, kutembea kwa miguu,kula mlo mmoja,kulala chini, kuvumilia matusi ,na udhalilishaji kwa lengo la kuhakikisha mwanamke wake ambaye hana mchango wowote wala hana MSAADA wowote wa kukuza maendeleo ya kiuchumi ya familia anakula vizuri,kuvaa vizuri,kutumia simu ya gharama,

ZINGATIA YAFUATAYO

Kama unapambana kumuinua kiuchumi Mwenza wako wakati yeye hana kazi yoyote wala hana MSAADA wowote kwako tambua kwamba unajichimbia kaburi wewe mwenyewe kwa mikono yako.

-Kama utajenga nyumba kwenye kiwanja cha Mwenza wako wakati wa ujenzi nyumba yote umejenga kwa fedha zako na hati miliki ipo kwa jina la mwenza wako tambua kwamba baada ya nyumba kukamilika ujenzi mwenza wako ataingiza Mwanamke au mwanaume mwengine lengo uibuke ugomvi muachane na nyumba utamuachia kwa sababu hakuna jina lako kwenye hati miliki.

-Kama utachukua mkopo kwa kuweka dhamana mali zako ili kumuinua kiuchumi Mwenza wako tambua kwamba mwenza wako akisimama vizuri kiuchumi anakuacha ghafla bila sababu zozote za msingi kwa sababu atakuona wewe sio mwenza wa HADHI yake.

-Kama mwenza wako ni msaliti,mlevi kupindukia, mcheza kamari, mhalifu,anapenda sana starehe,anatumia pesa nyingi bila mahesabu ikiwa utapambana kumbadilisha tabia ni wazi kwamba unajichimbia kaburi wewe mwenyewe kwa mikono yako.Binadamu huwa hathamini jasho la mtu mwengine isipokuwa jasho lake yeye mwenyewe.

Hivyo uwekezaji wako ambao unafanya kuboresha maisha ya mwenza wako ni HASARA kwako na ndio kifungo chako kwake.
Ikiwa leo mahusiano yamevunjika baina yako na mwenza wako je nani atapata HASARA? Ikiwa mwenza wako hana cha kupoteza tambua kwamba unajichimbia kaburi wewe mwenyewe kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye mahusiano hayo.

Tambua kwamba maumivu ya mahusiano kuvunjika ni sawasawa na uwekezaji wako kwenye mahusiano hayo.
Ikiwa Mwenza wako hakupi ushirikiano wowote endapo utafanya uwekezaji wowote kwake hilo ndiyo kaburi lako kwake.

Fanya uwekezaji taratibu taratibu wakati mwenza wako anafanya uwekezaji taratibu taratibu.Hakikisha mahusiano yanapovunjika nyote mpate hasara sio upate hasara pekeako.
Mwenza wako kama anafanya uwekezaji kimyakimya labda anajenga kwa siri, kufungua biashara kwa siri na wewe fanya hivyo kwa sababu ukifanya kinyume chake unakwenda kuwachukia wanaume au wanawake wote ulimwenguni.
 
Mama Ndege huyo jamaa ulimwonea huruma ukaanzisha naye mahusiano?

Angalia chini ya huu uzi utaziona threads zangu nyingi tu na zitakupa utulivu wa akili
 
Mungu ana njia nyingi za kukutanisha watu!

Na upendo hauna kanuni!ogooa sana ukakutana na Dem ukamuona wa kawaida halafu mkaanza kuishi mtaa au kushirikiana halafu code ya moyo wako zikaanza kufunguka pole pole utakua deep Hadi tutakuonea huruma!!

Usimdharau mtu kwa kumuona wengine Wana nguvu deep in them inayoweza kukuangusha chini puuuh!!
 
Fanya uwekezaji taratibu taratibu wakati mwenza wako anafanya uwekezaji taratibu taratibu.Hakikisha mahusiano yanapovunjika nyote mpate hasara sio upate hasara pekeako.
Mwenza wako kama anafanya uwekezaji kimyakimya labda anajenga kwa siri, kufungua biashara kwa siri na wewe fanya hivyo kwa sababu ukifanya kinyume chake unakwenda kuwachukia wanaume au wanawake wote ulimwenguni.
Shukrani kwa kukazia Mkuu, nitakucheki private baadae
 
Back
Top Bottom