EPL: Spurs hataki sare wala kufungwa na Chelsea leo!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,279
25,857
Leo,Spurs wanateremka dimbani wakisaka ushindi tu dhidi ya Chelsea. Endapo Spurs atapata ushindi,Leicester itawapasa kusubiri hadi kumalizika kwa mechi mbili za mwisho za EPL. Hapo Spurs watafikisha alama 72,alama 5 nyuma ya vinara Leicester.

Matokeo ya sare au kufungwa kwa Tottenham Hotspurs yatawapa ubingwa Leicester. Hiyo itatokana na ukweli kwamba Spurs wataachwa alama 7 au 8 ambazo hawataweza kuzilipa kwa mechi mbili zitakazosalia. Hakika leo ni do or die kwa Spurs.
 
Chochote kinaweza kutokea katika mpira ila lei ana nafasi kubwa sana ya kuwa bingwa na itakuwa ajabu kama wasipokuwa mabingwa wacha tusubiri saa chache naona Chelsea atataka kumbania mpinzani wake ili amtoe nishai ni game nzuri kuitizama ila tot wapo katika waqt mgumu sana nadhani kuliko kipindi chote cha uhai wa club.
 
Hamna Dele Alli wala Mason, yaani kama ni tennis, Leicester walikuwa na 40 - 0 (forty love) na 3 championship points, ila spurs kachomoa moja kwa droo ya Manu, hivyo sasa ni 40-15, yaani leicester ana two championship point, leo spurs aliahinda inakuwa 40-30, na leicester akishindwa kuifunga everton inakiwa DEUCE, ila sioni kwa form ya leicester kupoteza 3 champinship point. Wa tennis watanielewa!
 
Mpira umeisha matokeo 2-2.

Leicester katwaa ubingwa kanufaika kwa sare kati ya Chelsea/Totenham.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom