Ligi Kuu England kuendelea leo: Chelsea kuumana na Manchester united

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210228_111625.jpg
Ligi kuu England inaendelea leo katika viwanja mbalimbali ambapo mchezo wa awali Crystal palace atakipiga dhidi ya Fulham saa tisa jioni.

Leicester city ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo itakutana na Arsenal ambayo inashika nafasi ya kumi na moja.

Na huko katika Dimba la Tottenham Hotspur wenyeji hao wataumana na Burnley ambayo hivi sasa inashika nafasi ya kumi na tano.

Mchezo mwingine ambao utakuwa na mvutano mkubwa ni kati ya Chelsea ambayo itakuwa darajani kuialika Manchester United.

Ikiwa Chelsea itashinda mchezo huo itakuwa na na alama 46 na itaishusha West ham United na kuweza kupanda nafasi ya nne.

Kwa upande wa Manchester United ikiwa itashinda itaendelea kujichimbia kunako nafasi ya pili.

Mchezo wa mwisho ambao utapigwa saa nne usiku Sheffield United ambayo inashika mkia kwenye msimamo wa ligi itaikabili Liverpool.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom