Epidemic ya Blogs na Websites Bongo …Nyingi Lakini Ubora ni Zero

gem08

Member
Jun 11, 2012
40
7
Je, Ni uhaba wa wataalam au ndiyo mazoea ya kupenda vya bure na rushwa!!

Tembelea website na blog za Bongo, ziwe za serikali, mashirika makubwa au za watu binafsi utashuhudia mwenyewe ninachokieleza hapa. Page hazina mpangilio (page alignment and inconsistency), hazivutii (matumizi mabaya ya typography, rangi na picha), vigumu kupata unachokitafuta (usability issues), maelezo yasiyoeleweka (no useful content and lack of clarity) na mengine mengi.

Mfano mzuri ni website ya serikali iliyokupewa msukumo mkubwa na rais wa Marekani Barak Obama iitwayo www.opengov.go.tz. Madhumuni yake yalikuwa kuwashirikisha wananchi katika masuala na shughuli za serikali ili kuhamasisha uwazi (promote transparency). Kama hilo ndio lengo lake, si lazima uwe na degree kufahamu kwamba pamoja na mambo mengine kinachohitajika kwenye website kama hii ni maelezo sahihi (useful content); user interaction kama emails na forms; na muonekano (look) ambavyo vitamshawishi mwananchi kushiriki (encourage public engagement). Kinachonishangaza ni upungufu wa ubora wa website hii kwa vitu basic kabisa ambavyo hata mwanafunzi (junior web developer) angeweza kufanya.

Orodha ya mifano ya website zisizo na ubora ni ndefu ila ona hizi chache ambazo ungetegemea ziwe angalau afadhali.

Nao wapenda kublog wameongezeka hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la blog na hali hii haioneshi dalili ya kupungua. Hata hivyo ubora wa blog hizo ni wa kutisha. Kwa lugha rahisi kabisa ni kwamba ‘zimelipuliwa' hakuna ujuzi. Wanablog wengi wanatumia free google hosting (yaani .blogspot). Elements zimebandikwa kila upande kwenye page hivyo msomaji anabaki ku-guess wapi pa kwenda. Nyingine hata maandishi hayaonekani.

Hivi majuzi tu nikiwa kwenye jamii forum kuna msomaji mmoja alikuwa anauliza wasomaji wengine ni wapi anapoweza kupata .com domain ya bure. Mwingine anaulizia internet ya bure. Ni swala la kushangaza kuona jinsi tunavyoitaka teknolojia bure bila kujali ubora.

Katika kulichambua swala hili nimeona kuna sababu kuu zifuatatzo:

  1. hali ngumu ya kimaisha;
  2. (2) kupenda vya bure;
  3. (3) rushwa; na
  4. (4) upungufu wa wataalam.

Binafsi nakubaliana kwamba hali ya mtanzania wa kawaida ni ngumu si ajabu ubora wa vitu ni mdogo. Hata hivyo iweje hata makampuni na serikalini bado hakuna ubora? Tatizo ni kwamba tumejenga mazoea ya kupenda vya bure na kutokujali ndiyo sababu inayopelekea hata tunapopata nafasi za uongozi iwe serikalini au kampuni binafsi bado tunajikuta kuchagua urahisi (cheap) na kusahau ubora (sacrifice quality)!

Swala la rushwa na ubinafsi linachukua nafasi kubwa. Katika uchunguzi wangu nilishtuka kusikia kiasi kilichotumika kutengeneza website ya kampuni moja kulinganisha na ubora wa website hiyo. Ni dhahiri kwamba bajeti iliyoidhinishwa haikutumika ipasavyo. Aidha kampuni ililipa bei ya juu kwa mtu au kampuni iliyotengeneza website hiyo au kuna mtu kabakiza chenji.

Kuhusu swala la upungufu wa wataalamu bado sikubaliani nalo. Japokuwa tuko nyuma, kuna vijana wengi wa kitanzania wenye ujuzi na wanaoweza kufanya kazi nzuri. Tuchukulie mfano mzuri wa ‘michuzi' blog iliyopata mafanikio makubwa. Mmiliki wa blog hii japokuwa anatumia free google service, ni dhahiri anatumia wataalamu wa tecknolojia kumtengenezea blog inayopendeza na kukidhi matakwa ya mtumiaji wakati yeye akitumia muda wake kuweka bidii kwenye fani yake ya ‘uandishi na upigaji picha' (yaani content). Sio ajabu kwanini anafanikiwa sana.

Mifano mingine ni hizi website zifuatazo ambazo naamini zimetengenezwa na watanzania:

Ukweli ni kwamba kuna matatizo ya kiuchumi, cultural na hata uongozi mbaya katika ngazi mbalimbali. Ukichukulia kwamba dunia ya sasa ni ya Internet, matatizo haya yanarudisha nyuma mafanikio ya nchi. Kwa kuwa hakuna physical contact kati ya msomaji na mwandishi, website ni kama kioo cha mwandishi. Hakuna mtu mwenye akili zake anayeweza kuamini kazi yako au kukuchukulia serious kama website yako imelipuliwa.

Kila mtu ana ujuzi wake. Ni unprofessional kutaka kufanya kila kitu peke yako. Wakati mwingine inabidi kutoa kidogo ili upate zaidi. Si lazima ulipe mamilion, kuna watu wenye ujuzi watakaokufanyia kazi nzuri kwa bei nafuu..shop around utawapata.

Mwisho ni kwa wajuzi na wataalam wa teknolojia. Kumbukeni teknolojia inabadilika kila siku hivyo tuna kila sababu ya kuendelea kujifunza mambo mapya constantly. Baadhi ya software tools nzuri kuzijua kwa maswala ya internet ni:

For Developers: PHP, Javascript, Wordpress, Joomla, CSS, ajax, JQuery, etc.
For Designers: Graphics - Photoshop, Gimp, etc.

goody@goodytechnology.co.uk
 
Nimekusoma, ila kwa upande wa watu binafsi. Nadhani suala la kipato ni issue sana. Na pia wataalamu wa bongo ni gharama. Binafsi nimehangaika na mahost wa tz mpaka nimekoma. Domain peke yake 15000 kwa mwezi, kuhost 45000 kwa mwezi. Nadhani unaona hilo tatizo. Wakati nje domain inaanzia 0.28$ mpaka 9$ . Nimekuwa nikipata msaada wa kiufundi toka Pakistan, yote kwa kuwa ukimgusa mbongo anaanza na dau kubwa kupita kazi.

Ni wakati wa mabadiliko, serikali kujali wataalamu (nafasi za kazi) na wataalamu kujali wateja
 
Nimeshangaa kusikia unalipa kiasi kikubwa hivyo. Kuhusu swala la Domain name naweza kuelewa kwa sababu inategemea ni domain extension gani (.com, .org, ectc) unayotumia. Mara nying extensions za Africa kama vile .tz nyinginezo zinakuwa za gharama? Hata hivyo sioni sababu ya kulipa kiasi kikubwa hivyo.

Nadhani tatizo hapa ni la wateja kutokujua au kusaka (shop around) palipo na unafuu wakati huo huo ubora ni wa juu.

Naweza kukuhakikishia kwamba mimi binafsi nina hosting company Goody Technology Solutions. Nina ofa package moja tu inayokupa kila kitu. Unaweza kuhost website zaidi ya kumi, una unlimite email, FTP accounts, free applications, free set up, good and quick customer support, n.k. Yote hii unalipa $9 yaani Tsh 16,000-20,000 tu kila mwezi. Hakuna other charges. Pia unaweza kupata huduma za webdesign au kukurekebishia uliyonayo kwa bei nafuu sana.

email yangu: goody@goodytechnology.co.uk
 
Bora umesema mkuu hizi blogspot za bongo zinatia aibu kwakweli.
 
rushwa, bad designers (yes we have capable designers but very few good ones) and most of them use templates that have already been designed by others and just change a few things, that's one, another problem is most people don't realize that web design is a profession like any other profession, if you need a good website you need to pay a good amount of money, if you need cheap, you'll always end up with an ugly looking site.

.Lazy designers, most designers don't like improving their skills, they keep on producing the same looking product for their clients, we can't compete with other countries by being lazy. i am also a web developer / designer
 
Kuna site kadhaa hapa Tanzania naona zipo kwenye kiwango cha kimataifa.

Welcome to Medical Stores Department | Medical Stores Department (Hii ni agency ya serikali)
The Official Website of Azam Football Club | Tucheze pamoja kwa furaha (timu mashuhuri ya mpira)

Na zinginezo nyingi.

Lakini kama ulivyosema rushwa imetawala sana na matokeo yake good designers hawalipwi vizuri na wanaamua kuachia ngazi na kutafuta dili ya maana.

Pia ujuzi wa watanzania wengi kwenye tovuti bado ndogo. Kuna watu hadi leo hii hawajui tofauti ya blog na website.
 
Nimeziona hizo website zian kiwango. Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu web developer a designer kukimbilia kwingine kunakolipa zaidi.
 
Well spoken. Mimi binafsi nina design websites. Kuna hii http://achuva.comlu.com ndio naifanyia kaza na nimeshaimaliza kwa kiasi kikubwa. All what people need to know ni kwamba web developing ni ujuzi na proffesion. Kila mtu sasa ana blog. Ni jambo zuri lakini ubora uzingatiwe.
 
Ninatafuta watu ambao we will work together on the site. It's heavy-duty site. Kinda like Yahoo.
 
Nimekusoma, ila kwa upande wa watu binafsi. Nadhani suala la kipato ni issue sana. Na pia wataalamu wa bongo ni gharama. Binafsi nimehangaika na mahost wa tz mpaka nimekoma. Domain peke yake 15000 kwa mwezi, kuhost 45000 kwa mwezi. Nadhani unaona hilo tatizo. Wakati nje domain inaanzia 0.28$ mpaka 9$ . Nimekuwa nikipata msaada wa kiufundi toka Pakistan, yote kwa kuwa ukimgusa mbongo anaanza na dau kubwa kupita kazi.

Ni wakati wa mabadiliko, serikali kujali wataalamu (nafasi za kazi) na wataalamu kujali wateja

kaka
msihangaike na mahost wa kibongo,kwanini muibiwe,mimi kwa mwaka nalipa TZ 50,000 FOR 1 GB DOMAIN.tena hii ni jamaa wa sri lanka,hawana shida na sio wababaishaji
 
Back
Top Bottom