EPA yaikoroga CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EPA yaikoroga CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyambala, Jan 6, 2009.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  EPA yaikoroga CCM


  na Esther Mbussi (Tanzania Daima)
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeandaa jarida mahususi linaloelezea historia ya wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Jarida hilo ambalo linaratibiwa na uongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam likiwa na lengo la kukisafisha chama hicho tawala na kashfa hiyo ya EPA linatarajiwa kuzinduliwa keshokutwa Alhamisi.

  Viongozi kadhaa wa juu wa CCM waliozungumza na Tanzania Daima jana akiwamo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ng’enda Kirumbe, walisema wanakusudia kulisambaza jarida hilo katika maeneo mbalimbali nchini bure.

  Kwa mujibu wa Kirumbe na viongozi wengine kadhaa wa CCM, jarida hilo ambalo linaonyesha kuwa ni mkakati wa chama hicho kujipanga kwa ajili ya chaguzi kadhaa zijazo, linakusudia kueleza namna kisivyokuwa na mkono wowote katika sakata hilo ambalo hadi sasa limesababisha watuhumiwa 21 kufikishwa mahakamani.

  Ili kufanikisha lengo hilo, jarida hilo linaelezwa kuwa na maandishi yanayokusudia kukanusha madai ambayo yamekuwa yakitolewa na wanasiasa kadhaa wa vyama vya upinzani kuwa CCM ilitumia sehemu ya fedha miongoni mwa shilingi bilioni 133 zilizoibwa EPA kwa ajili ya kampeni na ushindi wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

  Habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaonyesha kuwa, tayari viongozi mbalimbali wa CCM wameshaanza kuzungumza na wanachama wao kuhusu jarida hilo.

  “Hivi karibuni kumeibuka matukio mengi ya upotoshaji kutoka kwa wapinzani, yenye lengo la kukichafua chama, yakiwamo ya Richmond, ufisadi na mengineyo, chama chetu hakikumbatii wala hakilei ufisadi na ndiyo maana serikali imechukua hatua kwa wote walioshiriki,” alisema kiongozi mmoja wa CCM alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuzinduliwa kwa jarida hilo.

  “Kwa hali hiyo, wote wasiojua undani wa EPA, watapata fursa ya kusoma jarida hilo, ndipo mtakapojua ukweli wa wizi huo na jinsi CCM inavyochafuliwa kuhusika na wizi wa fedha za EPA,” alisema kiongozi huyo wa CCM.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kirumbe alisema jarida hilo liko katika hatua za mwisho za kuchapwa baada ya kuhaririwa wiki chache zilizopita.

  Alisema jarida hilo litatolewa bure kwa viongozi na baadhi ya wanachama watakaopenda kujua na kuelewa kwa undani historia ya EPA.

  “Baadhi ya wanasiasa wa upinzani kwa makusudi au kutojua historia ya EPA wamekuwa wakiwapotosha hata kuwagawa wanachama kwa kuwaambia kwamba CCM ilihusika katika kuiba fedha hizo ndani ya BoT, hivyo tumeona ni busara kuwafafanulia Watanzania ili kuelewa kuwa CCM haikuhusika.

  “Na kuanzia sasa kila suala ambalo litaonekana kuleta utata miongoni mwa wanachama na wananchi, chama kimeandaa jarida hili ili kutoa ufafanuzi kuepusha migongano na mfarakano usio wa lazima ndani ya chama,” alisema Kirumbe.

  Hata hivyo, alisema ufafanuzi zaidi kuhusu suala zima la jarida hilo atautoa siku ya Alhamisi wiki hii wakati wa uzinduzi wake ambao bado haujajulikana namna utakavyofanywa.

  Kashfa ya wezi wa fedha za EPA kwa mara ya kwanza ilifichuliwa kupitia katika mtandao wa intaneti kabla ya kupelekwa bungeni na Mbunge wa Karatu, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa.

  Kuibuka kwa kashfa hiyo ya EPA bungeni, kulisababisha mtafaruku mkubwa baada ya wabunge kadhaa wengine wa upinzani wakiwamo Hamad Rashid Mohamed (CUF) na Zitto Kabwe (CHADEMA) kuishikia bango serikali kutokana na sakata hilo.

  Kuibuka kwa sakata hilo kulisababisha Dk. Slaa afikie hatua ya kuandaa hoja binafsi kuzungumzia wizi wa fedha ndani ya BoT, uamuzi ambao hata hivyo ulizimwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye aliamua kumzuia.

  Tangu wakati huo hadi leo hii, viongozi wa upinzani na hususan wale wa CHADEMA wamekuwa wakiitaja Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ambayo ilichota kiasi cha shilingi milioni 40 katika akaunti hiyo ya EPA kuwa iliundwa mahususi kwa ajili ya kusaidia kampeni za urais na ubunge za CCM.

  Tuhuma hizi za kuihusisha CCM na wizi huo wa EPA mara kadhaaa na kwa njia tofauti zimekuwa zikikanushwa bila ya mafanikio na viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho tawala.
  juu
  Maoni ya Wasomaji
  Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
  Maoni 12 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
  MAZURI YOTE MNATUAMBIA NI KWA SABABU YA SERIKALI YA CCM.

  JE! YALIYOTOKEA EPA NI USIMAMIZI WA SERIKALI YA CHAMA GANI? WANACHAMA WA CHAMA GANI? WAMEFANYWA NINI? KAGODA VIPI?

  na mjb, dar, - 6.01.09 @ 10:54 | #6100

  Mwanzo wa ngoma ni lele. Bila shaka mtaeleza kwa undani pesa ya EPA ilvyoingia kwa BAHATI MBAYA SANA kwenye campaign za 2005. Pia mtaonyesha kusikitishwa na jinsi wanachama wenu waaminifu na ambao wengine wapo kwenye kamati ya maadili ya chama CCM walivyotafuna pesa hiyo na ambavyo mnaamini kugunduliwa kwa wizi huo ni AJALI YA KISIASA ambayo ingeweza kuepukwa kama mambo fulani fulani yangefanyika!

  na TICO, Mwanza, - 6.01.09 @ 10:08 | #6105

  CCM wanatafuta sumu ya kijarida cha CHECHE!

  na fido dido, tanzania, - 6.01.09 @ 10:15 | #6108

  Kuna baadhi ya wakati mtu hujaribu kujinasua kwenye tope ali apate kutoka kumbe ndio anazidi kujizamisha.

  Sasa hivi Chama Caha Mafisadi (CCM) imeanza kujinasua kwa kuanzisha vijijarida ili kujisafisha na ufisadi kwanini iwe sasa hivi wakati mwamnzo walipoambiwa kuna ufisadi ikawa kama kawaida yao kuanza kutisha watu watoe vielelezo au watakuwa mashakani. Hii njia ya kuanzisha vijarida ni ulaji mwengine wa aina yake ndani ya Chama kwa kisingizio cha kujisafisha.

  Kila siku mnajinata kwenye maredio na maruninga kuwa Serikali ya CCM imejenga mabarabara, zahanati na imeleta mshikamano lakini kwenye ufisadi uliosaidia CCM kushinda kwa kishindo mnataka kujivua.

  Chama Cha Mafisadi (CCM) hamtoki, hamtoki, hamtoki kwani siku zenu zimekaribia na ni 2010.

  na Mere Mwaipopo, Dar-Es-Salaam, - 6.01.09 @ 10:19 | #6109

  Waacheni walete kijarida chao wanadhani watajisafisha nacho kumbe ndio watazidi kujipaka matope! Mara nyingi wahenga walisema kwenye ukweli uongo hujitenga. Rostam na Malegesi mbona serikali ya ccm inaogopa kuwapandisha kizimbani? Hawa ndio watakaotoboa siri fedha walizokomba walizipelejka wapi. Huo mwingine wa hicho kijarida ni usanii tu

  na Kalundi, Tanzania, - 6.01.09 @ 10:27 | #6115

  MAFISADI JUWENI WATANZANIA TUNAWASANIFU, MTATUTAMBUA 2010 NDICHO KIAMA CHENU...LETENI HICHO KIJARIDA MSISAHAU KUJIBU; SERIKALI YA CHAMA GANI ILIYOONGOZA KIPINDI CHA EPA...???MAFISADI WAKUBWA...!!!!

  na Stone, Arusha, - 6.01.09 @ 11:02 | #6120


  acheni mambo yenu ya ubabaishaji nyie mafisadi mmezoea kuleta hayo mastail yenu ya kiwiziwizi

  yaani mmeiba weeee sasa mnaona tumeshtuka mtataka kutudanganyia pipi.
  hapewi kura mtu yeyote wa familia ya kifisadi 2010.
  acheni nawenzeni waongoze nchi sio nyie pekee ndo mwajua saaaana kuongoza..
  acha ubabaisahji watu tuna masira yetu hapa

  na maisha, dar ,tz, - 6.01.09 @ 11:26 | #6127

  Kijarida hicho kielezee kwa undani Kagoda ni ya nani na wahusuka wa kagoda wanapandishwa Kizimbani kujibu shutuma za kuchota fedha za EPA.Kama CCM wana akili kweli walitakiwa kutengua kitendawili cha Kagoda na siyo kuanzisha kaepa kadogo ka jarida.Wanachotaka kueleza umma ni upuuzi mtupu.Hiyo ni kuonyesha wazi ccm imeishiwa kweli siku ya kifo miti yote huteleza.Kwa ccm sasa wamekosa sera kabisa.Sioni sababu za kimsingi zinazoifanya ccm kuanzisha ulaji mwingine wa fedha za walala hoi.Kwa hilo tutawafungulia mashtaka mengine ya matumizi mabaya ya fedha za umma.Wamesema watagawa bure kijarida hicho kwa fedha ya nani,ya kwao waliyooiba kutoka EPA au ni hiyo ya mlala hoi

  na Ruto, Dodoma, - 6.01.09 @ 11:37 | #6130

  KWELI CCM IMEFILISIKA LAKINI NANI MWINGINE WA KUZIBA PENGO HILO? UKITAZAMA VYAMA VINGINE VYOTE VINA KASORO NYINGI ZAIDI YA CCM. MCHANGO WAO MKUBWA UMEKUA KUTOA SIRI ZA MAOVU YANAYOFANYWA NA SERIKALI YA CHAMA CHA CCM LAKINI UVUNGUNI MWAO KUNANUKA UOZO WA VYAMA VYAO.
  HERI HILI ZIMWI TULIJUALO KULIKO TUSILOLIJUA WAJAMANI.
  KAMA KUNA FAIDA KWETU WADANGANYIKA KUMTOA CCM POA, LAKINI TUSIJE RUKA MKOJO TUKATINGA KWENYE ****.
  PENGINE ITAKUWA VEMA TUPIGE KURA ZETU 2010 KWA KUWEKA USAWA WA WAGOMBEA TOFAUTI WA PANDE ZOTE ZA VYAMA VYOTE ILI KUWEPO NA IDADI SAWA YA UONGOZI. UPINZANI USHAMIRI NA UWE NA NGUVU.

  na Biswalo, Niko Dar, - 6.01.09 @ 11:56 | #6134

  UTOLEWAJI WA KIJARIDA CHA KUKANUSHA AU KUTOSIKA KWA CHAMA TAWALA NA EPA NI HATUA YA MWANZO NZURI WA KUPAMBANA NA WASOMI UCHWARA WANAOSHIRIKIANA NA BAADHI YA MAGABACHORI NA WAMANGA KUHAMISHA RASILIMALI ZA NCHI HII NA KUWAACHA WAZAWA KUWA NI MASKINI WA KUTUPWA.
  WAACHENI WAUNGAME MADHAMBI YAO NA ADHABU AU MSAMAHA NI JUU YA WAZAWA.LA
  MSINGI TUJIANDAE VEMA KUKATAA PILAU AU
  KANGA AU PESA ZAO WAKATI WA KAMPENI ZAO
  TUJUE KUWA SAHANI MOJA YA PILAU HAIWEZI
  KUBADILISHWA NA SHANGINGI LA MILLIONI
  80 LA AKUPAYE PILAU HIYO,NA KUPELEKA WATOTO WAKE ST,ATHONY INERNATIONAL SCHOOL NA WAKO AKIISHIA DARASA LA NNE.
  WAZAWA AMKENI 2010 IWE YA HISTORIA.
  ALUTA KONTINUA.

  na Mkwalla, Tanga, - 6.01.09 @ 11:56 | #6135

  Mkwalla nakala yako lau kama ingekua haijajaa chuki na magabacholi na wamanga, ningesema ni mawazo murua. Usiwe na chuki kwa mtu kwa sababu tu eti anakula kuku kwa mrija na wewe unasakamwa na dagaa wakavu. Kama wameiba wapate adhabu yao lakini kama walioiba ni wazawa wenzako na wanawekeza kwa hao wakuja, chuna mzawa mwenzio. Tatizo mji wowote wenye mabaraza mengi hamuishi bila maneno ya chokochoko, wivu, unafiki, fitina, nk. Hii kujianika kwenye mabaraza ya watu kukwepa jua kali na kukosa kazi za kufanya ndio inawaletea tabia ya uhasama kwa wanaoishi maisha bora kuliko wewe. LAUMU WANAOKUONGOZA SIO UENEZE LUGHA YA CHUKI KWA WENGINE.

  na Baferoo, Tanga/TZ, - 6.01.09 @ 12:08 | #6137

  CHAMA CHA MAFISADI[CCM]KINAJARIBU KUWAPA
  WATANZANIA PICHA KUWA HAKIHUSIKI NA WI ZI WA FEDHA ZA EPA.MWISHO WAKE HATA WALIOPANDISHWA KIZIMBANI CCM ITASEMA WAMESHINDA KESI HIVYO INABIDI SEREKALI
  IWALIPE.HILO TUNAJUA LAKINI HIVI MTU HUWA
  ANALAZIMISHWA KUPIGIA CCM KURA AU ANACHAGUA MWENYEWE MTU NA CHAMA CHA KUPIGIA KURA?.WATANZANIA ACHENI KUPIGWA CHANGA LA MACHO MCHANA KWEUPE.TUJINASUE KWA HAWA MAFISADI TUSIFANYWE MISUKULE.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi hii CCM bado inadhani ssisi ni wa mwaka 47????????
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Waeleze ukweli jinsi wanamtandao walivyofanikisha ubaguzi wao kwa kubuni wezi wa fedha za kuwahonga wapigakura na kushinda kwa kishindo.kesi za EPA zilizo mahakamani na Kagoda ikifichuliwa zitaweka wazi wizi wa fedha za EPA.Nani alijua kuna fedha za EPA kama si Viongozi wa CCM na Viongozi wa Serikali ambao ni wa CCM.Waliopanga wizi huo ni wao na kufanikishwa na Wahindi wanaokumbatiwa wakijifanya ni wafadhili wa chama kumbe wanatumia fedha walizosaidiwa kuiba.Watanzania msome yatakayoandikwa kuhusu EPA na mtafakari na kuchukua hatua kwa uchaguzi 2010.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Common sense kitu kama sio kweli kwa nini ukivalie njuga,chukulia kama uzushi tuu.
  Naona dhamira inawasuta wanataka kujitakasa,too late
   
Loading...