GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,468
- 108,621
Yaani kabisa (Mtoto) Mvulana au Msichana wa Darasa la Tano hadi la Saba anafuliwa Nguo zake, anaamshwa kwenda Shule, akila anaacha Vyombo mezani House Girl avitoe na anaamshwa Asubuhi kujiandaa kwenda Shule?
Na kinachonishangaza na Kunisikitisha zaidi unakuta Wazazi Wao kipindi cha Utoto (Udogo) Wao wamekula mno Msoto wa Kimalezi kutoka kwa Wazazi na Walezi ambao uliweza Kuwajenga vyema Kiakili na Kimaadili hatimaye leo wameyafikia Mafanikio waliyoyapata.
Nawashukuru mno Wazazi na Walezi wangu ambao kiukweli GENTAMYCINE nilipokuwa Mdogo walikuwa wakinipa (wakinifundisha) Majukumu mbalimbali ya Kimaisha (ya nyumbani na maishani) ambapo kwa Udunduna (Ujinga) wangu Kipindi hicho nilikuwa naona hawanipendi na Wananitesa ila nilivyokuwa na mpaka leo hii najiona ni mwenye bahati ya Kupewa Msoto ule na Wao kwani Wamenijenga vyema Kimalezi, Kiutu, Kiuwajibikaji na Kimaadili pia. Mwenyezi Mungu awabariki mno na sana.
Mitoto ya Siku hizi ikipigwa (ikichapwa) tu kidogo inaanza Kulia na Kudeka halafu Mzazi nae anamuacha na kuanza 'Kumbebisha' Mwanae wakati Kudadadeki enzi zangu GENTAMYCINE nikizingua tu 'Home' nilikuwa nakula Kipigo cha Kishalubela (Kitakatifu) kutoka kwa 'Mshua' na kabla sijakaa sawa Kuugulia (Kusikilizia) Maumivu Mjomba au Mzee wa Jirani nae (nao) wakija walikuwa wakinipa 'Vipondo' vile vile kwanini nisinyooke na kuwa na Adabu?
Tuliolelewa Kiukakamavu (Kijeshi) na Wazazi pamoja na Walezi wetu tumepata Faida Kubwa kuliko hawa Watoto (Vijana na Wasichana) wa Siku hizi (wa leo) ambao wanalelewa 'Kimayai' na 'Kivideo' zaidi ambapo tayari tunaokaa na Jamii tumeshaanza kuona Athari zake ambapo wengi wao ni Wapumbavu (Mapopoma) sana, hawana Adabu na wapo wapo tu.
Mitoto ya Siku hizi hata haipelekwi Vijijini (hasa wakati wa Likizo) ili kujifunza Maisha yote na Likizo zote wanabaki Dar es Salaam na kupelekwa tu Kuzurula katika 'Korido' za 'Mlimani City' wakati enzi zetu akina GENTAMYCINE ikifika tu Likizo Kudadadeki Safari Kijijini kwa akina Babu na Bibi na ukifika huko Unalima, Unachunga Ng'ombe, Unafundishwa Kuvua Samaki Ziwani na kuwakwepa Mamba wasikufanye Kitoweo chao cha Siku na unabeba Maji kutoka Mtoni kwa umbali wa Tegeta Nyuki na Mbagala Kipati na Maisha yanaenda hulalamiki.
Kizazi cha sasa 'Kimeharibika' Kimalezi!!!