Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,440
- 1,029
Siku moja watoto watatu,MWIGULU,NAPE na LUSINDE waliamua kwenda picnic sehemu fulani.Basi wakabeba mazagazaga kibao,misosi na vinywaji vya kutosha.Wakasafiri kwa mguu kwenda eneo la picnic yao umbali wa kama kilometa 10.Walipofika eneo husika wakagundua vinywaji walivyobeba haviwezi kufunguliwa bila opener na kwa bahati mbaya wote walisahau kubeba opener.MWIGULU na NAPE wakamshauri LUSINDE arudi nyumbani kuchukua opener.LUSINDE akakataa akihofu kwamba akiwapa mgongo tu,watapiga misosi yote peke yao. Baada ya kumshawishi sana,LUSINDE akakubali kurudi nyumbani kufuata opener kwa kiapo kwamba hawatakula hata biskuti moja mpaka atakaporejea na opener.MWIGULU na NAPE wakasubiri masaa matatu,LUSINDE hajarudi,masaa 6,masaa 9....,wakaona huu ujinga,tutakufa njaa bure,wakadaka misosi,ile wanajiandaa kuanza kula...mara LUSINDE akakurupuka kutoka kichaka cha jirani huku akisema,'nilijua tu hamtanisubiri na ndo maana sijaenda nyumbani nikajificha hapa kichakani ili niwapime imani zenu,sasa hapa hatumwi mtu na nyumbani siendi ng'o!'.