Rubi , enzi za mwalimu kuna mambo mengi sana. Nakumbuka juu ya maduka ya kaya. Kununua bidhaa kwa foleni. Bidhaa zenyewe adimu, hivyo ikipatikana lazima itunzwe na itumiwe kwa uangalifu. Nakumbuka siku moja wakati nikiwa mdogo baba yangu alinikuta nalamba sukari ambayo alisota sana mpaka kuipata. Nilichapwa viboko ambavyo navikumbuka mpaka leo, miaka mingi ikiwa imepita.