Enzi Jakaya watu waliiba ila na wa chini tulizipata kwenye mzunguko, enzi za Magufuli watu wameiba ila walizificha

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
3,967
12,951
Najaribu kutafakari "wizi" uliotokea awamu zote mbili za JK na JPM.

Wizi sio mzuri ila kuna wizi wa kusaidiana (tuache unafki hili lipo)

Enzi za JK upigaji ulikuwa mwingi, ila wapigaji walikuwa wanaziachia pesa kwenye mzunguko watajenga majumba hapa kila sekta itafaidika mpaka mama ntilie wa mwisho ataipata (ukweli huu tuuamini ulikuwepo na umetusaidia)

Enzi za JPM upigaji tunaambiwa ulikuwa mwingi ila wapigaji pesa walifungia na ndio maana mzunguko ulikuwa mgumu (wajinga wanasema heshima ya pesa imerudi, hakuna kitu kama hicho)

Tuache unafki, nani alitusaidia hapa kati ya JK na JPM.

Na mnaosema mama anaongozwa na JK kama ni kweli basi freshi tu , ni kheri turudi enzi za JK kuliko kubakia enzi za Kayafa.

Sibariki Upigaji ila upigaji upo na ni sehemu ya maisha yetu. Ila Kayafa aliamua kuwa mbinafsi kwa kuiba na genge lake.
 
Rais aunde task force ya kufuatilia hizi fedha kokote ziliko duniani zirudi serikalini. Wastaafu wanahangaika miaka bila mafao kumbe kuna mchwa wanazitafuna vilivyo.
 
Wizi usio na faida kwa wote.

Anayeiba hazifurahii hizo pesa.

Anayeibiwa naye anazidi kuwa kapuku tuu.

Total wastage.
 
Back
Top Bottom