Hamasa zake na uzalendo wa Rais Magufuli kwa taifa naiona Tanzania mpya siku za usoni

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Toka Mh JPM apewe ridhaa na watanzania katika kutuongoza katika kipindi cha miaka mitano kuna kitu tunatakiwa kukielewa na zaidi sana kumuunga mkono kwayo.

Cha kwanza alisema atapambana na Mafisadi wanaoitafuna Nchi kupitia mikataba mibovu,Na kweli sasa tunashuhudia vigogo wakubwa wakifunguliwa mashtaka mbalimbali kwa kulihujumu Taifa.

Pili alisema atafufua Viwanda tayari Viwanda maelfu vimefunguliwa hasa mkoa wa Pwani.

Tatu katika kufufua Viwanda alisema atatatua suala la umeme na kuachana wizi mkubwa kupitia hizi (Power Plants) na kwa kumaanisha tayari mradi mkubwa wa Stiegles kule Rufiji umeanza ambao utazalisha Megewati 2015 na tatizo la umeme Nchini kuwa historia.

Nne alisema Elimu bure msingi hadi secondary na tayari ametekeleza na zaidi sasa hivi kuna maboresho ya kuwa na elimu bora na kutatua changamoto za walimu na vitendea kazi.

Tano mradi mkubwa wa SGR ambao ni lango la uchumi kwa nchi za Rwanda Congo Burundi Zambia Malawi Uganda na Zimbabwe hili lipo sanjali na kuboresha Bandari yetu ili kusiwe na vikwazo kwa wafanyabiashara wa nchi hizi.

Sita wafanyakazi hewa ambalo limekuwa tatizo sugu na mchwa kwa baadhi ya watendaji ambao sio waaminifu lakini zaidi matumizi mabovu ya pesa kama safari,warsha na makongamano mengi ambayo nayo yalikuwa Tatizo kubwa lakini sasa limedhibitiwa .

Saba mwaka huu serikali inakusudia kupeleka muswada Bungeni ili kila Mtanzania hasa wa secta binafsi ambao ni 65% hawana bima za matibabu waweze kuwa nazo.

Nane secta ya Madini ndio ilikuwa shida kubwa kwa mikataba mibovu ambao imeigharimu Taifa sana,Mwaka jana Bunge limebadirisha sheria zote za madini ili sasa na sisi tuweze kunufaika na Madini yetu. Tisa Nchi imerudi kwenye nidhamu kama ilivyokuwa awamu ya kwanza ya Mwl JK Nyerere.

Magufuli ndio kioo cha Taifa kwa hamasa zake ambazo mpaka jana zimefanikisha kupeleka Nchi kwenye michuano ya Afcon nchini misri baada ya miaka 39.

Rai yangu kwa Watanzania wote naomba tumpe ushirikiano Rais wetu Mpendwa kumsadia kwenye maboresho hasa ya Kitaifa ili nchi yetu isonge mbele..JPM KIOO TUELEKEACHO Asanteni tujadli kwa ustaraabu na tuache jazba na matusi 0758 308494

Sent using Jamii Forums mobile app
 
machizi huwa hawaponi pumbv kutwa kucha kusifia tuuuu. hata ukilala na shemeji utasema viva magufuli viva pumbavu
 
Mpya ya wapi wwe,waganda wangekaza mmepata hata sare? Walilegeza sababu walishavuka.
 
Back
Top Bottom