Enzi hizo

dah! mkimnyima namba mwenye mpira anaweka mpira wake kwapani anasepa! dah nakumbuka niliwahii kutoa kucha nilichofanya ni kuweka mchanga kwenye kidonda game likaendelea
 
kama mwenye mpira uliwahi kumnyima kitu basi huo mpira huchezi na ukiwa mbishi mpira unawekwa kwapani halafu anaondoka nao na game inaishia hapo hapo
 
Mimi nilikuwa 'NYANDA' Hakipiti kitu hapo, nikitoka hapo jasho, vumbi na mchanga vyote pamoja na kuoga mpaka nishikiwe bango maana nimechoka sana hehee!!
 
Daaaah! Long time, mtaa kwa mtaa chandimu kinapigwa halafu marehemu brother alikuwa mlinzi (hakipiti kitu!) Those were the best days of my life!! Wish I could turn back the hands of time!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…