Enyi serikali na DAWASCO, kero ya maji Dar hasa Kimara na Mbezi itaisha lini?

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Mwanzo mlisema mwisho wa March, baadaye mkasema May, baadaye July. Yaani imekuwa ni mwendo wa kusogeza tarehe mbele!

Je, shida ni nini? Bomba bado halijamalizika au nini? Ajabu ni kwamba hata zile sehemu tulizokuwa tunapata maji walau mara moja kwa wiki sasa ni miezi inakwenda mitatu hatupati hata tone! Shida ni nini jamani.

Kimara na Mbezi yote, ukiacha baadhi ya watu walio usawa wa si zaidi mita mia tano kutoka Morogoro road maji hayafiki kabisa. Tatizo ni nini? Mbona mwaka jana shida haikuwa kubwa hivi?

Tafadhali sikieni kilio chetu, enyi wahusika, na mtoe taarifa nini kinaendelea!
 
Mcfm40
Ndugu hao jamaa wa Dawasco wanaona wakitupatia maji sisi kwao ni hasara ni bora wawauzie watu wa magari, haingii akili vioski vina maji Kila siku lkn kwenye mabomba yetu hayafiki
 
Kwetu kibamba shida ya maji naweza nikasema imekwisha... japo yanatoka kwa wiki mara mbili lakini ni mengi, na mabomba yamesambaa kwa kila nyumba iliyovuta maji... nashindwa kuelewa kwanini kimara maji yamekuwa shida isiyoisha.
Juzi nimeenda kimara, gorani kwa bibi yangu nimekuta anaosha vyombo kwa maji jagi moja... so sad
 
Waziri wa Maji hebu fuatilia hawa matapeli wa dawasco kwani tumepiga mguu zaidi ya mara 9 pale kimara lakini hakuna msaada HASA SISI WA BARABARA YA MAKABE BAADA YA KUVUKA MTO LIBOKWE. Tuokoe Ndugu waziri kwani sasa wanatuuzia maji kwa magari yao dumu 1 elfu 15.
 
Mnyika anapita humu jukwaani, anapaswa awasilishe hizo hoja kwenye mamlaka husika
 
Mwanzo mlisema mwisho wa March, baadaye mkasema May, baadaye July. Yaani imekuwa ni mwendo wa kusogeza tarehe mbele!
Je shida ni nini? Bomba bado halijamalizika au nini? Ajabu ni kwamba hata zile sehemu tulizokuwa tunapata maji walau mara moja kwa wiki sasa ni miezi inakwenda mitatu hatupati hata tone! Shida ni nini jamani.

Kimara na Mbexi yote, ukiacha baadhi ya watu walio usawa wa si zaidi mita mia tano kutoka Morogoro road maji hayafiki kabisa. Tatizo ni nini? Mbona mwaka jana shida haikuwa kubwa hivi?

Tafadhali sikieni kilio chetu, enyi wshusika, na mtoe taarifa nini kinaendelea!
Mkuu kwa sasa wako busy kuhamia dodoma na pesa zote zimepelekwa huko!!! hawana ela za kuwaletea maji kwa sasa!!
 
Vumilieni tu tunampango mzuri tu kwa wateja wetu tunataka mabomba yenu yatoe maji na maziwa ndio sababu mradi unachelewa.
 
Mkuu kwa sasa wako busy kuhamia dodoma na pesa zote zimepelekwa huko!!! hawana ela za kuwaletea maji kwa sasa!!
Haha. Yaani inatia hasira sana! Kumbe Dawasco wana maslahi na kukosa kwetu maji eeh! Ni kweli kila siku Magari ya maji yanapita mtaani kwetu cha ajabu mambomba yetu hayatoi maji. Wao wanayatoa wapi?
 
Waziri wa Maji hebu fuatilia hawa matapeli wa dawasco kwani tumepiga mguu zaidi ya mara 9 pale kimara lakini hakuna msaada HASA SISI WA BARABARA YA MAKABE BAADA YA KUVUKA MTO LIBOKWE. Tuokoe Ndugu waziri kwani sasa wanatuuzia maji kwa magari yao dumu 1 elfu 15.
Acha tu ndugu yangy. Maji yanauzwa ghali utadhani bia!!!?
 
Dawasco hawana huruma wala hawajali! Nasikia wakati mwingine wanafungulia presdure ndogo makusudi ili tununue kwenye magari yao!
 
Mwanzo mlisema mwisho wa March, baadaye mkasema May, baadaye July. Yaani imekuwa ni mwendo wa kusogeza tarehe mbele!
Je shida ni nini? Bomba bado halijamalizika au nini? Ajabu ni kwamba hata zile sehemu tulizokuwa tunapata maji walau mara moja kwa wiki sasa ni miezi inakwenda mitatu hatupati hata tone! Shida ni nini jamani.

Kimara na Mbexi yote, ukiacha baadhi ya watu walio usawa wa si zaidi mita mia tano kutoka Morogoro road maji hayafiki kabisa. Tatizo ni nini? Mbona mwaka jana shida haikuwa kubwa hivi?

Tafadhali sikieni kilio chetu, enyi wshusika, na mtoe taarifa nini kinaendelea!
NASEMAA MPAKA MUHAMIE DODOMA MKOME KILA MTU KMR MBEZI DODOMA AENDE NANII
 
Bora huko, huku kinyerezi ni Mwendo wa kuchimba visima tu, dawasco haijulikani kabisa huku
 
Mwanzo mlisema mwisho wa March, baadaye mkasema May, baadaye July. Yaani imekuwa ni mwendo wa kusogeza tarehe mbele!
Je shida ni nini? Bomba bado halijamalizika au nini? Ajabu ni kwamba hata zile sehemu tulizokuwa tunapata maji walau mara moja kwa wiki sasa ni miezi inakwenda mitatu hatupati hata tone! Shida ni nini jamani.

Kimara na Mbexi yote, ukiacha baadhi ya watu walio usawa wa si zaidi mita mia tano kutoka Morogoro road maji hayafiki kabisa. Tatizo ni nini? Mbona mwaka jana shida haikuwa kubwa hivi?

Tafadhali sikieni kilio chetu, enyi wshusika, na mtoe taarifa nini kinaendelea!
Mkuu nipo Mbezi Makabe . DAWASCO walituchangisha pesa wakatufungia mabomba. Ila tangu wamefunga mabomba maji yalitokA kama mara 2 tu. Ni miezi 3 imepita. Mpaka sasa hvi hakuna maji. DAWASCO kila siku hawana jibu. Tumehangaika mpaka tumechoka. Hakuna msaada wowote
 
Mkuu nipo Mbezi Makabe . DAWASCO walituchangisha pesa wakatufungia mabomba. Ila tangu wamefunga mabomba maji yalitokA kama mara 2 tu. Ni miezi 3 imepita. Mpaka sasa hvi hakuna maji. DAWASCO kila siku

hawana jibu. Tumehangaika mpaka tumechoka. Hakuna msaada wowote

Sijui wanasikia hiki kilio hawa? Hawa hawatoi taarifa ni nini kinaendelea. Sasa sijui kwa vile walishatuzoesha shida? Kazi kutupa matumaini yasiyokuwepo.
 
Mwanzo mlisema mwisho wa March, baadaye mkasema May, baadaye July. Yaani imekuwa ni mwendo wa kusogeza tarehe mbele!
Je shida ni nini? Bomba bado halijamalizika au nini? Ajabu ni kwamba hata zile sehemu tulizokuwa tunapata maji walau mara moja kwa wiki sasa ni miezi inakwenda mitatu hatupati hata tone! Shida ni nini jamani.

Kimara na Mbexi yote, ukiacha baadhi ya watu walio usawa wa si zaidi mita mia tano kutoka Morogoro road maji hayafiki kabisa. Tatizo ni nini? Mbona mwaka jana shida haikuwa kubwa hivi?

Tafadhali sikieni kilio chetu, enyi wshusika, na mtoe taarifa nini kinaendelea!
Kwa taarifa yako, maji kimara hayawezi kupatikana. Wauza maji wote wametengeneza mtandao wao na watu wa DAWASCO, ili wakate maji wao waje kutuuzia na magari. Jaribu kufanya utafiti utaelewa na kama kuna mtu anabisha alete sababu za kukosekana maji sehemu hizo.
 
Back
Top Bottom