Sorrow to Joy
JF-Expert Member
- Jan 22, 2012
- 292
- 59
Tehe tehe Hamis77, eti wa UD ndiyo wanawasimamia wa DIT&MUST! Ni upogo wa hali ya juu. Nakumbuka enzi zile nikisoma pale DIT nilifaulu vizur O-Level kule Tech school, ila form6 haikuwa first choice nilipenda kusomea ujuzi siyo kukariri tena physics(sisi kule tech sec tukiita Engineering Science) ambayo ni full calculations. Kwa mfano kwa mitaala ya wakati ule, topic kama angular motion, projectile motion, magnetomotive forces(mmf-siyo ile emf ya physics) na mashines tulizisoma secondary, wakati wenzetu wa shule zisizo za ufundi walizikuta kidato cha tano. Kwa hiyo watu wengi tuliotoka tech sec schools mimi nikiwemo na wenzangu wengi tu kutoka Moshi Tech, Tanga Tech, Ifunda,Iyunga na Musoma Tech, tena wengi ni division I za points7 hadi div II. za points 18 tulikutana pale DIT tena ni PCM wote. So baadae wengi walibaki DIT kuchukua ADE na sasa ni BEng ambayo nami nilichukua hiyo na pia kusajiliwa kama Prof Eng na ERB. Bahati ni kwamba wale tuliotoka tech sec school tumekutana kwny game hata za structural design na kwa kweli tunategemeana sana tofauti na story hizi ambazo ni za wanafunz. Watu kama Prof Luhanga, Mwandyosya na hata Mshoro ni product za mwanzo za Dar Tech, bila kusahau Dr Nkwera wa NACTE, ni zao la Mtwara Tech then DIT
namkumbuka prof majani wa uclas(rip) kwamba kuna watu wanafundishwa kuwa punda ( watendaji) na wengine wanafundishwa kufikiri! Kauli nyingine tamu ilitolewa kwenye mahafali ya dit sikumbuki mwaka, na prof mayunga nnkhunya (rip) nesi hawezi ku claim udokta kisa anashinda na kuwajua vzr wagonjwa!
weee ni kiazi sana. Unafahamu tofauti ya gie na ge?? Unadhani kondoro kukubali hii ni kiazi?? Kilaza we
kilaza shangazi yako.
Darius, eti waliomiss A level? Hujui ukisemacho. Yaani yale majembe ambao PCM tulifaulu sana tena division1 za points 7 na kuendekea tuliweka f6 kama chaguo la pili kwa kukwepa kukariri notisi za secondary. Itakumbukwa kuwa f6 ni advanced tu ya f4 siyo taaluma yenye ujuzi. Ni kupoteza muda tu. Kwa hiyo si kweli kuwa eti kwenda DIT au MUST,TCA ni kuwa mtu alikosa nafasi. Form6 na shule ya msingi hamna tofauti siyo kwa ugumu, la bali ni ujuzi, so watu ambao wako focused waliachana nayo, kwani walijua degree utapata tu.
Darius, eti waliomiss A level? Hujui ukisemacho. Yaani yale majembe ambao PCM tulifaulu sana tena division1 za points 7 na kuendekea tuliweka f6 kama chaguo la pili kwa kukwepa kukariri notisi za secondary. Itakumbukwa kuwa f6 ni advanced tu ya f4 siyo taaluma yenye ujuzi. Ni kupoteza muda tu. Kwa hiyo si kweli kuwa eti kwenda DIT au MUST,TCA ni kuwa mtu alikosa nafasi. Form6 na shule ya msingi hamna tofauti siyo kwa ugumu, la bali ni ujuzi, so watu ambao wako focused waliachana nayo, kwani walijua degree utapata tu.
Ubora labda wa mdomoni na kelele, siyo uhalisia. Na ndo maana pale DIT ukitoka f6 unakuka miaka4, ukitoka FTC(kwa wakati ule, sasa ni Diploma) unapiga miaka3 tu kwa nn? So BSc Eng kwanza haipo kiuhalisia kwani hamna sayansi yyte ifanyikayo.
dah hii maada kweli ni tamu sasa hebu tuhamie st joseph jamani kwa mtazamo wangu wanaosoma hapo wako fiti sana kuliko hata dit tena kile chuo kina displine ya hali ya juu so wako vizuri sana kenye civil na computer coz wanatumia mfumo wa india na kama unavyojua india ipo juu sana kwenye field ya engineering!
udsm wanatoa Bachelor of Science in engineering, wakati DIT ni bachelor of engineering. udsm ni designers, dit ni watendaji technicians. huwezi kuwalinganisha maana kazi zao ni tofauti.
sijakudhalilisha mkuu. mimi mwenyewe my huby ni engineer wa DIT. Ila huo ndio ukweli,just accept it.
Kwanza sayansi nini, pili engineering ni nn? Ukijibu maswali haya bila ushabiki utapata jibu. Science imejikita kwenye utafiti na ugunduzi. Ila Engineering ni zao la sayansi yaani Engineering ni Applied Science. Ndo maana vyuo vingi kama Ujerumani na South Africa wanatumia BEng na siyo BSc Eng, kwa kutambua ukweli huo. So hata pale CoET, kuweka B of Sc in Eng ni by the way, hamna sayansi ifundishwayo zaidi ya hizi analytical methods za Engineering ambazo, Sir Isaac Newton, Watts, Pascal na wengine walishafanya.