Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF) limemchagua Eng. Hamad Masoud Hamad kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho leo Februari 22, 2026.
Baraza hilo limeketi leo chini ya mwenyekiti mpya Yusuf Mirambo Camil kwenye Ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam, akiambatana na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Haroub Mohamed Shamis na Makamu Mwenyekiti Bara, Miraji Mtimbwiriko, waliochaguliwa jana.
Mbali na katibu huyo, kikao hicho kimewathibitisha Zainab Amiri Mndolwa kuwa Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi; Mohamed Zuberi Kirungi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Itifaki na Udhibiti na Eng. Mohamed Ngulangwa kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge, Sera na Utafiti.
Pamoja na majukumu hayo, Eng. Mohamed Ngulangwa pia atakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
Awali Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilithibitisha Uteuzi wa Mhe. Eng. Hamad Masoud Hamad na Mhe. Rukia Kassim kuwa wajumbe wa BKUT.
Akitoa hotuba yake ya kwanza Mwenyekiti alisisitiza umuhimu wa Umoja na Mshikamano na kuwa tayari kusahau mabaya yote yaliyopita ili kuhakikisha Chama kinaimarika na kuweza kufikia Malengo yake ya kushika Dola.