Endapo uchaguzi mkuu ukirudiwa!

PURE CRAP! kama huna cha kupost siukae kimya? Aggghhhh!!!!!

najua huna la kusema sababu huna imani kama inawezekana sababu kama Dr Slaa aliongoza ktk majimbo ambayo watu wameelimika hivyo basi katika majimbo ambayo bado wapo gizani tukiwapa mwanga lazima ccm ipotee ktk masikio ya watu kwa mabaya waliyofanya mpaka sasa.
 
Acha kuwatukana mbwa!

Jabulani unanivunja mbavu,ata mbwa wana haki zao sio? Wazungu bwn eti haki za wanyama,ukiwatesa unashitakiwa yaan mauza uza! Mtu ana maisha magumu anawakamata kuku kichwa chini miguu juu akiwapeleka sokoni kuwapiga bei,mgambo hao!,eti kwa nini unawatesa kuku,faini...Cjui kama kwa sheria izi tutafika!
 
Ni miezi miwili imepita tangu Rais achaguliwe ila yaliyofanyika ni machungu kwa wapiga kura kwani yamekuwa kinyume kama ifuatavyo
1. Kupanda bei ya bidhaa mf gesi na mafuta, na umeme
2. Kashfa ya Dowans na ununuzi wa rada
3. Kurusu Arusha kuwe na mgawanyiko wa kisiasa ambao utaleta madhara siku za usoni
Kutokana na sababu izo nilizozitaja kama endapo uchaguzi mkuu ukirudiwa Mh Jk kupata urais ni NDOTO kwani ni miezi miwili imekuwa BORA MAISHA kwa watanzania na sio MAISHA BORA YENYE KUJALI WALE WA TABAKA LA CHINI.
Extremly pure crap! Acha kuota ndoto za mchana.
 
najua huna la kusema sababu huna imani kama inawezekana sababu kama Dr Slaa aliongoza ktk majimbo ambayo watu wameelimika hivyo basi katika majimbo ambayo bado wapo gizani tukiwapa mwanga lazima ccm ipotee ktk masikio ya watu kwa mabaya waliyofanya mpaka sasa.
Mkuu kuwa mkweli slaa aliongoza katika sehemu zenye wakristo wengi. na kwa sbabu kampeni zilikuwa kanisa kwa kanisa ndo maana ikawa hivyo. Si kwa slaa sikiongozi mzuri, big no. Ila watu walionyuma yake ndo tatizo kwetu sisi. Hebu angalia wale watu wakule rukwa walivyotengwa na kanisa, mimi mwenyewe binafsi mbona marafiki zangu wakristo walikuwa wanasema waziwazi? lakini kwa kukukumbusha zaidi ngoja nikumegee kakipande haka kwa mwanankijiji kwenye makala zake, Asante;

Makanisa na viongozi wake dhidi ya JK

Mojawapo ya mambo ambayo yametokea wakati huu wa uchaguzi ni majibizano ya kiana kati ya viongozi wa kanisa na uongozi wa Rais Kikwete. Haijawahi kutokea wakati wowote ambapo viongozi wa kanisa wamekuwa na nguvu na uwezo wa kusema mambo dhidi ya serikali iliyoko madarakani kama wakati huu.

Kwa juu juu tunaweza kuona kuwa kanisa linafanya kazi yake ya 'kinabii'; lakini huu unabii ambao unaonekana kuwa na nguvu wakati wa uongozi wa Muislamu ni unabii wenye mashaka. Viongozi wa Kanisa wamekuwa wakali na wakati mwingine hata kuonyesha mgongano wa wazi dhidi ya Rais Kikwete; ni nani amesahau yaliyotokea Mwanza au yale yaliyotokea Mbeya wakati wa kampeni?
Lakini viongozi hawa hawa hawajahi kutoa tamko lolote dhidi ya yale yaliyofanywa wakati wa utawala wa Rais Mkapa ambaye ni Mkristu. Kashfa za EPA, Meremeta, manunuzi ya Rada na ndege ya Rais vyote vilifanyika wakati wa Mkapa. Lakini hadi hivi sasa haya yanapozungumzwa inakuwa kama yalifanyika chini ya Serikali ya Kikwete.
Hakuna viongozi wa dini ya Kikristo ambao wamekuwa na ujasiri wa kutaka Mkapa na watendaji wake wawajibishwe (hata kama wametoka madarakani). Sasa huu unabii wao unachagua? Sasa Muislamu aelewe nini katika hili? Inakuwaje viongozi hao hao wanajionyesha kuwa ni wakali wakati wa Richmonds/Dowans lakini walikuwa kimya wakati wa ITPL? Kwa nini inaonekana Mkapa alikuwa na nafuu wakati yeye naye ni mtu wa kutoka chama kile kile anachotoka Kikwete wakiwa na sera zile zile za kichama na wakitumia kimsingi watu wale wale?
Lakini safari hii makanisa na viongozi wake walienda mbali zaidi vile vile. Walikuwepo viongozi ambao walizungumza na umma na kufanya mambo ambayo mtu yeyote mwenye akili timamu alijua walikuwa wanamaanisha nini. Wapo ambao ati kwa mara ya kwanza walisitisha ibaza za Jumapili ili waumini wakapige kura; wapo ambao walishindwa kabisa kujizuia na siku ile ya uchaguzi wakizungumza kwa nyuso zenye matabasamu waliwaharikisha waumini wao waende kupiga kura na kufanya 'uamuzi sahihi'.
Dk. Slaa hakuwakemea viongozi wa Kikristo au makundi ya Wakristo yaliyokuwa yanaonekana kumpigia debe wazi.
Misikiti na viongozi wa dini ya Kiislamu

Lilikuwepo hata hivyo kundi jingine nalo ambalo lilikuwa limeapa kabisa kuwa haijalishi itakuwaje lakini 'Mkristo hamuondoi Muislamu'. Kundi hili nalo halikufanya kazi yake kwa kificho; hawa walikuwaja na lengo moja tu nalo ni kumtetea Muislamu 'mwenzao' dhidi ya mbinu chafu dhidi ya makanisa. Ingetosha kama wangekuwa wanajibu uongo au mbinu mbaya dhidi ya Kikwete; lakini wao walienda mbali kwani na wao wakaanzisha mashambulizi dhidi ya Dk. Slaa kwa sababu ya dini yake.

Kwanza walishambulia Ukatoliki wake na vile vile walishambulia upadri wake. Mtu yeyote ambaye alikuwa anafuatilia siasa za Tanzania alikuwa anajua mapema kabisa kuwa Dk. Slaa aliwahi kuwa Padre wa Kikatoliki. Hili halikuwa jambo geni hata kidogo. Lakini lilivyoletwa kwenye kampeni liligeuzwa kuwa Ukatoliki dhidi ya Uislamu; kwamba 'Padri Slaa' ametumwa na Kanisa na hivyo akitawala atatekeleza matakwa ya Kanisa. Na wapo ambao waliamini kabisa hilo kwani lilitoka kwenye magazeti na radio ambazo waliziamini.
Wengine walienda mbele na kusambaza nyaraka kwenye misikiti wakitaka waislamu wajitokeze kwa wingi kupiga kura ili 'makafiri' wasije kumuingiza mtu wao. Mambo yaliyofanywa na baadhi ya wachungaji na mapadri makanisani ili kumuinua Slaa yalifanywa na baadhi ya mashehe na maimamu misikitini ili kumuinua Kikwete. Na kinachoshangaza hayakuwa siri! Haya wala hayakuhitaji 'deep cover' ili mtu aweze kuyafichua. Yalifanywa na mengine bado yanafanyika mchana kweupe.
Kikwete hakuwakemea viongozi wa Kiislamu au makundi ya Waislamu ambayo yalionekana kumpigia debe wazi wazi.
Ningeweza kwenda mbele zaidi lakini hapa itoshe kudokeza kuwa udini huu bado upo na msingi wake kama nilivyosema ni ujinga. Udini huu hautaondolewa kwa kunuia au kwa kusema 'tuachane na udini'. Ingekuwa ni rahisi hivyo, ubaguzi wa rangi ungetokomezwa kwa kusema 'tuachane na ubaguzi wa rangi'. Kama vile kauli za 'uzembe haufai' haziwezi kuondoa uzembe vivyo hivyo kauli tunazosikia kuwa 'Watanzania waachane na udini' haziwezi kuuondoa udini.
Kumbuka kama nilivyosema udini msingi wake ni ujinga. Hadi hivi sasa hakuna hatua zozote za makusudi na za kijasiri zilizochukuliwa ili kushughulikia udini. Unaweza kufikiria kwamba ukiwakamata wenye kupandikiza udini basi unakomesha udini. Hili si kweli hata kidogo. Udini hauwezi kuondolewa kwa kuwakemea wahusika au kwa kuwatia pingu watu - sijui kama tuna magereza ya kutosha labda siku hizi chache baada ya msamaha wa Rais!
Tusipoamua kwa dhati kushughulikia huu udini tunaliandaa taifa letu kuendelea kuwa katika mpasuko wa kudumu utakaokuwa unajirudia rudia kila baada ya miaka mitano au kila wakati ambapo wagombea wawili watakuwa wanatoka dini tofauti.
Na ukiangalia vizuri utaona kuwa hisia hizi sasa zimetoka kwenye siasa tu na kuanza kugusa ajira na mahusiano ya karibu. Wakati wananchi wa kawaida wanashirikiana bila kuulizana dini au kujali dini ya mtu mwingine wasomi wetu na watawala wetu wanazidi kusukumiza hii sumu taratibu.
Ndugu zangu, udini hauwezi kutoka hivi hivi; na kwa kadiri ya kwamba watawala wetu hawataki kuuita udini kwa jina lake halisi (ubaguzi wa kidini) wataendelea kujaribu kuficha vichwa vyao mchangani kama mbuni. Lakini hali ilipo sasa ni mbaya kwani yawezekana kuna mtu kaingia madarakani tena kwa sababu ya dini yake au kuna mtu kakataliwa kwa sababu ya dini yake. Vyovyote vile ilivyo, tunajenga msingi mbaya sana wa siasa zetu huko mbeleni maana tusipoangalia itabidi tuanze kuulizana dini kabla mtu hajaajiriwa ili watu wa dini fulani wasiwe wengi mahali fulani. Tutafikia mwisho tutakuwa tayari kupewe kiongozi ambaye hana uwezo alimradi tu ni wa dini yetu.
Nimesema kwa kirefu kuwa udini wetu Tanzania ni wa kijinga; lakini, jambo linaloendana na hilo ni kuwa udini uliopo Tanzania ni wa viongozi. Wadini halisi wa nchi hii siyo Wamachinga, vijana mitaani, kina mama na baba sokoni na wananchi vijijini! La hasha, wadini wa nchi hii wamehitimu katika vyuo mbalimbali, wanavaa tai na suti na wanaheshimiwa kama viongozi wa kada mbalimbali. Wadini wa Tanzania kundi la viongozi wa kisiasa, viongozi wa kidini na watendaji wa taasisi mbalimbali. Ndio hawa walioanzisha udini, ndio wanaupalilia, na ndio hawa hawa wanaotarajia kuvuna matunda yake. Na wao wenyewe wanaamini kabisa kuwa wanasema vitu vya 'kisomi' kumbe wanathibitisha tu kile kilicho wazi; ujinga unaohitaji kuondolewa kwa haraka.
Wakati umefika tuanze kuwakataa, kuwapinga na kuwabeza wanapomwaga sumu yao huku wakichanganya na kimombo ili kuonekana wanasema jambo la maana. Kama mabadu zetu waliondoa tofauti zao za kilugha, kikabila na kidini wakaunganishwa na imani ya kuukataa utawala wa Mjerumaini kwenye vita ya majimaji, zimefika zama sasa Watanzania wenye kujali Utanzania wao hasa kuwakataa na kuwapinga viongozi wadini ambao wanazungumza lugha za kidini, wanaovumilia udini na ambao wanaendelea kuchochea udini kiana. Ukitaka kumjua ni nani mdini - waulize wanaposema 'udini' wanamzungumzia nani! - Utaona kama watawataja watu wa dini zao! Ndio alama ya wadini wetu, kwamba udini uko kwa watu wa dini nyingine tu siyo kwao wenyewe na siyo kwa watu wa dini yao! Ni Udini wa Kijinga.
 
Back
Top Bottom