Emmanuel Nchimbi atalipa kisasi

Huyo GS mgeni wa CCM si mtu mwaminifu kwa Mamlaka hata japo kwa kiasi, na ndiyo maana alimgomea Kikwete na maamuzi yake ya 2015. Mbaya zaidi, alimgomea huku akiimba na mapambio kwa kupayuka na wazi akitambua alikuwa akifanya usaliti!

Nimhakikishie Samia, atambue anaye GS muunda makundi na asiye chelea kuunda maasi na asiye na uvumilivu hata kidogo!

Kingine, kwa hulka ya Emmanuel ni wazi pia hataweza kufanya kazi kwa amani na Paul Makonda. Hivyo, ni suala la mda tu wawili hao wataumizana na mmoja wao lazima atampisha nwingine kwa kupangiwa kazi nyingine.

Kwa hakika ya nafsi yangu, Nchimbi anaenda kutengeneza makundi ndani ya Chama kama ilivyo kawaida yake.
Sana hata mimi mawazo yangu ni hayo ni kama demu alikusaliti halafu unaamua kumrudia eti amejirekebisha hakuna kitunkama hicho, huyu atakuja kuwasumbua
 
Siyo kweli, Emmanuel Nchimbi huwa ni mwadilifu sana kwa mamlaka inayompa nafasi. Kumhukumukwa tukio la 2015 ni kukosa ufahamu wa siasa za Tanzania. Kwani ni mbunge gani wa CCM au mwanasiasa wa CCM ambaye hakuwa anamuunga Edward Lowassa mwaka 2015? Ni Kikwette tu na ndiyo maana walipoimba wimbo "tunaimani na Lowassa akapiga makofi'. Ile ni ajali tu katika siasa
Napenda Loyalty ya Dr Nchimbi, hakuweza kumsaliti Lowassa. Safi sana.
 
Makundi lazima yawepo,

Chama hakiwezi kupoa kama kiporo cha ugali,
Huku Bashite huku Mchimbi, Kuna January na Madelu Mchemba,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Umeiweka vizuri...chama cha siasa lazima kiwe na makundi ndani..makundi yanasaidia ku shape mwelekeo wa chama na kufanya walio madarakani wasijisahau kwani humo chamani wapo wenye kuzitaka hizo nafasi.

Wabongo tuache fikra za kwamba tafauti ya mawazo ni uasi....uasi iwe ni kukiuka katiba!
 
Paulo Makonda anaondoka, Nchimbi amesema anapenda mijadala na watu wenye akili, sasa Makonda hana akili.

And, indeed, Makonda will be ousted unceremoniously.

Alikataa pema pa Chongolo, sasa kaletewa mwamba.
Alikataa pema pa Chongolo? Alikataaje?
 
Siyo kweli, Emmanuel Nchimbi huwa ni mwadilifu sana kwa mamlaka inayompa nafasi. Kumhukumukwa tukio la 2015 ni kukosa ufahamu wa siasa za Tanzania. Kwani ni mbunge gani wa CCM au mwanasiasa wa CCM ambaye hakuwa anamuunga Edward Lowassa mwaka 2015? Ni Kikwette tu na ndiyo maana walipoimba wimbo "tunaimani na Lowassa akapiga makofi'. Ile ni ajali tu katika siasa
Bado kuna watu wanaamini nchimbi kumuunga lowasa ilikua ajali ya kisiasa!na waliomuunga mkono membe je!!?

Ule ni mchoro kama maigizo mengine!

Mimi namuona nchimbi kama waziri wa mambo ya ndani ndani ya CCM,kama unakumbuka vizuri akiwa waziri was mambo ya ndani alifanya Nini Bas ndicho anachoenda fanya ndani ya CCM!!

Vuta kumbu kumbu!
 
Mimi huwa nashindwa kuwaelewa watu huenda ni tatizo langu pekee maana Nchimbi anashambuliwa kwa kuwa alijitokeza hadharani kupinga mchakato wa kuteua mgombea urais 2015 yeye akiwa timu Lowasa.Kwangu mimi inaonesha jinsi alivyo na msimamo na asiyeyumbishwa kwa kile anachokiamini.CCM ndio waliopata athari za moja kwa moja kutokana na msimamo huo wa Nchimbi kwa wakati ule lakini hao hao CCM ndio tena wameamua kumteua kuwa GS wao sioni shida hapo.
 
Tatizo lako usukuma unakusumbua.
Nchimbi angekuwa Msukuma wala usingeanzisha uzi
Kwahiyo na wewe unaamini nchimbi yupo pale kumsaidia mama awe Raise awamu nyingine!!?

Alichomfanyia lowasa akaukosa urais ndicho atamfanyia mama!

We unafikiri nchimbi alikua timu Lowasa na sio team "maamuzi ya wakubwa DS"!!?

Chongolo alikua loyal kwa jk na mama,huyu yupo loyal kimantiki Kwa mama lakini deep down in loyal Kwa wale jamaa wenye maamuzi!!

Nchimbi anakuja kuwamaliza wasiotakiwa na wenye mfumo wao!

Subiri utaona!!
 
Huyo GS mgeni wa CCM si mtu mwaminifu kwa Mamlaka hata japo kwa kiasi, na ndiyo maana alimgomea Kikwete na maamuzi yake ya 2015. Mbaya zaidi, alimgomea huku akiimba na mapambio kwa kupayuka na wazi akitambua alikuwa akifanya usaliti!

Nimhakikishie Samia, atambue anaye GS muunda makundi na asiye chelea kuunda maasi na asiye na uvumilivu hata kidogo!

Kingine, kwa hulka ya Emmanuel ni wazi pia hataweza kufanya kazi kwa amani na Paul Makonda. Hivyo, ni suala la muda tu wawili hao wataumizana na mmoja wao lazima atampisha nwingine kwa kupangiwa kazi nyingine.

Kwa hakika ya nafsi yangu, Nchimbi anaenda kutengeneza makundi ndani ya chama kama ilivyo kawaida yake.
Kwa hiyo unataka mtu mwerevu Dr.Nchimbi, aweze kufanya kazi na mtu mjinga Bwn.Bashite ili iweje yan???
 
Inaelekea humjui Emanuel Nchimbi.Alikuwa anatumia haki yake ya kidemokrasia.

Haya mengine ni speculation tu isiyokuwa na uzito wowote. Yaani unamjua Nchimbi kuliko CCM? Katika watu wanaoijua CCM vizuri ni Nchimbi ameanza nayo tokea akiwa chipukizi. Hizo ni assumptions za fisi kungojea mkono udondoke.
Anaelewa fika ccm hakuna kitu inaitwa demokrasia..wana kuuubaliana tu ila ye kwa kiburi aligoma kukubaliana. Ndio maana hata yeye ameanza kampeni kwa samia ya vipindi viwili, anajua sio suala la kidemokrasia.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Inaelekea humjui Emanuel Nchimbi.Alikuwa anatumia haki yake ya kidemokrasia.

Haya mengine ni speculation tu isiyokuwa na uzito wowote. Yaani unamjua Nchimbi kuliko CCM? Katika watu wanaoijua CCM vizuri ni Nchimbi ameanza nayo tokea akiwa chipukizi. Hizo ni assumptions za fisi kungojea mkono udondoke.
Na kwa kuongezea, CCM hakuna mtu ambaye ni mkubwa kuliko chama, vinginevyo Chongolo angesalimishwa na ukubwa wake.
 
Bado kuna watu wanaamini nchimbi kumuunga lowasa ilikua ajali ya kisiasa!na waliomuunga mkono membe je!!?

Ule ni mchoro kama maigizo mengine!

Mimi namuona nchimbi kama waziri wa mambo ya ndani ndani ya CCM,kama unakumbuka vizuri akiwa waziri was mambo ya ndani alifanya Nini Bas ndicho anachoenda fanya ndani ya CCM!!

Vuta kumbu kumbu!
Sands of times!! Nchimbi hawezi kuwa loyal kwa Lowassa kwa kuwa aliyempa uteuzi ni Samia. Akifanya hivyo anastahili kupelekwa Mirembe hospital
 
Paulo Makonda anaondoka, Nchimbi amesema anapenda mijadala na watu wenye akili, sasa Makonda hana akili.

And, indeed, Makonda will be ousted unceremoniously.

Alikataa pema pa Chongolo, sasa kaletewa mwamba.
Tatizo mnaongea mambo msiyoyajua mkifikiri mnayajua. Ebu fuatilia ndani ya UVCCM uone kama Nchimbi na Makonda kama hawakuwahi kufanya kazi pamoja.
 
Sands of times!! Nchimbi hawezi kuwa loyal kwa Lowassa kwa kuwa aliyempa uteuzi ni Samia. Akifanya hivyo anastahili kupelekwa Mirembe hospital
Ishu ninkwamba atakua loyal kwake huku akivujisha mipango Kwa wale jamaa!

Hata jpm aliwaamini watu lakini wakawa wanatoa info site hadi deal done!!

Unapokua mkubwa mataarifa ni mengi Hadi kuchakata unashindwa umwamini yupi!!

Kwa hizo kauli ni rasmi jamaa anamwaminisha mteuzi kwamba nipo upande wako lakini mteuzi hawezi jua jamaa anawaza nini!!

Jpm aliimbwa sana kwa style hii hii Tena zaidi lakini mambo yakavuja sana!!
 
Nchimbi ni sawa na ‘soldier of fortune’ (mercenary) vita ikiisha anaangalia biashara ingine, mkataba na Lowassa uliisha 2015.

Ila hii vita ya 2025 kama ita kuwepo awatoiweza iwapo chaguo ni mtu maalum wa kurekebisha dira na sioni wa kumsumbua ‘Bi Tozo’ zaidi ya Mwinyi.

Just a theory not factual
Kwani fomu si inatoka moja tu na chama kimeishajipanga kupokea fomu moja tu hiyo hiyo!?.

Tulisema upinzani hakuna demokrasia kwa sababu unaongozwa na wafalme badala ya viongozi, sasa kimewarudi CCM hao hao kwamba 2025 Malkia/Mfalme anaendelea kwa fomu moja, sijui hii nayo ni kukosa demokrasia ndani ya CCM au!?

Hii habari ya fomu moja pia walimletea Magufuli 2020 akawatimua akasema CCM siyo mali binafsi yake kwamba kama 2015 Kikwete angeendekeza kanuni ya fomu moja je, yeye Magufuli angekuwa rais?

Baada ya kauli yake hiyo na kufungulia watu wachukuwe fomu, kilichofuata ni kuwa wote waliokuwa na kiu ya kuchukuwa fomu wakajipima na kujitathmini upya na kuamua kujiondoa woooote akabaki Magufuli pekee.

Nadhani dhana ya fomu moja ni dhana ya uoga na mtu kujiona hatoshi na utendaji wake kumsuta mwenyewe.
 
Nchimbi aliitwa kujitetea na akakiri na kuomba msamaha kwa sauti ya unyenyekevu sana. Kwangu ninaona ni bora mtu akiriye na kuomba msamaha. Nchimbi ni kama Nape - January Makamba ndiyo gaidi - huyu jamaa hawezi kabisa kubow down!
Kamati ya Maadili ya CCM inatisha kuliko Mahakama ya Rufaa; japo haina jela.
 
Huwa nafananishaga sana umakini na misimamo ya Mh.Nchimbi na misimamo ya Hayati Mzee Mkapa.

Infact I see a lot of Benjamin Mkapa in Emmanuel Nchimbi.

Nadhani mama akimaliza muda wake hiyo 2025 akabidhiwe Nchimbi. He is presidential material
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom