Sana hata mimi mawazo yangu ni hayo ni kama demu alikusaliti halafu unaamua kumrudia eti amejirekebisha hakuna kitunkama hicho, huyu atakuja kuwasumbuaHuyo GS mgeni wa CCM si mtu mwaminifu kwa Mamlaka hata japo kwa kiasi, na ndiyo maana alimgomea Kikwete na maamuzi yake ya 2015. Mbaya zaidi, alimgomea huku akiimba na mapambio kwa kupayuka na wazi akitambua alikuwa akifanya usaliti!
Nimhakikishie Samia, atambue anaye GS muunda makundi na asiye chelea kuunda maasi na asiye na uvumilivu hata kidogo!
Kingine, kwa hulka ya Emmanuel ni wazi pia hataweza kufanya kazi kwa amani na Paul Makonda. Hivyo, ni suala la mda tu wawili hao wataumizana na mmoja wao lazima atampisha nwingine kwa kupangiwa kazi nyingine.
Kwa hakika ya nafsi yangu, Nchimbi anaenda kutengeneza makundi ndani ya Chama kama ilivyo kawaida yake.