Itachukua miaka mingi sana kwa Upinzani kushinda uchaguzi na kuunda serikali, hasa Serikali ya Muungano. Sababu kubwa ni kwamba, upinzani unatumia muda mwingi sana kutamka neno CCM badala ya hata jina la chama chao wenyewe. Ukweli ni kwamba, wanapofanya hivyo (kwa kudhani wanaibomoa CCM), wanakuwa wanaijenga zaidi. Na ndio maana CCM haina lolote la kusema kuhusiana na kutumika kwa jina lao (maana wanajua ni kwa manufaa yao). Vivyo hivyo, wananchi wengi wenye hasira na CCM hulitamka sana jina hilo. Hivyo watu wengi hujaribu kutafuta habari zaidi kuhusiana na CCM. Hii inafanya watu wengi wajue CCM kuliko chama kingine chochote cha siasa. Labda ndio maana hata Mh. Rais alisema, inawezekana upinzani usishinde kabisa na kuongoza nchi.
Ndugu zangu siasa ni ngumu sana, hasa ukiwa mpya kwenye uwanja huo. Wengi wetu tunadhani wananchi wanaopiga kelele kuhusu CCM wanaichukia. Sio kweli. Ukweli ni kwamba, wanatamani CCM mpya tu, basi. Hata humu ndani wapo wengi wanaosema CCM haifai, ila ikifika uchaguzi wanaichagua tena kwenye ngazi zote. Hilo sio kosa. Kosa ni kuchagua kiongozi usie na imani ya uwezo wake.
Uchaguzi huru na wa haki hautegemei International observer kuamua kama ulikuwa huru na wa haki. Uhuru na u-haki wa kuchagua unaanzia kwenye fursa ya kushiriki kwenye kuchagua, kuchagua kwenyewe na hatimae matokeo na jinsi yanavyotolewa. SI lazima uchaguzi huru na wa haki uwe ni ule tu ambao serikali iliyopo madarakani inaposhindwa.