Ni kweli leo hii ukimchukua mwanafunzi wa chuo kikuu ni aibu mtu hata kujieleza hawezi cjui tatzo nini, hata ukimpataia mada aielezee ni shida kibaya zai vitendo ni ziro,ukienda makazin mtu unakuta anafanyiwa matazamio mwaka mzima what do you means? je problem kwa government,Society or personal student??Mfumo wa elimu unatatizo kwa sababu upo kinadharia kuliko vitendo hivyo hushindwa kuwaanda vijana kukabili soko la ajira.
Pia tatizo la ajira nchini linasababishwa na uwezo mdogo wa uchimi wetu. Hatuna sekta za uzalishaji ambazo vinaweza kuajiri watu wengi. Watu wengi wanategemea kuajiriwa serikalini na wachache katika sekta binafsi.
Kutegemea kuingiza bidhaa (import) husababisha ukosefu wa ajira katika sekta ya uzalishaji kwasababu nchi haina viwanda vinavyoajiri watu kwa ajira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja.
Uwepo wa sera ya ajira isiyo linda maslahi ya wazawa, pia kushindwa kuwabana wawekezaji katika kuajiri vijana wa tanzania.Pia kushindwa kusimamia sera ya ajira ya taifa.
Mfumo wa elimu upo kinadharia kuliko vitendo hivyo waajiri wengi wanataka watu wenye uzoefu ili wawapate kuwa na uzoefu kivitendo kuliko kinadharia. Hebu fikiria vijana wamehitimu masomo wakiomba kazi wanaambiwa Wanataka uzoefu wa muda flani hivi, sasa mtu ametoka chuo atapata wapi uzoefu ili aweze kuajiriwa?, wakati hata kazi za kujitolea hawapati, sasa huo uzoefu atapata wapi?
ni kwi mkuu watu wanasomea mitihan na si kuelewa ni shidaaaMfumo wa elimu c mbaya kihivo. content ni kubwa tu. kuna tatizo la jitihada binafsi ya anayesoma. mtu anayejitxhidi na ana malengo ya dhati kujua kitu mfano lugha atajua vizuri tu. wanafunzi wengi wanakariri tu kwa ajili ya mtihani. pindi hakuna mitihani kusoma huwa ni kama adhabu.
Watu wanapenda sana starehe ngonjera ngonjera. kusoma ni nadra sana.