Elimu yetu

Oct 13, 2018
35
259
RUGE YUPO TANGA ANAFUNDISHA FURSA VIJANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Mwaka Jana Siku kama ya Leo niliandika kuwa Huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu wakikimbizana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitwa Fursa. Najiuliza pale Mlimani wanafundisha nini? Najiuliza pale SUA wanafundisha nn? Najiuliza shule zetu za A Level wanafundisha nn? Huku ngazi za chini kunafundishwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofundishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu Nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindwa kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuka falsafa yetu ya elimu inasemaje?

#Trend ipo hivi wanaomaliza Darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliza form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliza form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi.

Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Hatuna clear Philosophy inayotuongoza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehitimu hata darasa la Saba aweze kujitegemea kwa kutumia fursa zinazomzunguka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofundisha au kufundishwa mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

#Shule zetu zilizokuwa zinafundisha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendelea kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

#Ibn Khladun Mwanafalsafa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukaririsha watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.

Kwake yeye content zilizokuwa zikifundishwa zilikuwa nyingi ni za kukaririshwa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunukiwa cheti

Hiki ndicho tunachokiona leo katika jamii yetu, atakayeweza kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgrade kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaandaliwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrade kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha.

#John Dewey huyu ni mwanafalsafa wa kiamerika yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzunguka mwanafunzi.

Hiki mdicho kinachofanyika kwa wenzetu wazungu, wanatemgeneza mitaala yao kulingana na kinachowazunguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavyo.

#Sisi tumengangania kufundisha na kakaririshana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote.....

Je tutaendelea kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

Je jukumu la kufundishwa content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundisha Fursa?

#Ukiona semina za kufundishana Fursa kama hizi zikishamiri sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

#Mikopo yote ya kujisomesha tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambia waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendeleza.

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosimamia miradi utakuta ni wachina wanazisimamia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technolojia yaani watu wanawaza kuuza Technolojia zaidi kuliko Korosho na wanatengeneza fedha.

Technolojia hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundisha Kinjekitile Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengeneza Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayomsaidia baadaye.

#Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikisha tunakokutamani vinginevyo tutakuwa tukihangaika kila mahali kutafuta wawekezaji.

Hizi Reli tunazojenga na Barabara zinakuja kuwarahisihia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kisafirishia huko gunia mia za Korosho au Karanga. Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

#Naamini sisi tunaozunguka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibarikiwa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsiri mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambui.

#Swala la msingi la Kujiuliza tutaanza Kubadilika Lini?

Ole Mushi.

0712702602
IMG_20181021_093446_555.JPG
 
Uzi kama huu huwezi kukuta "Watu" wanachangia! Ingekuwa sijui Diamond amemla denda Wema Sepetu mpaka sasa Reply na Views zingekuwa laki moja! Hili Taifa lina "Watu" wa hovyo na IQ ndogo kupindukia na hasa tunaowadekeza eti "Viongozi wetu"!
Chukulia issue kama ya " MO DEWJI" ni aibu kwa Taifa! Watu ambao tumewaamini na kuwapa Mamlaka wanafanya "Usanii" wa kishamba na "kum- frustrate" Local Investor na Potential ambaye ni Icon kama huyu kwa "Kumteka" na kumdhalilisha mbele ya Dunia! Nani anaweza kutuamini sisi Watanzania!

MO Dewji hapa Tanzania alikuwa anaelekea kuwa kama Alhaji Aliko Dangote kule Nigeria! Inasemekana pale Nigeria huwezi kusimama zaidi ya dakika 10 katika barabara yoyote iwe ni Lagos,Abuja,Kano au Enugu yaani Miji yote bila kupitwa na Lorry la Alhaji Aliko Dangote,ama limebeba cement,au Chumvi au Mafuta au Sukari au Mbolea au Tomato Sauce ama bidhaa nyingine! Na MO Dewji kadhalika hapa Nchini Kwetu! MO Dewji anasambaza bidhaa nyingi sana hapa Nchini!

Hata hii SGR tunayojenga kwa "Mbwembwe" ni Watu kama kina MO Dewji ndo wanaweza kui-utilize na kutupa faida kwa kuacha kutumia Ma-lorry kusafirisha bidhaa na badala yake kutumia SGR!

Sasa tuna "Washamba" wanadhani ukishakuwa na treni ya umeme au ya mwendokasi basi itakuwa tu inakimbia kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda hata bila bidhaa wala abiria nakurudi na hayo ndo maendeleo ya "Vi-wonder"! Aibu sana!
 
Mleta mada umezungumza jambo la msingi lakini Mimi ninachoamini, Tanzania tuna tatizo la kijamii zaidi ya tatizo la kimfumo
 
Hakika umenena kweli tupu, huwa najiuliza maswali mengi kuhusu aina ya elimu tuliyonayo bila kupata majibu. Uzuri kuna walio mbele yetu; kama tungefata njia zao, angalau basi kwa kuchambua yale yanayokwenda sambamba na mazingira yetu ingesaidia sana. Lakini hili la kumkalilisha mtu eti mzungu fulani ndiye aliyegundua ziwa fulani au mlima upi, sijui itatufikisha wapi! Binafsi nilichosomea sicho nifanyacho baada ya kuona hakina tija, ila nimehamia kwa kitu ambacho nilifanya tangu utotoni, ambacho nakipenda.
Still a long way off...
 
Mkuu umeongea fact tupu nadhani tatizo lipo sasa kwa waliopewa mamlaka ya kusimamie elimu nchi ....wakaechini wajitafakari tunawezaje kutoka katika hii hali tuliyonayo of course itatuchukua muda kufika kwenye ya vitendo na kumjengea uwezo mwanafunzi lakin naamini tuanze tu taratibu sio fahari kujisifu tunatoa elimu bure na kuwa na shule nyingi ilihali product inayotoka hapo haina faida yoyote katika jamii
 
Amani ya bwana iwe nanyi,

Mkuu umetoa hoja ya msingi sana lakini kingine mfumo wetu wa elimu unatakiwa ubadilishwe badala ya kumuandaa mwanafunzi ili aje kuwa job seeker basi tumuandae ili aje kuwa job creator katika nyanja mbalimbali, pamoja na hilo vilevile inatakiwa tuwekeze nguvu zetu katika vyuo vya kati ambavyo vinatoa taaluma inayoendana na mazingira tunayoishi, nadhani tukizingatia hili tutafika mbali sana.
 
Chukulia issue kama ya " MO DEWJI" ni aibu kwa Taifa! Watu ambao tumewaamini na kuwapa Mamlaka wanafanya "Usanii" wa kishamba na "kum- frustrate" Local Investor na Potential ambaye ni Icon kama huyu kwa "Kumteka" na kumdhalilisha mbele ya Dunia! Nani anaweza kutuamini sisi Watanzania! MO Dewji hapa Tanzania alikuwa anaelekea kuwa kama Alhaji Aliko Dangote kule Nigeria! Inasemekana pale Nigeria huwezi kusimama zaidi ya dakika 10 katika barabara yoyote iwe ni Lagos,Abuja,Kano au Enugu yaani Mini yote bila kupitwa na Lorry la Alhaji Aliko Dangote,ama limebeba cement,au Chumvi au Mafuta au Sukari au Mbolea au Tomato Sauce ama bidhaa nyingine! Na MO Dewji kadhalika hapa Nchini Kwetu! MO Dewji anasambaza bidhaa nyingi sana hapa Nchini!
Hata hii SGR tunayojenga kwa "Mbwembwe" ni Watu kama kina MO Dewji ndo wanaweza kui-utilize na kutupa faida kwa kuacha kutumia Ma-lorry kusafirisha bidhaa na badala yake kutumia SGR!
Sasa tuna "Washamba" wanadhani ukishakuwa na treni ya umeme au ya mwendokasi basi itakuwa tu inakimbia kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda hata bila bidhaa waka abiria nakurudi na hayo ndo maendeleo ya "Vi-wonder"! Aibu sana!
Kiongozi umetema madini mno big up sana.
 
1. Hivyo vitabu tu vya akina Dr. Livingston, Mkwawa, ....tunakoseakosea kuviandika mpaka ma-prof wanakunja sura bungeni katika kuvitetea.
2. Hiyo hiyo elimu ya kukariri, mwanafunzi anatumia miaka 13 ili aweze kusoma na kuandika (2+7+4).
3. Tuongeze juhudi kujenga 'mabanda' na kuyapa hadhi, vyeo kama shule za sekondari za kata, shule ya msingi, ...
 
RUGE YUPO TANGA ANAFUNDISHA FURSA VIJANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Mwaka Jana Siku kama ya Leo niliandika kuwa Huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu wakikimbizana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitwa Fursa. Najiuliza pale Mlimani wanafundisha nini? Najiuliza pale SUA wanafundisha nn? Najiuliza shule zetu za A Level wanafundisha nn? Huku ngazi za chini kunafundishwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofundishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu Nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindwa kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuka falsafa yetu ya elimu inasemaje?

#Trend ipo hivi wanaomaliza Darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliza form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliza form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi.

Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Hatuna clear Philosophy inayotuongoza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehitimu hata darasa la Saba aweze kujitegemea kwa kutumia fursa zinazomzunguka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofundisha au kufundishwa mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

#Shule zetu zilizokuwa zinafundisha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendelea kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

#Ibn Khladun Mwanafalsafa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukaririsha watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.

Kwake yeye content zilizokuwa zikifundishwa zilikuwa nyingi ni za kukaririshwa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunukiwa cheti

Hiki ndicho tunachokiona leo katika jamii yetu, atakayeweza kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgrade kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaandaliwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrade kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha.

#John Dewey huyu ni mwanafalsafa wa kiamerika yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzunguka mwanafunzi.

Hiki mdicho kinachofanyika kwa wenzetu wazungu, wanatemgeneza mitaala yao kulingana na kinachowazunguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavyo.

#Sisi tumengangania kufundisha na kakaririshana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote.....

Je tutaendelea kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

Je jukumu la kufundishwa content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundisha Fursa?

#Ukiona semina za kufundishana Fursa kama hizi zikishamiri sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

#Mikopo yote ya kujisomesha tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambia waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendeleza.

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosimamia miradi utakuta ni wachina wanazisimamia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technolojia yaani watu wanawaza kuuza Technolojia zaidi kuliko Korosho na wanatengeneza fedha.

Technolojia hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundisha Kinjekitile Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengeneza Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayomsaidia baadaye.

#Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikisha tunakokutamani vinginevyo tutakuwa tukihangaika kila mahali kutafuta wawekezaji.

Hizi Reli tunazojenga na Barabara zinakuja kuwarahisihia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kisafirishia huko gunia mia za Korosho au Karanga. Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

#Naamini sisi tunaozunguka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibarikiwa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsiri mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambui.

#Swala la msingi la Kujiuliza tutaanza Kubadilika Lini?

Ole Mushi.

0712702602View attachment 905683
Hoja kama hizi ziko katika kutujenga zaidi safi sana kiongozi.
 
Kama
Uzi kama huu huwezi kukuta "Watu" wanachangia! Ingekuwa sijui Diamond amemla denda Wema Sepetu mpaka sasa Reply na Views zingekuwa laki moja! Hili Taifa lina "Watu" wa hovyo na IQ ndogo kupindukia na hasa tunaowadekeza eti "Viongozi wetu"![/QUOTE KAMANDA umewaza kitu kikubwa saana
 
Walimu hawathaminiwi,wanakandamizwa tu.Unadhani watawafundisha vijana wa kitanzania ili waweze kukabiliana na mifumo ya kujiwezesha?
Na vip curriculum inaeleweka?
 
gud meseji mkuu... bila google yani umeandika kwa hisi kali mno, hope uwe na nafasi wizara fulani japokuwa wengi wakifika uko wanajisahau.... all the best mkuu
 
Safi sana Ole....Umeitoa kule 'jamvini kwetu' hadi huku.Good move tujisahihishe kama Taifa
 
Asante ndugu,,mi niende moja kwa moja kwenye ,,"Tuanze kubadilika lini,?;"

,"Nadhani tuanze kubadilika sasa," tatizo la elimu yetu sio philosophy, tunatumia falsafa ya COMPETENCE BASED ambayo tumeinyumbua kutoka kwenye falsafa bora zaidi duniani ya PRAGMATISM EDUCATION BASED PHILOSOPHY, ambayo hata EDUCATION FOR SELF RELIENCE ni tawi lake,,tatizo letu lipo kwe Curriculum (mitaala) yetu haiendani na falsafa yetu ya elimu,,COMPETENCE BASE PHILOSOPHY huwez mkuta mwanafunz anakaa kwenye vyumba vya madarasa badala yake anatakiwa awe,,mashambani kujifunza kilimo bora,,karakana kujifunza ufundi stadi,,madarsa yanatakiwa yawe ni mashambani,,mabanda ya kuku na ng'ombe,masokoni ,migodini,baharini na kwenye mito na maziwa,,,,
Nini kifanyike?.
Mtoto akigraduate kama hajafanikiwa darasa la saba kwenda form one,,wapelekwe VETA ,,wakimaliza form four kama combination ya mtoto sio kwenda ENGENEARING,DOCTOR,PILOT, wapelekwe VETA wote na wale ambao hawajapass ,,,waalimu waandaliwe kuandaa watoto kivitendo zaidi pia tupunguze mambo mengi yasyo na tija kwenye vitabu vya KIADA na masomo ya stadi za kaz,tehama na haiba na michezo yapelekewee vifaa na pawe na penalt kwenye CA Continous Assessment ya masomo hayo,,,,ELIMU YETU NCHI YETU,,,asanteni
 
Back
Top Bottom