Elimu ya wabunge wetu imechangia kutufikisha hapa tulipo

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,165
1,309
Katika kipindi cha miaka mingi watanzania tumeona na kusikia wabunge wetu wanavyo toa maamuzi yenye utata ktk masuala nyeti yanayohusu nchi yetu .Tumeona kwenye kwenye bunge la katiba na kupitisha sheria mbalimbali . Je ni kitu gani kinawapelekea wabunge wetu kutoa au kukubali uamuzi wenye kasoro, Kwanza kabisa ni Elimu , upeo wa elimu ya walio wengi ni mdogo sana na matokeo yake katika mijadala muhimu utaona uchangiaji wao ni dharau na kebehi kwa wabunge wengine na mwisho huenda akamalizia na uchekeshaji,
Sijamsikia Zitto ,Bashe au Tundu lissu akichekesha chekesha wabunge. Wabunge wetu wengi wamedoda sana katika masuala ya kitaifa na kimataifa hata wanapochangia kitu fulani wanashindwa kutoa reference kwenye sehemu nyingine au nchi nyingine.Utasikia mbunge anasema wale walio tia sahihi mikataba ya madini wahukumiwe kunyongwa , je na wale waliopiga kura za ndio kwenye miswada yenye utata tuwafanye nini
 
Back
Top Bottom