Elimu ya Vito ndani ya Maandiko ya kale

Elimu ya Vito ndani ya Maandiko ya kale

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
ELIMU YA VITO NDANI YA MAANDIKO YA KALE.

Tutaangazia maandiko kutoka kwenye Kitabu cha cha Mafumbo (The Book of Codes) maarufu Biblia.

Bila shaka mnajua kwa nini The Bible ni 'the most authentic book' na nilishasema mara nyingi sana, kwa nini napenda kuirejelea.

Msiojua au mliosahau niulizeni.

This is my favourable book anyway.

Nimefanya Bible Research wakati nafanya Masters ya Theology & Divinity, najua safari ya hiki kitabu, tangu mwaka 325AD.

Tuendelee . . .

Kwenye Biblia (The Book of Laws), wanazuoni, wanaizungumzia milango 12 ya mbinguni, lakini kimsingi (basically) wanazungumzia habari za milango 12 ya Nyota, kwa sababu kule kunakoitwa mbinguni ni kwenye ulimwengu wa kinyota (cosmic/ astral world)

Wanasema kila mlango umetengenezwa kwa VITO VYA THAMANI (gemstones), kila mlango tofauti na mwingine!

Inabidi utumie kichwa (akili/ elimu) badala ya moyo (Imani/ hisia) kufumbua fumbo hili.

Mwandishi anazungumzia Vito vinavyoendana na Nyota lakini katika mkutadha wa kile ambacho yeye alikusudia kukiwasilisha kwa wasomaji wake.

Ni muhimu watu wajue kuwa Biblia si kitabu cha dini fulani, ni kitabu cha mafumbo kwa karne nyingi.
Kina mafumbo (siri) ambayo ukiyafumbua utafanikiwa kwenye haya maisha.

Ndio maana ukienda makanisani utakikuta.

Misikitini utakikuta.

Kwenye mahekalu na masinagogi utakikuta.

Kwenye secret societies kipo pia.

Kwa waganga wa kienyeji utakikuta.

Kwa wachawi kipo.

Kwa wasio na dini utakikuta mpaka wengine wanakitumia kama 'mto' (pillow) kulalia ili wasisumbuliwe na wachawi!🤪

Mimi na wanautambuzi wengine tunakiita THE BOOK OF LAWS (Kitabu cha Sheria/ Kanuni) na ni the most authentic book!

Sasa kwenye hicho kitabu, ukisoma utaona kinawazungumzia wataalam au wabobevu wa masuala ya Nyota (the wisemen) au mamajusi (kiswahili), kuwa walipokuwa huko kwao Mesopotamia (Iran ya sasa), waliiona Nyota ya Simba (Leo) ikiangaza kwenye ulimwengu wa kinyota (cosmic World) na kwa kutumia vifaa vyao vya kazi, kwa mujibu wa teknolojia ya wakati ule, wakaanza kuifuatilia mpaka walipofika Bethlehem ya Uyahudi alipokuwa amezaliwa Yesu Kristo, almaarufu Bwana Yesu!

KUNA AINA TANO ZA KUSOMA NYOTA YA MTU, MIE NAJUA NNE NA UWA NAFUNDISHA MBILI TU.

Kuna dimensions mbalimbali za kinyota, wengine wanasema mtu ana nyota nyingi, ni sawa tu; lakini the accurate ni ile ya sun sign, ambayo inazingatia birth date na hapo ndipo tunapata kile tunachokiita NATAL/ BIRTH CHART.
Wote humu ndani mnaelewa bila shaka, what's all about the Natal Chart!

Tuendelee . . .

Hao the 'wisemen' walifuata utaratibu wa kidiplomasia mpaka wakafika mahali pale alipozaliwa Yesu, wakakaribishwa ndani.

Kabla hawajafanya lolote WALIMSUJUDIA!

Kwa nini?

Ili wasamehewe dhambi?
HAPANA!

Ili waokolewe?
HAPANA!

Ili iweje sasa?

Kwa nini wakisujudie kichanga kilicholala bila kutambua lolote?

JIBU: Hawakuwa wakisujudia kichanga, bali nyota ya utawala (ufalme), ambayo ni Nyota ya Simba (Leo zodiac sign)

Mfalme husujudiwa!

Mtu hawi Mfalme baada ya kuwa Mfalme, anakuwa Mfalme kwa asili yake, yaani kwa kuzaliwa!

Mfalme ni Mtawala, ni kiongozi wa watu, ndivyo ilivyo Nyota ya Simba!

Kwenye dini, Yesu anaitwa Simba wa KABILA la Yuda, yaani Mtawala au Mfalme wa Wayahudi!

Waswahili wamemwimbia nyimbo "Simba wa Yuda anaunguruma" nafikiri walimaanisha Mfalme anatoa amri au maelekezo!

Wale mamajusi (the wisemen) baada ya kukaa kwa siku kadhaa, kabla hawajaondoka, walifungua mizigo (hazina) yao wakachukua DHAHABU pamoja na UVUMBA na MANEMANE, wakawakabidhi wazazi wa Yesu kisha wakaondoka.

Kwa nini Dhahabu na si madini mengine?

Kwa sababu DHAHABU pamoja na mambo mengine, hutumika kufyonza nishati hasi (nguvu mbaya) kwa watu wa nyota ya Simba, lakini pia huvuta nguvu ya kifalme kutoka kwa Mfalme Jua ambaye ndiye Mtawala wa Nyota ya Simba!
Kwa hiyo watu wenye nyota ya Simba wakivaa miilini mwao vitu vya madini ya Dhahabu kama Pete, Cheni, Bracelets nk, wanakuwa wanajikinga na mambo mengi mabaya, lakini pia inawasaidia kung'arisha nyota zao kama Jua na kuwafanya wawe na mvuto usio wa kawaida..

UVUMBA na MANEMANE ni mafusho ambayo huchomwa ili kuondoa nuksi, mikosi, mabalaa na mambo mabaya mabaya kwa watu wa nyota ya Simba.
Kwenye mafusho ya Nyota ya Simba, uwa ni lazima tutie ndani uvumba na manemane, kwa sababu ndani yake kuna energy ya utakaso wa nyota husika.

Ndio maana the wisemen (mamajusi) waliacha hizo bidhaa kwa ajili ya Yesu, ili atimize kusudi lake.

Tafuta Biblia usome Matthew 2:1-9,11

Imeandikwa;
"Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
"Yuko wapi yeye aliyezaliwa MFALME WA WAYAHUDI?
Kwa maana TULIIONA NYOTA YAKE MASHARIKI, nasi tumekuja kumsujudia."
Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii kusema;
"Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa KWAKO ATATOKA MTAWALA Atakayewachunga watu wangu Israeli."
Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, "Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie."

Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; DHAHABU na UVUMBA na MANEMANE."

Soma kwa utulivu utaelewa kwa nini kila mtu anawakilishwa na Nyota fulani!

Wewe unapokuwa ndipo na nyota yako inapokuwa.
Wewe na Nyota yako ni UMOJA, you're inseparable.
Kwa lugha rahisi nyota yako ni wewe na wewe ni nyota yako.

Ili mtu mbaya akuharibie, hahitaji mambo mengi, bali kuijua nyota yako na kucheza nayo, maana Nyota ikifanyiwa 'ulozi' ni wewe unakuwa umelogwa.

Ndio maana wale wanaosema tutakuombea nyota yako irudi, ni waongo wakubwa!

Wale pia wanaosema watakupa hirizi ili nyota yako ing'are ni matapeli kama matapeli wengine. Wote hao ni wapigaji!

Kwa nini?

1. Hakuna maombi ya kurejesha nyota.

2. Hakuna hirizi au dawa za aina moja zinazosafisha nyota zote.

Nyota haiibiwi kabisa wala haichukuliwi; isipokuwa inaweza kufunikwa, kuzibwa na kuchafuliwa.

Kama itaibiwa au kuchukuliwa, basi mtu atakuwa chizi, zezeta au msukule (namaanisha machoni kama mtu, lakini kiuhalisia anakuwa sio mtu)

ELEWA HILO, WALA USIJE UKADANGANYWA!

Pia Kila Nyota husafishwa na aina tofauti ya visafishaji au vitakasaji (zodiac cleansers), ingawa baadhi ya Nyota kwa sbb za 'mfanano' wake kwa namna moja au nyingine, zinaweza kutakaswa, kuoshwa, kusafishwa kwa madini/ mawe/ Vito vya aina fulani na au mafusho yanayofanana, kama vile Nyota za Ng'ombe (Taurus) na Mapacha (Gemini) hung'arishwa na madini ya ZUMARIDI (Emerald)

Ngoja niwaletee na maandiko mengine yanayozungumzia mawe au vito muone umuhimu au faida ya kuwa navyo.

VITO NA MADINI MAARUFU AMBAVYO BIBLIA INADAI NDIVYO VIMETUMIKA KUUJENGA MJI MTAKATIFU WA MBINGUNI:

1. Kuna Gold (Dhahabu)

2. Diamond (Almasi)

3. Jasper (Yaspi),

4. Sapphire (Yakuti),

5. Chalcedony (Kalkedoni),

6. Emerald (Zumaridi),

7. Sardonyx (Sadoniki),

8. Sardius (Sardio),

9. Chrysolite (Krizolite),

10. Beryl (Berili),

11. Topaz (Topaz),

12. Chrysoprasus (Krisopraso),

13. Jacinth (Yakintho)

na

14. Amethyst (Amethisto)

Ni kwa mujibu wa Kitabu cha Ufunuo (Revelation 21:10-22)

"Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa KITO CHENYE THAMANI NYINGI kama kito cha YASPI, safi kama bilauri;
ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.
Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.

Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.
Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya YASPI, na mji ule ulikuwa wa DHAHABU safi, mfano wa kioo safi.
Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa VITO VYA THAMANI vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa YASPI; wa pili YAKUTI SAMAWI; wa tatu KALKEDONI; wa nne ZUMARIDI;
wa tano SARDONIKI; wa sita AKIKI; wa saba KRISOLITHO; wa nane ZABARAJADI; wa kenda YAKUTI YA MANJANO; wa kumi KRISOPRASO; wa kumi na moja HIAKINTHO; wa kumi na mbili AMETHISTO.

Na ile milango kumi na miwili ni LULU kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni DHAHABU safi kama kioo kiangavu.

Kuna kitu mmekielewa?

Kitu gani hicho)

Tueleze kwa ufupi.

Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA ☠️ 💀 (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
downloadfile-6.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom