Elimu ya Uzalendo ihimizwe kwa wananchi

Elimu ya Uzalendo ihimizwe kwa wananchi

AjunaFelix

New Member
Joined
Jul 29, 2018
Posts
2
Reaction score
6
NAOMBA SERIKALI IHIMIZE ELIMU YA UZALENDO KWA WANANCHI WAKE.
Na Felix Ajuna

Kuna muda nakaa nafikiria nchi yangu natamani sana serikali ingehimiza zaidi juu ya Elimu ya uzalendo ilihali tukiimiza upendo wa nchi yetu na kufuata mila na tamaduni zetu kama watanzania.

Kiukweli ili tufikie mafanikio lazima tuwe wazalendo wa kweli na sio wazalendo wa mdomoni, Tukijifunza kwa baadhi ya nchi zilizoendelea hua wanatanguliza utaifa kwanza mengine baadae sisi huku tunatanguliza umimi kwanza utaifa baadae jambo ambalo sio rafiki sana kwa afya ya maendeleo ya nchi.

Kutokana na kukosa uzalendo kwa Taifa ndio maana unaona mambo mengi yanakua hayaendi mfano, unakuta mtu anaamua kuiba tu chuma Cha kutengenezea daraja ili akatengeneze jiko, maana hana uchungu na Hilo daraja, ukienda maeneo mengi matendo kama hayo hutokea hii ni kutokana na watu kutokua na uchungu na Taifa.

Kuna mataifa watu huishi kimila kijamii na kitaifa, mfano: kijana anaweza kutumwa kupambana kwaajili ya maendeleo ya jamii yake, nchi yake n.k, na akaweza kufanyahvyo ni kwasababu anaamini kuwa jamii yake aliyoishi yano inauzalendo wa kuweza kuisaidia familia yake, kuwatunza watoto wake n.k bila matatizo yeyote au madhara yeyote. Ila tukiangalia jamii yetu kiukweli uzalendo ni mdogo sana kijana akitumwa kwenda kupambana kwa ajili ya jamii yake au Taifa na akaacha familia anaweza rudi akakuta Kuna mambo kashasaidiwa. Hii yote pengine ni kutokua na uzalendo.

Leo angalia asilimia kubwa ya watu wanaopata nafasi wapo kwaajili ya masilahi yao binafsi na sio ya jamii au Taifa, hii itaendelea kizazi hadi kizazi kama serikali haito liangalia suala hili kwa jicho la pili, inaweza kupelekea Taifa kushindwa kuendelea.

Kiukweli kunamahali tunakwama kabisa, Leo unaweza kuta muhibiri rushwa ndio mla rushwa mkubwa kwa style hii si tunatengeneza kizazi kibovu kwenye jamii.

Leo watu ambao ni wazalendo wa Taifa lao ndio wanaonekana washamba mfano: mtu kapewa mradi fulani akakamilisha mradi pasina kuiba hata shillingi huyu anaonekana mshamba ila yule ambae ataiba na kujinufaisha yeye ataonekana ndio mjanja dah,,

Kama tutakua wazalendo wa kweli tunaweza kusaidia kuleta maendeleo kwa haraka na kufika mbali, lakini pia hatuta wapa maadui nafasi ya kuweza kuingilia mambo yetu, na kutuharibia nchi yetu.

#uzalendokwanza
#utaifakwanza
#mungu wabariki viongozi
#mungu ibariki Tanzania

felixajuna9@gmail.com
0762625515
JamiiForums445062523.jpg
 
0762625515View attachment 2050975
Hii Hali imeota mizizi miaka na Miaka, pia ikihanikizwa na wenye nafasi ya kuonyesha njia ndio wanageuka waziba njia. Kuna shida kubwa kwenye siasa za kiafrika na tawala zake, upo utepetevu mkubwa kwenye uzingatiaji wa Sheria taratibu, kanuni na hata katiba zetu. Jambo linalovunja moyo na kukatisha tamaa walio wengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom