Elimu ya tanzania

mazingira magumu ya shule ( No infrastructures, no teachers, books/hakuna vitabu maalum kwa wanafunzi watunzi kibao nao ni wezi). Inasikitisha sana ukitembelea shule za sekondari vijijini au hata za msingi wanafunzi wanaenda kucheza tu. hakuna uwiano kati za shule za msingi na mijini.
 
Nikitugani kinachangia elimu ya tanzania izidi kushuka?

Kikubwa ni kutojifahamu na kutokukubali ukweli. Kila mtanzania anajifanya anajua. Wapo wachache wanaoigiza, wanajua kuwa hawajui ila inabidi waigize kuwa wanajua. Wapo majority hawajui kuwa hawajui au wanajua kidogo na wanafikiri wanajua sana. Sasa hii ndio aina ya watu inayoendesha serikali katika kila nyanja. Tunaishia kuchemsha tu. Mtu kapata digrii kwa kudesa anakuwa rais, mwingine waziri, mwingine mwalimu, na kila mmoja anaonyesha kuwa anajua sana, hasa wakati wa kufukuzia ile kazi. Baadaye mnagundua kuwa hana shule yuko sawa tu kama wengine, ila ndio hamuwezi kumfukukuza. Badala yake mnaajiri mtendaji/mwalimu mwingine ambaye naye anaonyesha anajua kumbe naye hamna kitu.

Chunguza sana, utaona kuwa watu wanajifanya wanashule, kumbe hamna kitu. Sasa dizaini hizo ndio wanafundisha kwanzia shule ya msingi hadi chuo. Na ni dizaini hizo ndio wanakuwa watendaji wa serikali, mpaka kwenye wizara zinazohusika na elimu. Nani atarekebisha? Walio kwenye sekta ya elimu moja kwa moja hawaoni matatizo, walio serikalini ambao wangeweza kurekebisha huo mfumo huo wa elimu kwa kujifanya kujua kwao, wanaishia kutoona hayo matatizo.

Kifupi ni kwamba tumeliwa....
 
Back
Top Bottom