Elimu ya Msingi sasa Miaka 6

Elimu ya Msingi sasa Miaka 6

Huku mtu hadi miaka 28 bado anafukuzia degree wkt nchi za wenzetu 28 alishafanya hadi Phd.
 
walicho kosea ni kufanya mtihani wa hesabu kwa ku shedi majibu. Linatengenezwa bomu fulanj ambalo litakuja kuwa hatari baadae
Yaani sijui ccm huwa wanawaza nini kwenye ushindani wa kitaaluma hapa duniani.
 
Kila mtu apambane na Elimu ya mwanae.
Msisitizo hapa ni kuangalia mustakabali wa taifa. Wenzako huko kwa mtoto mmoja mmoja wa kila mzazi walishavuka kitambo.Ni taifa dhidi ya taifa na siyo mtoto wa fulani dhidi ya mtoto wa mwingine.Ni mtazamo mpana zaidi wenye maslahi ya kitaifa.
 
haya sasa ndio mapinduzi ya kielimu, tija sio kukaa muda mrefuu darasani (miaka saba) bali tija ni kuwa msingi bora wa kusonga mbele, hivyo hata miaka mitano ilikuwa ina tosha.
 
Matayarisho ya sera hii ya linaanza kushirikisha wa dau mwaka 2008 na kukamilika 2014. Maadiliko yaka an za mwaka 2015 kwa kubadilisha mita ala ya std 1& 2 kisha 3&4 na 5&6 imefanyika mapema mwaka huu. Pia mafunzo ya mabadiliko ya mitàala kwa darasa la awali ili fanyika mwaka huu mwanzoni.
 
Sera ipo mtandaoni naomba wadau ipakueni na kusoma. Sera omeondoa elimu ya msingi (primary education) na kuwa elim msingi ( basic education) na mfumo huo unabadiloka kutoka 1+7+4 +2 +3+ na kuwa 1+10 +2 +3+. Sera hii sasa in a raja kuwa elimu ya chini ni kidato cha nne. Hivyo mwanafunzi anapoanza darasa la awali ambalo kwa mujibu wa sera hii ni lazima (compulsory) ataendelea na shule had kidato cha nne (nonstop,). Mabadiliko haya yameanza kwa kuboresha viwango vya walimu viendane na sera kwa kuwataka walimu wote wenye grade A wawe na kiwango cha elimu ya diploma na kuendelea. Hata vyuo vya ualimu havitoi tena course ya Grade A.
 
Mabadiliko haya yangekuwa yafanya ke mwaka 2019 ila waziri wa elimu alishasitisha kutokana Changamoto za miundombinu na walimu. Hasa kuwezesha madarasa mwili std vi na vii kuingia kidato cha kwanza kwa pamoja. Pia miundombinu haijaansaliwa kumudu Idadi ya watoto watakao hitajika kuingia form I.
 
Sa
Sera mpya ya elimu inayotarajiwa kuanza kutumika muda wowote kuanzia sasa pale matayarisho yatakapokamilika, pamoja na mambo mengine inatarajiwa kupunguza muda wa kusoma elimu ya msingi kutoka miaka 7 ya sasa hadi miaka 6.

Kwa mujibu wa Naibu waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda, sera hiyo iliyozinduliwa na Rais Kikwete mwaka 2014 itaanza kutekelezwa hapa nchini mara baada ya maandalizi ya utekelezaji wake kukamilika. Chini ya sera hiyo mfumo mpya wa elimu utakuwa 1+6+4+2+3+ yani mwaka mmoja wa chekechea, miaka sita shule ya msingi, miaka minne sekondari (0-level), miaka miwili sekondari (A-level), na miaka mitatu au zaidi ya elimu ya juu, badala ya mfumo wa sasa wa 1+7+4+2+3+.

[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]:
Naipongeza serikali kwa sera hii mpya ya elimu. Ukweli ni kwamba maika 7 ilikuwa mingi sana kwa elimu ya msingi. Inafika mahali mnaanza kurudiarudia tu mambo yaleyale. Mimi nilipokuwa darasa la 5 nilikuwa najaribu kufanya mitihani ya darasa la 7 na ninafaulu. So naamini tukiwawezesha vizuri watoto wetu na kuweka mikakati bora ya elimu miaka 6 inawatosha kabisa.

Suala la msingi tuboreshe maslahi ya walimu na tuwalipe stahiki zao zote ili wawe na moyo wa ufundishaji, then tuboreshe miundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa, na tuhakikishe mtaala wa elimu unaandaliwa vizuri katikia namna itakayomfanya mwanafunzi amalize darasa la sita akiwa na uelewa wa mambo anuai.

Wingi wa miaka sio tija sana. Leo tuna watoto wanasoma miaka 7 na bado wanaenda sekondari hawajui kusoma wala kuandika. Unajiuliza wamefaulu vipi. So jibu hapa ni kwamba bado miundombinu ya elimu, maslahi ya walimu na mtaala wa elimu havijaboreshwa. Mtoto wa namna hii hata akikaa darasani miaka 10 bado hawezi kubadilika.

Sera hii mpya ya elimu itasaidia kupunguza muda wa kukaa shuleni na hivyo kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao mapema.

Nchi nyingi zilizoendelea wamerahisisha mfumo wa elimu. Kwa muda mfupi unakuta mtu ameshahitimu masomo yake. Unakutana na kijana ana miaka 19 tayari ni graduate, ana degree yake moja. Wakati hapa bongo miaka 19 jitu liko form 3 au form 2. Hapo bado hujafeli form 4 uanze kupiga mark time za kureseat. Yani hadi unakuja kupata degree na mvi zimeota.

Kwa hiyo naipongeza sana serikali na naitaka ikamilishe maandalizi haraka ili sera hiyo ianze mapema iwezekanavyo.!
safi sana maana watu sasa wanazeeka mapema
 
Back
Top Bottom