Elimu ya Msingi sasa Miaka 6

Elimu ya Msingi sasa Miaka 6

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Sera mpya ya elimu inayotarajiwa kuanza kutumika muda wowote kuanzia sasa pale matayarisho yatakapokamilika, pamoja na mambo mengine inatarajiwa kupunguza muda wa kusoma elimu ya msingi kutoka miaka 7 ya sasa hadi miaka 6.

Kwa mujibu wa Naibu waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda, sera hiyo iliyozinduliwa na Rais Kikwete mwaka 2014 itaanza kutekelezwa hapa nchini mara baada ya maandalizi ya utekelezaji wake kukamilika. Chini ya sera hiyo mfumo mpya wa elimu utakuwa 1+6+4+2+3+ yani mwaka mmoja wa chekechea, miaka sita shule ya msingi, miaka minne sekondari (0-level), miaka miwili sekondari (A-level), na miaka mitatu au zaidi ya elimu ya juu, badala ya mfumo wa sasa wa 1+7+4+2+3+.

[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]:
Naipongeza serikali kwa sera hii mpya ya elimu. Ukweli ni kwamba maika 7 ilikuwa mingi sana kwa elimu ya msingi. Inafika mahali mnaanza kurudiarudia tu mambo yaleyale. Mimi nilipokuwa darasa la 5 nilikuwa najaribu kufanya mitihani ya darasa la 7 na ninafaulu. So naamini tukiwawezesha vizuri watoto wetu na kuweka mikakati bora ya elimu miaka 6 inawatosha kabisa.

Suala la msingi tuboreshe maslahi ya walimu na tuwalipe stahiki zao zote ili wawe na moyo wa ufundishaji, then tuboreshe miundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa, na tuhakikishe mtaala wa elimu unaandaliwa vizuri katikia namna itakayomfanya mwanafunzi amalize darasa la sita akiwa na uelewa wa mambo anuai.

Wingi wa miaka sio tija sana. Leo tuna watoto wanasoma miaka 7 na bado wanaenda sekondari hawajui kusoma wala kuandika. Unajiuliza wamefaulu vipi. So jibu hapa ni kwamba bado miundombinu ya elimu, maslahi ya walimu na mtaala wa elimu havijaboreshwa. Mtoto wa namna hii hata akikaa darasani miaka 10 bado hawezi kubadilika.

Sera hii mpya ya elimu itasaidia kupunguza muda wa kukaa shuleni na hivyo kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao mapema.

Nchi nyingi zilizoendelea wamerahisisha mfumo wa elimu. Kwa muda mfupi unakuta mtu ameshahitimu masomo yake. Unakutana na kijana ana miaka 19 tayari ni graduate, ana degree yake moja. Wakati hapa bongo miaka 19 jitu liko form 3 au form 2. Hapo bado hujafeli form 4 uanze kupiga mark time za kureseat. Yani hadi unakuja kupata degree na mvi zimeota.

Kwa hiyo naipongeza sana serikali na naitaka ikamilishe maandalizi haraka ili sera hiyo ianze mapema iwezekanavyo.!
 
Wazanzibar wao toka 2014 wameanza kuitumia kwahivyo wao hakuna kitu Standard seven kitambo sana so wametutangulia
 
Hiyo mbona imeshaanza muda mrefu sana. Mwaka wa tatu huu toka iingie sokoni.
 
Tuna sera na mikakati mingi lakini, mara zote tunaenda mbele na kurudi nyum...

Cc: mahondaw
 
Tatizo sio darasa .Tatizo walimu Kwanza waboreshewe kipato chao
 
Duuuh kwa hiyo LY itakuwa standard six
 
watu wanajibalaguza
Bila malsai mazuri yakilinganishwa na sekta nyingine tutamaliza nguvu bure
 
Secondary o-level iwe 3years halafu advance napo iwe 3 yrs ( advance kuna topic ndeeefu ambazo bila tuition huwez cover, organic chemistry ..kina benzene na matakataka yake yoote, practical za physics n.k) au vinginevyo baadhi ya topic zifutwe
 
Kila mtu apambane na Elimu ya mwanae.
 
Hata hiyo miaka 4 kwa olevel ni mingi mpaka sasa kuna shule wao ufundisha masomo ya form 1 kwa miezi 3 baada ya hapo uingia f2 na bado ufaulu vizur kidato cha 4
 
Itafaa sana, kwani miaka saba ilikua ni kupotezeana mda tu, ila pia walimu waongeze juhudi ya kufundisha, maana kuna shule hizo, hata hiyo miaka saba ni michache, unakuta mwanafunzi yupo la tano au sita lakini hajui kusoma wala kuandika, hivyo bila juhudi kwa walimu wa shule kama hizo hii sera itakua mzigo kwa wanafunzi wa shule husika.
 
Hiyo mbona imeshaanza muda mrefu sana. Mwaka wa tatu huu toka iingie sokoni.
Unazungumzia nchi gani mkuu? Mbona mwaka juzi na mwaka jana watoto wamefika darasa la saba?
 
Huo mfumo ulishaanza nadhani wanafunzi waliopo darasa la tatu sasa wataishia la sita kama sikosei.
 
Back
Top Bottom