kwenye hili jamani kuna tatizo. Kwa sababu ukianzisha mjadala huu - TCU wanakuambia ndio wenye madaraka. Lakini madaraka hayo ya kukaa kimya bila kuhakiki hizo degree za wenzetu sijui ni madaraka gani. Lazima tufikie mahali kila mwenye degree hata kama ameipata nje kabla ya kuajiriwa hapa home awe ameisajili kwenye rejesta maalum. Hii itasaidia pia kujua tuna wenye degree wangapi. Maana sasa ina katisha tamaa kwa wale wanaosoma na kukatwa maksi vyuoni kwa sababu tu lecturer hujaongea nae vizuri na wenzio wanazipata kwa njia ya mkato. Sijui kwa staili hii kama tutafika pamoja na hiyo ari zaidi, nguvu zaidi.