Bajeti ni mpango unaogawanya mapato kwenye matumizi mbalimbali
Ni mpango unaoonyesha mchanganuo wa mapato na matumizi kwa ajili ya jambo au mambo yanayotarajiwa kufanywa.
Ni muhtasari wa makadirio ya mapato na jinsi yatakavyotumika ndani ya muda ulioweka.
Vile vile bajeti ni matarajio au makisio ya mapato na matumizi
UMUHIMU WA BAJETI
Inarahisisha kufanya maamuzi ya namna ya kufanya matumizi na kuweka akiba
Inasaidia kuwa na matumizi ya tahadhari kufuatana na mapato
Inasaidia kuwa na nidhamu ya kujiwekea akiba.
Kama ikizingatiwa, inasaidia kufikia malengo ya kifedha mtu aliyojiweka
Inasaidia kuwa na usimamizi mzuri wa fedha
MUUNDO WA BAJETI
Bajeti ina sehemu kuu mbili nazo ni;-
i. Mapato
Hapa unahorodhesha mapato yako yote ambayo unategemea kupata katika kipindi husika, mfano, mshahara, kusuka, kufua nguo, kuuza nguo n.k baada ya hapo unapata jumla ya mapato sehemu ya kwanza
ii. Matumizi
Hapa pia unaweka jinsi utakavyo tumia mapato yako hapo juu mfano, nauli, chakula, vocha, unapata jumla, baada ya jumla lazima uweke kipengele cha AKIBA
Jambo ya mwisho ni unachukua mapato unatoa matumizi kujua kama una ziada au pungufu.
BAJETI YA NYUMBANI NA BIASHARA
Bajeti ya nyumbani ni mpango unaoonyesha mchanganuo wa mapato na matumizi muhimu kwa ajili ya shughuli au mambo ya nyumbani
Bajeti ya biashara ni ile ambayo inahusu shughuli mbalimbali zinazohusiana na mapato na matumizi muhimu yaliyoelekezwa kwenye biashara husika.
UMUHIMU WA KUTENGANISHA BAJETI YA NYUMBANI NA BIASHARA
Kujua mapato halisi yatokanayo na biashara na kuweza kuainisha matumizi yake
Kujua matumizi halisi ya nyumbani na kuweza kuyatofautisha na ya biashara
HITAJI LA LAZIMA NA HITAJI LISILO LA LAZIMA
HITAJI LA LAZIMA ni kile kitu ambacho ukikosa huwezi kuishi mfano chakula, nyumba
HITAJI LISILOLAZIMA ni kile kitu ambacho ukikosa utaendelea na maisha kawaida mfano vilevi, starehe
Mahitaji kua lazima au sio lazima inategemea mtu na mtu mfano kuna mtu kulingana na shughuli zake gari ni hitai la lazima na mtu mwingine sio lazima.
KALENDA YA MSIMU
Kalenda ya misimu ni dhana ambayo inasaidia kuonyesha mapato na matumizi kwa kuendana na miezi AU msimu fulani
Inasaidia kuonyesha mapato ya kila mwezi na namna matumizi yanavyokuwa.
Vile vile huonyesha uhalisia wa vyanzo mbali mbali vya matumizi
Huonesha miezi ambayo kuna uzidio wa kipato au uzidio wa matumizi
Husaidia mtu kujipanga kujua miezi ambayo kipato ni kidogo ataishi vipi kwa kuweka akiba miezi yenye kipato kikubwa.