MAANA YA MKOPO
- Mkopo* ni fedha ambayo taasisi za fedha au za mikopo zinatoa kwa wateja wake ili kukidhi mahitaji ya msingi/mtaji na kwa ajili ya kuboresha biashara.
- Pia ni fedha ambayo mkopaji anaweza kuitumia katika kipindi cha muda mfupi au ndani ya kipindi cha muda fulani, ambapo atatakiwa kufanya marejesho kulingana na riba au gharama waliyokubaliana na mkopeshaji.
- Fedha hii ni mkopo wa amana na hisa za wateja katika kutoa huduma ya fedha.
- Kwa hiyo mkopo una gharama zake kupitia riba na gharama za uandaaji.
- Mkopo si mali ya benki bali ni mali ya wateja wa benki ambapo benki inasimamia fedha za wateja na kuwa mdhamini kwa wateja wanaoomba mikopo.
- Mkopeshaji anaweza kuwa: Benki, Taasisi za Mikopo au mtu binafsi
- Riba ni gharama inayolipwa unapotumia pesa ya mkopo
SABABU ZA KUCHUKUA MKOPO
Sababu za kuchukua mkopo ni pamoja na:
1. Kuutumia katika uwekezaji
2. Kushughulikia/kutatua mambo ya dharura
3. Kwa ajili ya kugharamia matumizi ya nyumbani
Mkopo kwa ajili ya uwekezaji utaleta faida ambayo mkopaji ataitumia kama rejesho la mkopo
Lakini mkopo wa matukio yasiyotarajiwa na ule wa matumizi ya nyumbani hauwezi kuleta faida, lazima ulipwe kwa chanzo kingine cha mapato
VYANZO VYA MIKOPO
Rafiki, Familia, Taasisi za Mikopo, Benki, Vyama vya Kuweka na Kukopa, k.m SACCOs na VICOBA
MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA KUCHUKUA MKOPO
1. Ratiba ya marejesho ya mkopo ikoje? (kwa wiki au kwa mwezi)
2. Ni kiasi gani nitakua nalipa kama rejesho?
3. Jumla ya marejesho yote ni kiasi gani ikijumuisha na riba?
4. Muda wakupata mkopo. Itanichukua muda gani kupata mkopo?
5. Ni vyanzo gani vya mapato na akiba nitakavyotumia kulipia mkopo?
6. Kama unakopa kwa ajili ya kununua kitu au kifaa: Pindi utakapomaliza mkopo kifaa hicho kitaendelea kutumika kukuletea pesa?
7. Ninahitaji kuweka dhamana ya mkopo? Kama ni ndio, ni ipi?
8. Ni yapi matokeo ya mimi kutolipa mkopo?
MKOPO MZURI NA MKOPO MBAYA
Mkopo mzuri ni mkopo ambao unamsaidia mkopaji kuboresha hali yake ya sasa na kumwezesha kufanya marejesho.
Mkopo mbaya ni mkopo ambao una faida ndogo kulinganisha na gharama, na kupelekea mkopaji kushindwa kulipa.
Maswali Muhimu Kuhusu Mkopo
1. Ni kiasi gani cha fedha zangu mwenye natakiwa kutumia?
2. Nahitaji kiasi gani cha mkopo?
3. Je, mkopo utanisaidia nini ambacho bila kuuchukua nisingekipata?
FAIDA ZA KUKOPA
i. Kupata pesa Zaidi ya zile ulizojiwekea (AKIBA)
ii. Kupata pesa nyingi Zaidi na kwa haraka pale unapopatwa na shida ya ghafla au muda unapokua mdogo katika uwekezaji
iii. Kutatua matatizo yanayojitokeza kwa ghafla
Ni Kipi Kitatokea Endapo Sitalipa Deni Langu?
I. Kutokua na amani muda wote
II. Kupoteza heshima yako
III. Itapelekea kupoteza mali zako, zitauzwa ili kufidia mkopo
IV. Kukosa Imani katika mikopo: hakuna ambaye atakukopesha tena.
Utawala Wa mikopo ni Muhimu sana, usikope kila siku na kila mahali.
Kwa ushauri Wa Masuala Fedha na Mikopo, uandishi Wa proposal ni WhatsApp 0769160382