MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,016
- 16,811
hivi jamani ni kweli tunataka kuwa na wasomi nchi hii au idadi tu ya watu ambao angalau wameenda shule? kuna vijana wawili nimekutana nao na nilipowauliza wakasema wote wapo kidato cha tano na karibuni wanaingia kidato cha sita. hivyo nikataka tu kujua kuwa wanachukua combinations zipi au gani ndipo nikashtuka kidogo kwa majibu yao kwani nilishajua kuwa hata wakienda chuo kikuu hawatakuwa na jipya kutokana na kwamba tangia huku chini hawakuwa na msingi mzuri wa hasa kujua wanataka kusomea nini au kuja kuwa nani hasa kitaaluma hapo baadae.
wa kwanza aliniambia anafanya kombi ya LDP akimaanisha Literature, Divinity na Physics.
wa pili akasema yeye anafanya kombi ya AKI akimaanisha Agriculture, Kiswahili na Islam.
najua humu kuna wasomi mliobobea na wajuzi wa mambo mbalibali yahusuyo elimu hivyo naomba michango yenu je hao vijana wako sahihi kwa hizo combinations zao wanazozifanya na kwamba zina tija au sisi wenye elimu zetu za zamani za kikoloni ndiyo tulipotea maboya?
karibuni tulifanyie uchambuzi hili suala.