Kwa muda nimekuwa nasoma majadiliano yanayohusu umuhimu wa elimu katika maisha ya jamii hasa ya Tanzania. Wengi wamechangia midahalo kama hiyo japokuwa kila kitu kinageuzwa kuwa ni swala la kisiasa. Labda hii inatokana na umasikini wa Tanzania na bara letu kwa jumla. Katika Afrika, na hasa Tanzania ya leo hakuna biashara inayokua na kuamsha mori za watu wengi kama mambo ya siasa. Sibezi umuhimu wa siasa kwa vile najua inagusa maisha ya kila mmoja wetu lakini kuna vitu vingi vinavyogusa maisha yetu na hatuvichngamkii hivyo kwenye majadiliano yetu.
Kwa ujumla wana JF wengi naona wanabeza sana maswala ya elimu kiasi kwamba wanaotetea maswala ya umuhimu wa elimu wanakuwa ni wachache mno. Wachangiaji wengi wanasema hapa Bongo swala la elimu siyo muhimu sana kwani hawaoni matunda ya watu waliosoma. Unaweza kufanya mambo mengi kutokana na uzoefu tu.
Swala la kubeza elimu limefika mpaka ngazi za viongozi wetu. Shule zinajengwa bila kupewa vifaa muhimu. Vyuo vyetu vikuu havina makatba za maana. Ukienda UDSM utaona Bookshop yao inauza vitabu vya Kindergarten! Hakuna vitabu vya chuo kikuu. Shangingi chache tu zingeweza kununua vitabu vya maktaba za vyuo au kuweka vitabu kwenye Booksho za vyuo. Kelele zimepigwa kuhusu watu wanojinadi kuwa wanadigrii za falsafa (PhD) lakini kumbe wamenunua. Wengine ni wabunge na hata mawaziri ambao wameendelea kuteuliwa. Hapa tungeweza kusema mengi sana jinsi ambavyo viongozi wan chi yetu wasivyothamini umuhimu wa elimu kwa nchi yetu.
Kutothamini elimu kumeathiri maendeleo ya nchi yetu kwa kiasi kikubwa sana. Hapa sizungumzii elimu ya ufundi peke yake. Kuna elimu kwenye biashara, ustawi wa jamii, utalii, mahoteli, ethics, michezo, n.k. Kwa mfano, sishangai kwa nini Tanzania haifanyi vizuri kwenye michezo kuliko nchi nyingine. Sishangai kwa nini watumishi wengi katika mahoteli yetu ni watu wa kutoka Kenya, siyo kiingereza tu bali hata ya kupanga visu na uma mezani! Sishangai kwa nini wafanya biashara wengi, wananchi na wageni wanaajiri zaidi watu wa nje kwenye sehmu nyeti za biashara zao. Hata mimi ningefanya hivyo kwani Mtanzania ukimpa kazi leo usiku mzima atakuwa anaota jinsi ya kukuibia!
Kuna wachangiaji kadhaa wamedai kuwa elimu siyo muhimi sana kwani wagunduzi wengi walikuwa hawana elimu kubwa lakini waliweza kugundua mambo muhimu kwa manufaa ya binadamu. Hao ni wengi kiasi gani kwa kweli sijui. Jee dunia inategemea wagunduzi wangapi wa siku zijazo watakuwa hawana elimu? Katika dunia ya leo, bado tunategemea kupata wagunduzi wasio na elimu?