SoC03 Elimu na wasaidizi wa kazi, puuzo lenye kuogofya katika ustawi wa familia

Stories of Change - 2023 Competition

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
30
29
Maisha ya uchakarikaji na utafutaji kuleta mkate wa kila siku katika familia ni hitaji lisilo na ukomo katika maisha ya mwanadamu.

Hali hii imesababisha mgawanyo wa majukumu katika malezi na usimamizi katika familia nyingi mijini na vijijini. Kufuatia hali hii hitaji la mtu aitwae msaidizi wa kazi limekuwa ndilo kimbilio la wengi.

Msaidizi wa kazi amekuwa ndie kimbilio la kwanza kwa wanafamilia wengi. Wimbi la kuajiri ma 'ngumbaru' na 'wajinga' ndio limekuwa zoea baya la wengi kwa kigezo kuwa hili ni kundi la watu wa ujira wa chini. Je, msomaji unajua cha nafuu ni gharama? Ndugu msomaji hebu kaa ujiulize maswali haya;

- Fikiria juu ya hatari ya kuajiri msaidizi wa kazi asiye na ufahamu wa kutosha katika mradi wako.

- Nyumba yenye samani sheheni za mamilioni unazomkabizi binti asiye na ufahamu aituze na kuihudumia, likitoke la kutokea utamlaumu nani?

- Binti/kijana wa kazi toka kijijini kule ambako kuona jiko la umeme au gesi ni hadi aende banda la video kuangalia tamthilia, leo umemkabizi jiko nawe umeenda kuzurula mjini! Usalama upo?

Je, 'mjinga' huyu uliemuajiri, anazijua haki zote za mtoto na malezi bora? Ukatili kwa watoto wajua wewe muajiri unaweza kuwa ni chanzo chake?

Mifugo yako shambani itahudumiwa ipasasyo kwa kuajiri mtu asiye na ufahamu?

Haya ni baadhi tu ya maswali ya kawaida sana na muda mwingi hupuuzwa lakini yana umaana mkubwa sana katika ustawi wa familia.

Msaidizi wa kazi za ndani na mashambani hana budi kupewa elimu ya msingi ili atambue baadhi ya mambo kabla ya ajira.

Baadhi ya athari zinazoweza kuepukwa kwa kutoa elimu kwa kundi hili ni kama zifuatazo:

- Kupunguza ukatili na utoaji wa malezi bora kwa watoto (msaidizi wa kazi ndie anaeshinda na watoto kwa muda mwingi).

- Kuepuka ajali na athari za ajali majumbani mfano moto.

- Kuepuka utapeli, wengi wa wasaidizi wa kazi hutolewa vijijini hivyo uhuni na utapeli wa mjini uliopo hawaujui kuepukana na hilo, elimu kwao ni muhimu.

- Athari zingine ndogo ndogo zaweza epukwa mashambani na majumbani.

Hitimisho
Wanajamii tusiogope kutoa elimu ya awali kwa wasaidizi wa kazi kwani kuna manufaa mengi kuliko hasara. Kwa elimu hizi za awali kundi hili la wasaidizi wa kazi litajua wajibu wao, haki zao na stahiki zao hivyo kazi kufanyika kwa ufanisi.

Kundi hili la wasaidizi wa ndani linaweza kupewa thamani kwa kufanya yafuatayo;

- Utoaji wa elimu ya awali yenye kujikikita katika;

- Haki za watoto na malezi bora kwa watoto.

- Elimu ya ujasiliamali na kazi za kawaida za majumbani na mashambani.

- Elimu ya jinsi ya kutumia vyombo vya moto na umeme.

- Elimu ya tahadhari na huduma za kwanza.

NB: Elimu inayoendana na kulingana na mazingira ya kazi ni muhimu, kama ni kilimo elimu iwe kwenye kilimo, uchimbaji madini elimu ya madini, malezi - elimu ya malezi nakadhalika.

Shime kwa jamii na serikali kuja na mfumo saidizi kwa kundi hili, ili kulipa thamani zaidi kuliko hali ilivyo sasa.
 
Dawa ni moja TU.

Iwe ajira rasmi mihahara mzuri uone kama hao watoto watapata kazi hizo.


Nchi za wenzetu kazi hizo ni deal. Waajiri walipe mishahara Ili hata graduate waombe Kaz za manu.bann.

Zaid ya Hilo owekazi ya kutwa tu sio full daiys and night.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom