Elimu na Shule

Nimeipenda hii mkuu vijana wazidi kuelimishwa ili waweze kuzikabili changamoto zinazowapata kwa kutumia elimu waliyoipata badala ya kusubiri vyeti vyao walivyovipata shule kutatua changamoto hzo
 
Hukuwa upande wa dini na mungu kwa "sababu ulizokuwa nazo"

Wewe ni mkinga wa iringa?

Ila asante sana kwa mada nzuri
 
mwaka 2002 nilimaliza elimu yangu ya secondary tulihitimu.wanafunzi 97.tuliofaulu tulikuwa 14 wengine wote hawakuwa na vigezo vya kusonga mbele. wakabaki kijijini kutafuta maisha. je hawa watu wangefundisha maarifa ya.kutafutapesa miaka yote 11 si wangekuwa matajiri?
 
elimu ya shule inatumika sana huwez ukawa unaona calculus lakini kwenye simu yako Na computer hvyo vyote vipo.Cha msingi nikujua jinsi ya kutumia maarifa uliyonayo kutatua matatizo.Lakini pia kumbuka CO kla maarifa yanahusiana Na kutatua matatizo Kuna vitu vengine ni abstract kama pure mathematics(cyo hyo ya alevel yaki magumashi) unakutana Na reimaann manifolds Na number theory ingawa inatumika ahata Na website ya jf forums lakini ni pure
 
"elimu bila malengo au kusudi ni kifungo cha fikra"

Nimependa huo msemo,kuna watu elimu huwa zinawanyima Uhuru wa kufikiri kwa kushindwa kufikiri nje ya box na kuwa wapo kwenye kifungo cha fikra.
 
Kuna umuhimu wa kubadilisha mfumo wetu wa elimu kwa maana hautusaidii kitu zaidi ya kujazana ujinga tu
 
Naamini hukuelewa somo ''Elimu ni Ufunguo wa Maisha'' ukisha upata tu huo ufunguo kitasa tafuta mwenyewe! usitafuniwe kila kitu utakuwa zuzu!!!

Elimu yako hiyo ya sayansi ya Fedha ni kubwa mno! ni zaidi ya msaada, kwanza kujua tu nina hiyo Elimu nanenepa tu! no stress! utaitumia vyema kwenye mauzo ya biashara yako ya vitunguu swaumu unavouza! utaonyesha tofauti kubwa hapo kwa kuchezesha hela kuliko mtu ambaye hajaenda shule! tena ni rahisi kutafuta masoko ya nje sababu unajua kucheza na fedha, na Lugha ya kuongea na wenye hela!

UKisha pata mtaji kwa kuwa unajua kucheza na hela unaweza ukawa agent wa wakulima maeneo hayo! je hujaajiliwa na wakulima bila wao kujijua? kushuka na kupanda kwa dola km kweli umesoma ni km unanusa! unaweza fanya chochote ktk ulimwengu wa fedha sababu umeshauza vitunguu una hela! km ni kulima utalima kisasa kwa sababu una uwezo na elimu ya kujua chochote ktk kilimo kirahisi.

Rafiki yako , Dentist huyo aliye ajiliwa hapo km Meneja wa Hospital anaweza uza hiyo huduma yake , akaishi, akatoa ushauri kwa wagonjwa wa meno hata nyumbani kwake tu, au akafungua Clinic ya meno ambapo atafanya kazi ya ziada hapo kwake, baada ya kazi, je? haja pata kipato cha ziada? akipanuka zaidi anaweza tema mzigo.

Tena mko vizuri mmejipanga wewe mpe akili ya financial management, na yeye atalinda afya ya kinywa na meno ya familia yako, ili usiugue ugue si unajua Afya ni mtaji?

Nashangaa elimu nzuurii hii unalia lia tu, Biashara Matangazo wakikujua wewe ni mtu wa fedha watakuita kufanya Auditing kwa wenye Biashara kubwa, hata kijiji kikubwa smartness na uaminifu tu baasi. utakuta mwaka mzima uko busy vitunguu utasahau!

Kuna Daktari kijana alikuwa mwenyekiti wa kijiji kabisaa!! sababu kijijini yeye ndo Boss akachagua sehemu yenye Rutuba akanunua akalima shamba la mahindi mpaka kuvuna, hela alioipata akanunua vifaa na kujenga Hospital ndo ikawa Biashara mpaka leo! anakazi mbili.
 
Umeongea vizuri sana, lakini mtoa mada hakumaanisha watu wasisome, bali jamii iangalie mahitaji ya elimu kulingana na mazingira, mifumo yetu ya elimu ipitiwe upya na mingine ibadilishwe kwenda sambamba na mahitaji ya jamii. Chukulia kwa mfano mtu anataka kuwa Mtabibu (Dr) lakini anasoma na kukaririshwa masomo ambayo hayatamsaidia katika fani yake kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…