Lyetu
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 1,333
- 3,541
Habari za weekend wapendwa katika bwana.
Naomba nianze na historia yangu kiufupi ili uweze kunisaidia ushauri.
Nina umli wa takribani miaka 24 kwa sasa. Miaka kadhaa iliyopita nilipohitimu darasa la saba na kupata ufaulu mzuri tu ila sikubahatika kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na ugumu wa maisha uliokuwa unaikabiri familia.
Baada ya hapo nikajikita kwenye ujenzi kama msaidizi wa mafundi kisha nikajihusisha na ununuzi na usafirishaji wa nafaka na hapa nilikuwa kama msimamizi kuhakikisha ujazo na ubora unakuwa kwa kiwango kinachohitajika na nililipwa 100,000 Hadi 150,000 kwa mwezi ilikuwa 2013.
Mnamo mwaka 2014 niliugua Sana kiasi cha kwenda kijijini kwetu kupata msaada na hapo ndipo Mungu akanikutanisha na mzungu ambae alikuja kututembelea pale nyumbani baada ya mzee wangu kununua solar kwenye kampuni yake na ndiye alikuwa mteja wa kwanza. Yule mzungu alikuwa anajihusisha na uuzaji wa mifumo ya mwanga kwa matumizi ya nyumbani inayotumia nishati ya jua.
Mzungu yule alinipenda kwa sababu niliweza kijieleza vizuri pia nilikuwa mwepesi wa kujifunza vitu kwa haraka na hii ilichangiwa na kujumuika na watu mbalimbali wenye rika na elimu tofauti tofauti. Basi akanipa fursa ya kujiunga na kampuni yake Bila hata kufanyiwa interview.
Niliingia kama afisa mauzo na badae kuhamishiwa idara ya Hardware upande wa Field Service Technician pia hii ilichangiwa na uwezo wa kujifunza na kuelewa vitu kwa haraka. Nikaona nisikae kizembe nikajiunga na masomo ya Basic Computer.
Huko pia nikaweka juhudi na Kuna muda nilikuwa najoin kidogo kwa walioko ngazi za juu kama vile IT ngazi ya cheti, nikajikuta nimepata knowledge kidogo Sana huko upande wa IT. Huku kwenye basic juhudi zilikuwa kubwa kiasi kwamba ikafikia hatua mwalimu wangu akawa ananipa darasa nifundishe. Basi nikawa nafanya kazi pia nafundisha.
Tukirudi huku kazini yale maujanja kiasi ya computer, typing skills pamoja na uwezo mkubwa kidogo wa excel basi nikawa mtu muhimu Sana na baadhi ya wafanyakazi wenzangu walinifata mala kwa mala ili nitoe msaada kwao pale wanapokutana na changamoto kwenye computer.
Hapo kazini nimebahatika kuwa karibu na IT department na nimeshakula matunda kiasi fulani kwenye project zao binafsi pale wanapokuwa wamebanana basi wananielekeza ni kipi nikafanye na najipatia chochote.
Watu wanaonizunguka wamekuwa wakinishauri nisome IT na kwa upande wangu ni kitu nachokipenda.
Malengo,
Kwa mwaka 2021 nimeplan nisome QT ili niweze kufika huko napohitaji kufika.
Changamoto,
Kwa mujibu wa maelezo niliyopata nikuwa ili nifike huko ni lazima nisome masomo ya sayansi ( ambayo naambiwa ni ngumu japo sina uhakika)
Changamoto niliyonayo nitawezaje kumudu haya masomo na kufanya kazi ukizingatia ni masomo ya miaka miwili pekeake?
Nitawezaje kuyamudu haya masomo nayosikia ni magumu na yanahitaji muda wa kutosha akati mimi muda wangu ni mchache?
Wakuu naombeni ushauri wenu kazi naihitaji elimu pia naihitaji nitawezaje kufanikisha vyote viwili Bila ya kuzorotesha upande mmoja.
Asanteni.