Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu, mtakumbuka wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka jana 2015 moja ya mambo tulioahidiwa ni kuwa CCM na CHADEMA (UKAWA) watatoa elimu bure kuanzia shule ya chekechea mpaka aidha sekondali na mwingine chuo kikuu.
Sasa CCM imeshinda na mheshimiwa Rais Magufuli kaahidi kutoa elimu bure tena kwa kusisitiza, kinachonishangaza ni hii kampeni ya kuchangia madawati inayoendelea sehemu mbalimbali nchini tena kwa kila familia.
Maswali ninayojiuliza ni:-
1. Michango hii ndio iliyolalamikiwa na mheshimiwa Rais hivo kuitoa kwa wazazi husika, sasa mbona wanaingizwa na wazazi ambao hawana watoto katika shule hizo?
2. Agizo la mheshimiwa Rais la kuwa na utamaduni wa kupewa risiti katika suala hili risiti inatolewa?
3. Kwa kuwa skuli nyingi za serikali zina upungufu wa vifaa (si madawati pekee), hakuta kuwa na michango mingine?
Wakuu, maswali ni mengi hivo nashawishika kufikiri elimu bure ni dhana tu.