Elimu bure inawezekana; si muujiza.!

Elimu bure inawezekana; si muujiza.!

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Leo ngoja niwasaidie jamaa zangu wa CCM ambao wengi wao hawajui Hesabu. Tangu Mgombea Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa atangaze Elimu bure, kuna watu wamekuwa wakiona huo kama muujiza.

Kwa kifupi zipo njia nyingi sana zinazoweza kufanya Elimu kuwa bure kuanzia Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Leo ngoja niongelee 'alternative' moja.

Kwa mujibu wa TAMISEMI Tanzania ina jumla ya shule za msingi 16,343 zenye wanafunzi 8.3 mil. Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka kutoka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka huu.

Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 54 kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, wanafunzi wa shule za msingi wanakadiriwa kugharamia kiasi cha Sh.10,000/= hadi 15,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi Tanzania wanahitaji Bilioni 80 waweze kusoma BURE.

Shule za Sekondari za Serikali zinakadiriwa kuwa 2,446 zikiwa na jumla ya wanafunzi 1,004,071. Kati yao wanafunzi 185,652 ni wa Shule za Kulala (Boarding), na wanafunzi 818,419 ni wa shule za kutwa (Day).

Wanafunzi wa Shule za kutwa wanalipa ada TZS 20,000 kwa mwaka. So ukichukua 20,000 × 818,000 utapata Bilioni 16.3. Wanafunzi wa shule za Bweni wanalipa ada TZS 70,000/= kwa mwaka. So ukichukua 70,000 × 185,652 utapata Bilioni 11.2.

Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu wa vyuo vya Serikal na vya binafsi wapo 200,986. Kati yao wanafunzi 162,987 wanasoma Course za 'Social Science, Law, Humanities, Education etc' ambao ada zao hazizidi Mil.2 kwa mwaka. So chukua 162,989 × 2000,000/= utapata Bilioni 325.

Wanafunzi 37,997 wanasoma course za "Science" kama Engineering, Udaktari etc na ada zao ni zaidi ya Mil.3 kwa mwaka. So hawa watahitaji Bil 113.5 kulipa ada ya mwaka mzima.

Fedha ya kujikimu pamoja na chakula (Meals & Accomodation) inayotolewa kwa sasa ni TZS 7,000 kwa siku kwa mwanafunzi mmoja. Hivyo basi mwanafunzi mmoja anapata Jumla ya Shilingi 1,680,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu ambao ni 200,986 wanahitaji Bil 337.

Fedha ya Utafiti (Research), Mafunzo kwa njia ya vitendo (Field) na vitabu (Stationeries) hutolewa jumla ya Shilingi 735,000/= kwa mwaka ambayo hugawanywa kulingana na asilimia ya mkopo ya mwanafunzi. Hivyo basi wanafunzi wote wanahitaji Bil 147 kwa mwaka.

Ukijumlisha gharama zote hapo juu utapata jumla ya Shilingi Bilioni 934 tu. Kwa lugha rahisi ni kuwa ili kila mwanafunzi nchini asome bure kuanzia Elimu ya msingi, sekondari na akifika Chuo Kikuu alipiwe gharama zote bure kwa asilimia 100%, serikali inahitaji kutoa Shilingi Bilioni 934 tu kila mwaka.

Swali, Je hizi Bilioni 934 zinapatikanaje?

Ukisoma hotuba ya Bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2014 utagundua kuwa Mlima Kilimanjaro peke yake unachangia karibu Bil.800 kwenye pato la Taifa (Gross National Income of $350 Milion).

Kwa lugha Rahisi ni kuwa tunahitaji Mlima Kilimanjaro mmoja tu ili watoto wetu wasome bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Yani tukiamua mapato yote ya Mlima Kilimanjaro tuyapeleke kwenye sekta ya Elimu bila kuchakachua, tutakua na uhakika wa kusoma bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu. Je hatuwezi??

Hapo hatujagusa Mbuga za wanyama, hatujagusa Bandari, Madini, Gesi, Mazao ya misitu, Uvuvi, Kilimo, Viwanda, etc. Tumegusa mlima Kilimanjaro peke yake. Kama CCM wanaona hawawezi wakae pembeni wanaoweza wafanye.!
 
hivi kuna watu bado wanaamini maneno ya Lowasa.!!!! Mlaghai anajaribu kuwadanganya wa Tanzania kwamba ataleta mabadiliko, wakati alikuwa madarakani kazi kupiga ma deal tu, leo hii anaongea tu maneno, shame on you Lowasa hatukupi kura zetu.
 
Lowasa alichosema alijua kinawezekana bila tatizo ccm wanasema haiwezekani kwasababu ya ufisadi wao.watanzania tumejaliwa utajiri mkubwa hatutakiwi kuwa masikin tumpe nafasi lowasa atutoe matongotongo tuone tulivyokua tunaibiwa kwa miaka mingi.tumewapa ccm miaka mingi hatujaona kitu tunawapa ukawa miaka mitano hii tuanze kuona tofauti.naaamin ukawa ikiingia hakuna mtanzania atakayekuja kuitaman ccm hata kwa rushwa zao
 
hivi **** watu bado wanaamini maneno ya Lowasa.!!!! Mlaghai anajaribu kuwadanganya wa Tanzania kwamba ataleta mabadiliko, wakati alikuwa madarakani kazi kupiga ma deal tu, leo hii anaongea tu maneno, shame on you Lowasa hatukupi kura zetu.

hivi wewe kazin kwako unaweza kubadilisha nini bila boss wako?
 
Umewasaidia sana mpe kura kura. Muone mziki wake utapenda mwenyewe
 
Mkuu,
Ungeiacha vile vile ikiwa kwa aya (paragraph) kama ilivyokua awali, pili "acknowledgement" muhimu kaka kuonyesha kuthamini kazi za wengine
 
Ninauhakika wewe utakuwa mwanabavicha.Sumaye miaka kumi kama waziri mkuu......Jizi Lowass miaka saba wizara mbili tofauti...miaka miwili waziri mkuuu....walishindwa nini kuyafanya haya wakiwa serkalini waje kuyafanya kwa pesa za ruzuku za vyama?.....Chama kimepokea matapeli

watanzania sisi ni watu wepesi sana kichwani na wewe ni mfano mzuri sana, mtoa hoja ametumia namba kujenga hoja wewe unatumia maneno matupu kupinga hoja. watanzania tufikie mahala tujifunze kufanya reseach na ku analyze fact ndio tutaweza kufika just because kiongozi fulani kasema haiwezekani that is not a FACT do your own research to collect fact and analyze it critically on your own hizi shule za kata shida sana
 
80+16.3+11.2+325+113.5+337+147=1030billion nadhani hiyo figure 934 inamapungufu kidogo pili namake assumption ulivyosema secondary ulichukulia o level na advance level kwa pamoja karibia figure zako zote zinamatatizo kila mtu anakubali serekali yetu inauwezo wa kusomesha bure kuanzia chekechea mpaka secondary i mean form six kwa suala la mpaka chuo ni ngumu tena haiwezekani tukiweza nadhani itakuwa nchi ya kwanza Africa hata South Africa wameshindwa ili tuweza kutoa elimu bure kote sehemu nyingi zitaathirika kupita maelezo ningependa pia nikusahihishe figure zako za chuo hazina maana kuna watu wa ngazi ya diploma umewaignore completely pia urefu course unatafutiana madaktari wanakaa mpaka miaka 7 kumaliza first degree awe daktari mahesabu yote uliyoyatoa ngazi ya elimu ya juu hayana maana gharama zake ni kubwa kuliko ulivyozikadiria kitu kingine ambacho umekisahau ni wanafunzi wa wanaosama vyuo na shule binafsi ambao hatakubali kuona wenzao wanasoma bure wao walipie tuache ubishani usiokuwa na maana U.S na UK elimu bure vyuoni imewashinda sembuse sisi hichi kitu cha elimu bure chuoni ni IMPOSSIBLE
 
Kidibwe na we una matatizo kidg kwaiyo akishindwa mzungu basi akiwezekani apa africa si ndio je na libya je au utasema wale ni waarabu mana muarabu dubai riba dhambi na wanafanikiwa kwa mafuta lakini nigeria wameshindwa ebu tubadilike ki mawazo nina imani watanzania wote elimu tuliyonayo inatosha sema ubinafsi tu kama we umefanikiwa na familia yako basi utaki mwingine apate uko tayari mtanzania afe na umasikini ata kama unacho pigania umuinue ata yule asiyenacho
 
Hela za kulipa malimbikizi ya walimu, wakandarasi na miradi mingi ya maendeleo imesimama ; tunaongeza na hizo bilion 934 za kusomesha bure !!! Wachumi wachambuzi waje kutupa utaalam wao juu ya hili.
 
hivi **** watu bado wanaamini maneno ya Lowasa.!!!! Mlaghai anajaribu kuwadanganya wa Tanzania kwamba ataleta mabadiliko, wakati alikuwa madarakani kazi kupiga ma deal tu, leo hii anaongea tu maneno, shame on you Lowasa hatukupi kura zetu.

Sema haumpi na sio hatumpi kura! Mbona mimi nitampa kura yangu Lowassa!
Ishu ya Wanafunzi kusoma bure mbona ni simple tu! Hata mie naweza isimamia kwa kutumia rasilimali moja tu ya madini ya Ulanga na wakasoma.....hapo sijagusia tanzanite, Almasi, I dhahabu, uranium, gas, nk
 
Kidibwe na we una matatizo kidg kwaiyo akishindwa mzungu basi akiwezekani apa africa si ndio je na libya je au utasema wale ni waarabu mana muarabu dubai riba dhambi na wanafanikiwa kwa mafuta lakini nigeria wameshindwa ebu tubadilike ki mawazo nina imani watanzania wote elimu tuliyonayo inatosha sema ubinafsi tu kama we umefanikiwa na familia yako basi utaki mwingine apate uko tayari mtanzania afe na umasikini ata kama unacho pigania umuinue ata yule asiyenacho

Nigeria population 173.6million Libya population 6.202million Nigeria Gdp 3,006.51 Libya11,964.73 nadhani umeona tofauti iliyopo kati ya Nigeria na Libya plus ubora wa mafuta unazalishwa Libya ni tofauti na wanageria thus why Gadafi alikuwa anauwezo wa kusomesha bure na ukimaliza form six alikuwa anakuuliza utasoma vyuo vya ndani au vya nje ukitaka kuoa ulikuwa unapewa mpaka pesa ya kuanzia maisha Libya ilikuwa nchi pekee Afrika yenye sehemu nzuri ya kutunzia nyumba za wazee kwetu sisi hatujafika huko pesa nyingi tunatumia kulipa madeni hewa thus why deni la taifa linaongezeka kila siku kwa riba,kuanguka kwa uchumi wetu wa ujamaa,upuuzi wa kujiingiza kwenye vita vya Uganda pamoja na mafisadi kama CCM yenyewe na akina Lowassa ndio waliotufikisha hapa tulipo sasa hivi elimu bure mpaka chuo kwa Tanzania ni ngumu itatucost karibia nusu ya budget yetu ya sasa sector zingine kama afya,Miundombinu na ulipaji wa deni itakuwa ngumu kumbuka sehemu kubwa ya budget yetu ni mkopo kutoka kwa wahisani ambao wao pia wameshindwa kuprovide free education kwenye nchi zao
 
Leo ngoja niwasaidie jamaa zangu wa CCM ambao wengi wao hawajui Hesabu. Tangu Mgombea Urais wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa atangaze Elimu bure, kuna watu wamekuwa wakiona huo kama muujiza.
Kwa kifupi zipo njia nyingi sana zinazoweza kufanya Elimu kuwa bure kuanzia Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Leo ngoja niongelee alternative moja.
Kwa mijibu wa TAMISEMI Tanzania ina jumla ya shule za msingi 16,343 zenye wanafunzi 8.3 mil. Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka kutoka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka huu.
Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 54 kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, wanafunzi wa shule za msingi wanakadiriwa kugharamia kiasi cha Sh.10,000/= hadi 15,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi Tanzania wanahitaji Bilioni 80 waweze kusoma BURE.
Shule za Sekondari za Serikali zinakadiriwa kuwa 2,446 zikiwa na jumla ya wanafunzi 1,004,071. Kati yao wanafunzi 185,652 ni wa Shule za Kulala (Boarding), na wanafunzi 818,419 ni wa shule za kutwa (Day).
Wanafunzi wa Shule za kutwa wanalipa ada TZS 20,000 kwa mwaka. So ukichukua 20,000 × 818,000 utapata Bilioni 16.3. Wanafunzi wa shule za Bweni wanalipa ada TZS 70,000/= kwa mwaka. So ukichukua 70,000 × 185,652 utapata Bilioni 11.2.
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu wa vyuo vya Serikal na vya binafsi wapo 200,986. Kati yao wanafunzi 162,987 wanasoma Course za 'Social Science, Law, Humanities, Education etc' ambao ada zao hazizidi Mil.2 kwa mwaka. So chukua 162,989 × 2000,000/= utapata Bilioni 325.
Wanafunzi 37,997 wanasoma course za "Science" kama Engineering, Udaktari etc na ada zao ni zaidi ya Mil.3 kwa mwaka. So hawa watahitaji Bil 113.5 kulipa ada ya mwaka mzima.
Fedha ya kujikimu pamoja na chakula (Meals & Accomodation) inayotolewa kwa sasa ni TZS 7,000 kwa siku kwa mwanafunzi mmoja. Hivyo basi mwanafunzi mmoja anapata Jumla ya Shilingi 1,680,000/= kwa mwaka. Hii ina maana kuwa wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu ambao ni 200,986 wanahitaji Bil 337.
Fedha ya Utafiti (Research), Mafunzo kwa njia ya vitendo (Field) na vitabu (Stationeries) hutolewa jumla ya Shilingi 735,000/= kwa mwaka ambayo hugawanywa kulingana na asilimia ya mkopo ya mwanafunzi. Hivyo basi wanafunzi wote wanahitaji Bil 147 kwa mwaka.
Ukijumlisha gharama zote hapo juu utapata jumla ya Shilingi Bilioni 934 tu. Kwa lugha rahisi ni kuwa ili kila mwanafunzi nchini asome bure kuanzia Elimu ya msingi, sekondari na akifika Chuo Kikuu alipiwe gharama zote bure kwa asilimia 100%, serikali inahitaji kutoa Shilingi Bilioni 934 tu kila mwaka.
Swali, Je hizi Bilioni 934 zinapatikanaje?
Ukisoma hotuba ya Bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2014 utagundua kuwa Mlima Kilimanjaro peke yake unachangia karibu Bil.800 kwenye pato la Taifa (Gross National Income of $350 Milion).
Kwa lugha Rahisi ni kuwa tunahitaji Mlima Kilimanjaro mmoja tu ili watoto wetu wasome bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Yani tukiamua mapato yote ya Mlima Kilimanjaro tuyapeleke kwenye sekta ya Elimu bila kuchakachua, tutakua na uhakika wa kusoma bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo kikuu. Je hatuwezi??
Hapo hatujagusa Mbuga za wanyama, hatujagusa Bandari, Madini, Gesi, Mazao ya misitu, Uvuvi, Kilimo, Viwanda, etc. Tumegusa mlima Kilimanjaro peke yake. Kama CCM wanaona hawawezi wakae pembeni tunaoweza tufanye.!

Kwan hawaelew hilo...wanaelewa sana na inawauma kuona kwanin hao wakuu ccm wasitekeleze hilo...kama magufuli anakwambia elimu ya bure mpaka form four manake ni nin...
kwanza maana yake ni kwamba hapo awali hakukuwa na bure form 4 so wanaiweka sasa ili angalau kujaribu kurudisha kura zilizoporomoka tangu aingie J.K...kwahili siwapongezi kwa kuwa wamekosa mbinu mathubuti za kuwateka wananchi...kwa mfano ukilinganisha sera hyo hyo ya elimu kwa pande zote mbili zinazogbea utaona kuwa lowassa amewashika vibaya mno...
Maana ya pili ni kwamba kwanini wasingeweka elimu bure mpaka vhuo kikuu...ahaa t's just simple, ni hivi ccm wanafanya kazi ndani ya system na si nje, kwahyo kukomea elimu bure mwsho form 4 maana yake ni kuwa wanajitahidi kutokupunguza mianya ya wao kupiga deal na kula pesa kilaini...ni simple tu yan ni kama vile ulivofafanua hapo kuwa mlima kilimanjaro tu pekeake waweza kusomesha bure mpaka chuo, tukichukulia kwa hesabu hizohizo kwa wao na bure yao mwsho form 4 maana yake hapo wanajikatia hyo iliyobak ya form6 na chuo wanakula wao....
Yan hiv vitu ni simple sana sema tu tunatofautiana kifikra katika kuchambua na kuelewa maana yake nini...
Nmekuja gundua kuwa elimu kama hizi zinahitajikasana kwa wale ambao bado wameegemea ccm ili kuwafumbua macho na kufanya maamuz ya busara.

Ni hayo machache tu wakuu
 
Asante kwa uchambuzi mzuri. Ukiweka mbali mlima kilimanjaro mapato yanaweza kupatikana kwa uthibiti tu wa matumizi mabaya na fedha inayopotea kwa ufisadi usisahau kina iptl. Inawezekana elimu bure mpaka chuo kikuu isiwezekane mwanzoni mwa uongozi wa lowasa lakini kwa dhamira yake anaweza akafanya elimu bure mpaka form six na nusu ya elimu ya chuo kikuu ikagharamiwa na serekali ingali nusu ingine mwanafunzi atalipa kwa kupewa mkopo wenye uhakika. Hakika hilo linawezekana.
 
Back
Top Bottom