Elimu bure inaanza lini?

vampire_hunter007

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
1,034
2,599
Habari wakuu,

Mi mgeni humu naomba kuuliza swali.....

Miongoni mwa vitu alivyovisisitiza kwenye kampeni zake Mh. Magu ni elimu bure mpaka kidato cha nne...Wengi walifurahia hili haswa alipotangaza kuwa utekelezaji unaanza this January....

Pia watu walishangilia baada ya mapato ya serikali kuongezeka na kutangazwa kiasi cha pesa kupelekwa mashuleni kwa ajili ya mpango wa elimu bure. Kuanzia January mwaka huu hakuna ada yoyote itakayotozwa.

Sasa juzi nilikwenda kutembea mitaa ya bagamoyo. Nilikwenda katika shule moja kufuatilia masuala yangu binafsi. Cha ajabu nikakuta almost zaidi ya robo tatu ya wanafunzi hawapo shuleni na baada ya kuuliza marafiki zangu walimu wa pale nikaambiwa wamerusishwa nyumbani kisa hawajalipa ada. Na wazazi wao wamegoma kutoa ada kwa sababu wameambiwa na Rais kuwa elimu ni bure..

Nilipohoji kwa nini walipe ada na elimu ni bure, nikaambiwa shule haijapokea maelezo rasmi ya kusitisha kutoza ada. Na wakisema wasitoze ada watoto watakaa na njaa maana ni shule ya boarding na hawajapewa pesa ya chakula.


Hii ilikuwa last week.

Swali langu ni je, hii elimu bure inaanza lini? Au zilikuwa ni "kampeni" tu za siku zote?

NB.
Sijataja jina la shule kwa sababu maalum na nitaitaja pale itakapobidi
 
Yaan leo ndo natoka kulipa hela za mchango wa chakula kwaajili ya mwanangu kimbwe......
 
hakuna elim bure jaman,rais alinukuliwa vibaya ....na gazeti la mawio ndo maana likafungwa.....
 
Back
Top Bottom