Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,015
- 2,191
Habari wakuu,
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Twaweza juu ya Maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko kwenye sekta ya elimu umeonyesha kuwa tangu sera ya Elimu Bure ianze kufanya kazi, bado asilimia 90% ya wazazi/walezi huchangia elimu katika shule za umma.
Pia, utafiti huo unaonyesha kuwa wananchi zaidi ya 70% wanaamini juu ya ubora wa elimu itakayotolewa endapo changamoto zilizopo kama za mishahara ya walimu, mazingira na vifaa vya kufundishia zikifanyiwa kazi.
Hizo ni data za kitafiti. Je, zinatoa mwanga mpya? Tuko kwenye hali gani na ni kweli hii itachangia kuinua elimu inavyostahili?
Hebu wadau tujadili..