Elimu Biashara; Mkopo v/s Saving

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,156
Nimeichukua mahali, Inaweza kukusaidia,

Ushawahi kuwaza kwanini kuna watu maisha yetu daily yanakua yanasukumwa na Mikopo? Ni kwa sababu tunakopa kununua vitu ambavyo baada ya muda wa mkopo na vyenyewe vinakua vimeisha au vimekaribia kuisha thamani. Mfano mzuri ni mkopo wa gari.

Kuna watu tupo radhi kukatwa 248,500/= kwa mwezi kwa muda wa miaka mitano kwa riba ya 18% kwa ajili ya kulipia mkopo wa 10m tuliotumia kununua vits lakini hatupo tayari Kufanya saving ya walau 220,000/= kwa mwezi kwa muda wa miaka mitano ili tuje nunua gari kwa cash yetu.

Sisemi tusinunue hapana maana kila mtu ana mahitaji yake na malengo yake.
Hata kama baada ya miaka 5 gharama ya gari itakua imepanda, bado kwa 220,000/= utakua umeweza kuhifadhi 13.2m ambayo inatosha kabisa kununua gari kwa kipindi hicho, au unaweza ukakuta bei zimeshuka kama sasa.

Najua wengi tutakimbilia kwenye Time Value for money, ila ukweli ni kwamba wengi wetu hatujipangi ni nini tunataka katika muda fulani bali tunakurupuka kutokana na hitaji la mhemuko la mda huo.

Mtu anaamka tu anasema kachoka shida ya usafiri na joto anataka push miguu minne, akichungulia kwenye akaunt salio halitoshi anajaza form chaap anachukua mkopo ili aanze pishana na wenzake sheli. Achana na hizi gharama za mafuta, service na parking tutaziongelea siku ingine.

Wakati unafanya saving ya miaka mitano ili ununue gari unaweza amua kuwekeza hela zako hata kwenye UTT - Vipande ambavyo kila siku vinapanda thamani na baada ya miaka mitano ukajikuta una hela nzuri tu. Miaka mitano ya kumaliza kulipa mkopo unakuta na Vits yenyewe imeshachoka, unajikuta na mshahara kidogo umepanda na unahitaji gari jingine, unajitwika mkopo Mwingine mkubwa kidogo, unaagiza gari ya juu na maisha yanaendelea.

Kwenye mikopo uchawi wake ni riba na miaka ya kulipa tu, ukichemka kufanya maamuzi kwenye haya utasotea mkopo ujute. Ndo mana makonda n madereva wa daladala ukiwachomekea tu utaskia toa gari lako la mkopo cz wanajua wengi hatuwezi afford kununua cash mpaka tuboost na mkopo.

By Albert Man Dea
Instagram & Twitter: @elimu_biashara
 
gari yangu ya kwanza nilinunua kwa savings tu.. sema kazi ilikuwa ya muda mfupi na ilikuwa ina marupurupu hatari..

jamaa kaongea point tupu.... japo kwa mazingira ya siku hizi kupata salary ya kusave laki 5 au 1m kwa mwezi sio shughuli ndogo...

kufanya kitu kikubwa inatakiwa uwe unasave hela nyingi.. ikizidi mwaka mmoja tu utaanza kula hela kabla hujatimiza lengo
 
Saving ni asset mkopo pia ni asset tatizo ni nidhamu ya pesa na matumizi sahihi ya pesa.
 
mkopo ni asset kivipi??? tupe darasa nasi tuelewe
Ngoja nisaidie hapa..mtoa mada amenena vema kama kutoa angalizo tuu..
Kwanza according to Robert kiyosaki..kuna aina mbili za mikopo.good debt na bad debt..good debt ni ile ambayo unachukua then unaenda kuzalisha(so mikopo unalipwa na biashara iliyotokana au iliyoendelezwa na mkopo),na hii ndio maana halisi ya kusema mikopo ni asset(hii ndo inatakiwa but in wachache sana hufanya hivi). Kwa upande mwingine bad debt n mikopo tunayochukua halafu haizalishi chochote(expenses) na hii. Ndo mingi na mibaya kabisa...so ushauri achana na bad debt otherwise itachukue miaka mingi sana.kusogea kiuchumi...
 
Saving ni asset mkopo pia ni asset tatizo ni nidhamu ya pesa na matumizi sahihi ya pesa.
Mkuu unazungumzia Ki Uhasibu au??
Manake Navyojua Mkopo uliochukua (deni) Ki Uhasibu ni Liability, sio Asset.
Ila Mkopo uliompa mtu (Unaodai) ndio asset
 
Back
Top Bottom