Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,628
Ni sehemu kwa jina lingine iliitwa "mama huruma" maana yake ni kuwa; huwezi kupata shida za kudumu.
Kujulikana kwa mji wa Kakola na viunga vyake ni kutokana na uwepo wa mgodi wa Acacia, biashara za maduka ni sababu ya kuwepo kwa mgodi wa Acacia, kuwepo kwa vyombo vya usafiri hadi mabasi ya moja kwa moja Dar ni sababu ya kuwepo kwa mgodi wa Bulyanhulu, majengo ya wafanyakazi yenye ramani za kimagharibi, uwepo wa hospital ya kisasa katika Kijiji cha Bugarama na secondary ya kisasa Bugarama ni sababu ya kampuni ya Acacia na mgodi wa Bulyanhulu. Uwepo wa msongamano mkubwa wa watu maeneo ya vijiji vinavyozunguka ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa kampuni ya Acacia. Kuibwa kwa makinikia na leo mgodi kutangaza kusimamisha wafanyakazi 1200 (kama nilivyotumiwa taarifa kupitia gazeti la Acacia) katika kampuni ya Acacia ni kumbukumbu ya kumkumbuka Mkapa na Jakaya kwa namna walivyokuwa wapiga.................. Msimamo wa raisi Magufuli na huenda kuwa mgumu kushaurika ni mwanzo na mwisho wa Bulyanhulu na ndoto za kuifanya jamii ya Bulyanhulu kuishi kama wenzao wa Ashanti Ghana. Bado naamini kuwa wa Canada na Waustralia si sawa na Wachina ama makaburu watakapopata nafasi katika kuuendesha mgodi huu.
I was a miner and am a miner. Poleni sana wafanyabiashara mlioko Kakola, Bugarama na Ilogi kwani nafahamu kitakachofuata kwani biashara zote zinategemea katikati na mwisho wa mwezi. Poleni pia mliokopa kwenye mabenki. Nitarudi siku nikifukuzwa huku